juma30

Senior Member
Jun 25, 2022
149
421
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA LA MWAKA 2023 (INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT – IGA, BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE EMIRATE OF DUBAI CONCERNING ECONOMIC AND SOCIAL PARTNERSHIP FOR THE DEVELOPMENT AND IMPROVING PERFORMANCE OF PORTS IN TANZANIA) BUNGENI TAREHE 10 JUNI 2023
1. UTANGULIZI

Tarehe 28 Februari, 2022 Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilisaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Dubai Port World (DP-World) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuhusu uwekezaji katika maeneo ya Bandari nchini. Aidha Tarehe 25 Oktoba, 2022 Serikali ilisaini makubaliano na Serikali ya Dubai (Inter- Governmental Agreement-IGA) kwa ajili ya ushirikiano wa kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini.

Dhamira njema ya Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha kuwa nchi inapata manufaa makubwa kutokana na kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Bandari zetu nchini kama lango kuu la uchumi, jitihada hizi lazima ziungwe mkono na watanzania wote. Nchi yetu ina kiu kubwa ya maendeleo na hivyo ni lazima raslimali zake zitumike kikamilifu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

2. UCHAMBUZI WA MKATABA (IGA)

Nchi yetu iko kwenye mageuzi makubwa ya kiuchumi na inaendelea kuingia mikataba mbalimbali hivyo ni wajibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara na Taasisi zingine za Serikali kuhakikisha kuwa mikataba tunayoingia ina manufaa makubwa kwa Taifa na kamwe tusikubali kuingia mikataba mibovu itakayolinyonya taifa letu na kurudisha nyuma jitihada za kujiletea maendeleo.

Kuhusu Mkataba wa IGA, muda na masaa tuliopewa leo wabunge kupitia Ibara za Mkataba wa IGA na kushauri na baadaye kufanya maamuzi hautoshi kwa jambo kubwa kiasi hiki lakini ninayo maswali kama ifuatavyo:-

(i) Kwanini kama nchi tunaingia mkataba wa IGA katika shughuli za uwekezaji kibiashara katika raslimali za taifa?

(ii) Ni njia gani iliyotumika kuichagua nchi ya Dubai na Kampuni ya DPW katika kuboresha, kuendesha na kuendeleza bandari zetu nchini.

(iii) Kwanini Kampuni ya DPW inatumia mwamvuli wa IGA kuja kuwekeza kibiashara katika Bandari za Tanzania?

(iv) Ni kweli kwamba kama nchi hatukuwa na namna nyingine ya kupata mwekezaji wa kuwekeza katika bandari zetu bila mkataba wa IGA? Mbona hakuna IGA kwenye Mkataba mkubwa wa zaidi ya Tsh. Trilioni 80 wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG) na mikataba mingine mikubwa ya raslimali za nchi ikiwemo madini?

(v) Kazi kubwa ya Mkataba wa IGA kwenye biashara ya Bandari kati ya DPW na TPA ni nini wakati biashara inakwenda kutekelezwa ya HGAs?

(vi) Kampuni ya DPW isingeweza kuwekeza au kufanya biashara na TPA bila mkataba wa IGA?

(vii) Kwanini scope ya mradi haiko specific kwenye mkataba wa IGA inazungumzia maeneo yote ya bandari, bahari na maziwa makuu?

(viii) Tathmini na utafiti gani uliofanywa ndani ya nchi kubaini mahitaji ya uwekezaji katika bandari zetu kabla ya kutafuta mwekezaji?

Hata hivyo nimefanya uchambuzi mdogo katika ibara za mkataba huu na kubaini changamoto zifuatazo, Ibara ya 1, Ibara ya 2, Ibara ya 4 ya mkataba wa IGA ambazo zinaeleza scope ya mradi na uwekezaji unaotarajiwa kufanywa.

2.1 Changamoto katika ibara hizi

(i) IGA inahusisha maeneo yote ya bandari za Bahari ya Hindi na maziwa makuu, hapa IGA ilipaswa kuwa na eneo maalum la uwekezaji ambalo ni Phase 1 badala ya kuyaingiza maeneo yote ya bandari nchi nzima.

(ii) Aina ya uwekezaji unaokwenda kufanywa haujawekwa wazi kwani imeelezwa kiujumla kuwa ni kuendeleza, kusimamia na kuendesha Bandari hali inayoweza kutoa nafasi ya kubinafsisha bandari wakati wa kuandaa HGAs jambo ambalo haliruhusiwi kwa mujibu wa Sheria ya Bandari na. 17 ya Mwaka 2004.

