Nampenda lakini basi

arabianfalcon

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,285
584
Habari zenu waungwa,
Nna jambo langu linaninyima usingizi, Kuna Mpenzi wangu wazamani sana nilidhani alikua ananipenda lakini nimegundua hanipendi au ananitumia tu
nilikua nae kwa mda wa miaka 8, ghafla nilikua na mimba yake akasema hayuko tayari niitoe,kwakua sikua na nia mbaya na yeye nikasikia kua anamtoto wa njee huku akisema nakupenda mpenzi nakupenda, sikutaka hata kumueleza nini kimetokea nimemwandikia ujumbe mfupi kua mimi na yeye basi sababu nimemueleza mdogo wake amenatosha kumueleza lakini maumivu nilionayo anajua Mungu,naombeni msaada wenu,lakini kurudi sitaki.
 
Pole sn...lakn miaka 8 ni mingi sn ulikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kujua msimamo wake mapema zaidi..dah pole bibie
 
Pole dada, jipe moyo, usimtende Mungu dhambi nyingine ya kuitoa hiyo mimba wala usihangaike na hilo limtu lisilojali hisia na maisha ya watu. Simama omba neema ya Mungu ikuvushe hapo salama. Huyo mtoto Mungu akikujalia ndiye atakayekuwa furaha na faraja yako, ndiye atakaye kupenda wewe. Dunia yote yaweza kukugeuka lakini mtoto wako atasema huyu ni mama yangu. Na huyo anayesema umuue sasa atakuwa anayakumbuka hayo maneno yake kila atakaposikia na kumuona huyo mtoto.
 
umeamua kuendelea...ni uamuzi mzuri...tulia kwa muda baada ya hapo tafuta replacement na maisha yaendelee.
 
Pole dada, jipe moyo, usimtende Mungu dhambi nyingine ya kuitoa hiyo mimba wala usihangaike na hilo limtu lisilojali hisia na maisha ya watu. Simama omba neema ya Mungu ikuvushe hapo salama. Huyo mtoto Mungu akikujalia ndiye atakayekuwa furaha na faraja yako, ndiye atakaye kupenda wewe. Dunia yote yaweza kukugeuka lakini mtoto wako atasema huyu ni mama yangu. Na huyo anayesema umuue sasa atakuwa anayakumbuka hayo maneno yake kila atakaposikia na kumuona huyo mtoto.

Pole sana, chukua huu ushauri hapa aliotoa LD.

LD....Ubarkiwe kwa ushauri mzuri.
 
  • Thanks
Reactions: LD
love-quotes-24.jpg

avoid taking deciision by assuming, u will end up loving no body
 
Pole bidada, kuwa mvumilivu katika hiki kipindi lakini usitoe hiyo mimba , na ipo siku baada ya kujifungua huyo mtoto utakuwa mtu wa furaha sana. Hayo ni mapito tu ya hapa duniani, be strong, songa mbele achana nae huyo jamaa asikupandishe presha zisizo na msingi ipo siku atajuta na kukupigia magoti tu!
attachment.php
 
arabianfalcon,
Pole Sana,

Binafsi, siamini sana kuwa unaweza kuwa na mtu kwa Miaka 8, then ujue hakakupenda kwa muda wote huo. I believe aliku/anakupenda.

Umemalizia kwa kusema kurudi hutaki, Inanionyesh aumeshafanya maamuzi. Lakini si vibaya ukifikiria kidogo. If ni sawa naomba uniambie kitu...............

1. Kwa miaka 8 yote mlikuwa wapenzi?, lengo lenu lilikuwa nn?, why hamkufunga ndoa, mlikuwa mnasoma? or what was an obstacle?

2. Ulipata Mimba yake mwaka wa ngapi? and mapenzi yakiwa yameisha or ukiamini yapo?

3. Ulipojua ana mtoto wa nnje ( unamaana gani nnje ya mahusiano yenu?, Je mliishi pamoja?),

4. Mdogo wake ulimueleza nini? and mdogo wake ulimpa taarifa tu au ulifikiri atoe maamuzi fulani?

Get back, hopeful kwa information hizi hata michango ya watu yaweza kuwa fruitful........

