Mhe. Mpina binafsi nakuvulia kofia kwa hoja zenye mashiko unazozitoa pale Bungeni. Jana wakati wa kupitisha Sheria ya manunuzi Mhe. Mpina alikuwa kinara wa kuishauri Serikali katika vipengele anavyoviona kuwa vinahitaji marekebisho.
Jana alimtoa jasho Waziri wa Fedha kila mara kutoa ufafanuzi kuhusiana na hoja zake. Ilifikia wakati mpaka Waziri wa Fedha anapata jazba kuhusiana na hoja zake ambazo kwa kweli zilikuwa hoja zilizo na mashiko.
Nimeona karibu Wabunge wengi hawapitii hizi sheria kabla hazijaingia Bungeni na jana asilimia 99 walikuwa kimya isipokuwa Jemedari Mhe. Mpina. Mhe. Mpina kwa kweli anasoma na kufanya utafiti ndo maana ushauri wake pengine unawaudhi wahusika.
Mwisho, nikupongeze Mhe. Mpina endelea kuishauri Serikali hata pale unapochukiwa.