(iii) IGA haijaonyesha Tanzania itanufaika vipi kutoka nchi ya Dubai badala yake inaeleza namna Kampuni ya DPW itakavyokuja kuwekeza kibiashara nchini. Na hapa binafsi nashindwa kuelewa sababu ya kuwepo IGA.

(iv) DPW ilipaswa kupewa kazi kwa utaratibu wa kawaida kupitia TPA na kwa Sheria za Public Private Partnership (PPP) Act na Public Procurement Act, no. 7 of 2011 badala ya kupitia mgongo wa IGA.

(v) IGA ilipaswa kuwa na makubalino ya Tanzania na Dubai pekee badala ya kujumuisha Kampuni ya DPW katika makubaliano ya IGA.

2.2 Changamoto za mkataba katika Ibara zingine.

(i) Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa shughuli za awali za kufanya upembuzi yakinifu na kufanya tathmini
itafanyika baada ya mkataba wa IGA kusainiwa. Upembuzi yakinifu ungebainisha mahitaji bayana na kujua ni mahitaji gani ya fedha yanahitajika na kuepuka kuingia mkataba tusiojua. Lakini pia kuanza kutekelezwa mkataba kabla ya kuridhia ni kinyume cha Kifungu cha 12 cha Sheria ya The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017)

(ii) Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Mkataba nchi yetu itakuwa imejifunga na masharti ya nchi ya Dubai pekee katika kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari zetu nchini kwani ibara hii inazuia mashirikiano na nchi zingine. Tanzania haitaweza kuingia kwenye mikataba mingine hata pale ambapo atatokea mfadhili mwenye masharti mazuri na nafuu na uwezo zaidi ya nchi ya Dubai.

Kwa kuwa scope ya IGA ni bandari zote nchini, Hali hii inaweza kutuingiza kwenye migogoro ya kiplomasia na nchi wahisani ambazo zimekuwa zikitoa misaada na mikopo katika shughuli za maendeleo kwa kuona baadhi ya njia kuu za uchumi tumeanza kuzibinafsisha na kubaguliwa nchi zingine washirika.

Nchi yetu ni kati ya nchi chache duniani zenye ushawishi mkubwa kimataifa tangu Uhuru kutokana na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa letu, Rais wa awamu ya Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Aman Karume katika kulinda uhuru wetu; kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa; kulinda mipaka ya nchi yetu; kutetea haki; kuimarisha ujirani mwema; na kutekeleza Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote kama dira na msimamo wetu kwenye uhusiano na nchi nyingine katika jumuiya ya kimataifa.

Ibara ya 20 kutokutumia Sheria za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro, usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules).

Hapa ifahamike kuwa nchi yetu ndiyo yenye raslimali na nchi ya Dubai na Kampuni zake wanakuja kuwekeza kibiashara hawawezi kupewa ulinzi wa kuvunja Sheria za nchi yetu, Kifungu hicho cha Mkataba kinakwenda kinyume na Kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017) ambapo Kifungu hicho cha Sheria tajwa kinaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia Sheria za Tanzania.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Mnyaa aliridhia kipengele hiki cha mkataba na kusaini huku akijua fika kuwa Sheria za nchi hazimruhusu na leo analishawishi Bunge liridhie Azimio linalovunja Sheria za nchi yetu.

(iv) Ibara ya 23 (4) Mkataba huu ukisharidhiwa hakuna upande utakaoweza kuuvunja katika mazingira ya aina yoyote na hata ikiingiwa hasara ya aina gani, kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba.

Hapa ifahamike kuwa uwekezaji unaofanyika ni katika raslimali za Tanzania na sio Dubai hivyo kitendo cha kuweka zuio la kujitoa kwenye mkataba hata kama hauna tija atakayethirika ni Tanzania ambapo wakati huo atakuwa akinyonywa na hana la kufanya na hii ni kwenda kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017).

(v) Ibara ya 23 (1) ni jambo la hatari kwa taifa kukubali na kuridhia mkataba ambao hauna ukomo wa utekelezaji wake, kifungu kinaeleza kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika au muda kwisha wa HGAs. IGA hii inachukua maeneo yote ya bandari nchini kama ilivyofafanuliwa katika ibara 1, Ibara ya 2 na Ibara ya 4 hivyo ni jambo ambalo haliwezekani kutokuwa na ukomo. Hapa inawezekanaje kumpa Dubai mamlaka makubwa kiasi hicho katika raslimali za nchi yetu.