Habari zenu waungwa,
Nna jambo langu linaninyima usingizi, Kuna Mpenzi wangu wazamani sana nilidhani alikua ananipenda lakini nimegundua hanipendi au ananitumia tu
nilikua nae kwa mda wa miaka 8, ghafla nilikua na mimba yake akasema hayuko tayari niitoe,kwakua sikua na nia mbaya na yeye nikasikia kua anamtoto wa njee huku akisema nakupenda mpenzi nakupenda, sikutaka hata kumueleza nini kimetokea nimemwandikia ujumbe mfupi kua mimi na yeye basi sababu nimemueleza mdogo wake amenatosha kumueleza lakini maumivu nilionayo anajua Mungu,naombeni msaada wenu,lakini kurudi sitaki.
 
1......Lakini kurudi sitaki.............eeeh na iwe kama upendavyo.
2. Usitoe tena mimba.
 
Asante sana smarter,
Tulikutana pamoja masomoni,mpaka tukawa tunafanya kazi mashirika tofauti,kunipenda alikua ananipenda bila shaka wakati huo nilikua naona.
Nimefikia mamuzi kwa sababu bora angenieleza kua sasa mie na ww basi kuliko kunifanya zuzu,baada yakunitumia kumpa msaada mpaka leo kawa mtu ndio kaona mie sifai kula raha manake nilimstahmilia shida zake, mimba sasa ina miezi 4,nimejua kama ana mtoto wa mwaka msichana alozaa nae ndio alinifata akanambia,niliumia sana manake nilikua Nampenda na nnamuamini sana nikamuliza mdogo wake akasema nikweli na mpaka nguo nilizokua na nunua mie ziko kwa huyo msichana,cha ajabu hata huyo bwana pia amebadilika yani ukiongea nae haizidi 5min atakwambia ntakupigia niko bit busy na hapigi,apana mdogo wake sijamwambia iliatoe mamuzi sababu sikuweza kumuona huyo kaka yake manake ningemuona sijui ningefanya nini kibaya au sijui ingekuwaje,mdogo wake nilimueleza sababu yuko karibu yake sana na atamueleza ili ajue kama najua na sitoweza kurejea kwake tena hata aniombe vipi, na mtoto wangu Inshallah ntamlea najua kama sio rahisi lakini ntajikaza iko siku ntasaha,samahani siwezi kuendelea kuandika kwani inaniuma sana mpaka nalia samahani kama sijajibu kama vile ulivyo tarajia.
 
Mamii usitoe mimba mwaya... Hakuna lisilowezekana chini ya jua. mtoto wako utaweza kumlea vzr tu. Ila usisahau kumuomba Mungu akuondolee stress wakati huu mgumu wa ujauzito... Kwani ukiwa na stress nyingi unaweza kumpoteza mtoto wako mwishowe ukakosa mwana na maji ya moto!.
 
Pole sana dia na be strong na muombe mungu atakupa nguvu tu,mim mwenyewe niko kwenye stress kama yako tena mim nimeish naye 13ys na nimetafuta naye mpaka kawa milioner!so painful tena ila nasali sana ipo siku mungu atajibu tu!
 
we are always doing the mistakes,, wanawake kuamin wanaume,, na kusema la kweli kila mtu na maadili yake yake tu, but kuish na man fo many yrs kama girlfriend and boyfriend s rahis kua na ww milelee mara nyingi ana plan B ktk mawazo yke ,but kilicho tokea ndio kimesha tokea ,be partient ,hiyo n sehemu moja ya maisha,, pengine kuna yr hapiness future on,, pole sana ,kwa yalio tokea,
 
Mh pole sana kwa mambo mazito hayo,ila usikate tamaa lea tu huyo kiumbe wa tumboni,ila huyo jamaa achana naye asije akakujeruhi tena.But next time usijilazimishe kuwa mahali ambapo unahisi kuwa hapana hatima nzuri.Mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba
 
Back
Top Bottom