(vi) Ibara ya 22 inaruhusu marekebisho ya vipengele vya Mkataba baada ya kukubaliana pande zote mbili.
Ibara hii inaipa mamlaka nchi ya Dubai kukataa baadhi ya marekebisho tutakayotaka kufanya kama nchi ambao ndio wenye raslimali za Bandari na hivyo nchi kuendelea kupata hasara ikiwa haina la kufanya. Ndiyo maana nimeuliza mapema nini faida ya IGA katika uwekezaji wa Bandari zetu?

2.3 Kasoro katika utiaji saini mkataba wa IGA

(a) Mkataba wa IGA kutosainiwa kikamilifu, Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini Mkataba huu imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa lakini upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi aliyesaini mkataba kwa niaba ya nchi ya Dubai amepewa Mamlaka na nani jina na cheo havikuwekwa isipokuwa kuna saini pekee inayomtambulisha, H.E Ahmed Mahboob Musabih ( Chief Executive Officer of The Ports, Customs and Free Zone Corporation).

(b) Kwa upande wa Tanzania utiaji saini umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi badala ya kushuhudiwa na Mwasheria Mkuu wa Serikali. Lakini pia Katibu Mkuu aliyeshuhudia hakuweka jina lake kwa upande wa Dubai aliyeshuhudia mkataba huo hajatajwa jina wala cheo chake.

(c) Kwa upande wa Tanzania sehemu ya Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi imesainiwa na sahihi mbili kwa wino wa kijani na wino wa bluu jambo limeleta sintofahamu kubwa kwa watanzania.

Mkataba huu unakosa uhalali wa kisheria kwa mapungufu yaliyopo na hauwezi kuridhiwa na Bunge kwa kuwa haujaidhinishwa kikamilifu (Proper Authorization) na pande zote mbili za Tanzania na Dubai kwa mujibu wa Sheria za Mikataba (International Laws) na kama ilivyosema Ibara ya 28 ya Mkataba kwamba Mkataba unathibitishwa kwa kutiwa saini na Mamlaka za Umma zenye uwezo wa kisheria na zilizopewa Mamlaka na Idhini ya kufanya hivyo. Kukosekana kwa majina na vyeo vya wahusika inaweza kutuingiza katika migogoro ya kisheria katika utekelezaji wa mkataba.

3. CHANGAMOTO ZA KIUJUMLA ZA MKATABA HUU

(1) Ifahamike kuwa IGA inayoingiwa ni kwa ajili ya kuwekeza katika Bandari za Tanzania na sio makubaliano ya uendeshaji wa Bandari za Tanzania na Bandari za Dubai hapa jukumu la nchi ya Dubai halijafahamika bayana ukiondoa makampuni yake yanayokuja kuwekeza nchini. Hivyo kinga inayopewa Kampuni ya DPW kupitia makubaliano ya IGA inaweza kutumika kunyonya raslimali za nchi ya Tanzania kama ulinzi ulitolewa na Ibara ya 7, Ibara ya 8, Ibara ya 20, Ibara ya 22 na Ibara 23 ya Mkataba nk.

(2) Pale nchi ya Dubai ikitokea imekumbwa na migogoro na kuwekewa vikwazo na Jumuiya za Kimataifa nchi yetu itarithi matatizo hayo na kuingia moja kwa moja kwenye matatizo makubwa tusiyohusika nayo.

(3) Suala la kuingia mkataba wa nchi ya Tanzania na nchi ya Dubai ni jambo kubwa ambalo haliwezi kufanywa kwa dharura, linahitaji ushirikishwaji mpana wa wananchi na wabunge kuanzia hatua za awali. Serikali ilipaswa kuleta MoU ambayo iliweka wazi vipengele vinavyokwenda kuandika mkataba badala ya kulishirikisha Bunge wakati mkataba umesainiwa. Mikataba inayohusisha uvunaji na utumiaji wa raslimali na Maliasili za Taifa ni lazima iwe na ushirikishwaji mpana kabla ya kuingiwa.

4. HITIMISHO

Nchi nyingi duniani zinajenga Bandari zake na kushirikiana na sekta binafsi kwa kupangisha na uendeshaji wa bandari huku umiliki wa ardhi na raslimali zingine zote kubaki kuwa mali ya nchi husika.

Taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu ripoti ya PPPLRC Public Private Partnership Legal Resource Centre inaeleza kuwa katika kuchagua njia ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari nchi nyingi zinahusisha sekta binafsi katika upangishaji na uendeshaji huku ardhi na miundombinu yote ya Bandari kubaki mali ya Serikali nanukuu “Different port management structures are used worldwide but in the majority of large and medium sized ports the landlord port model is used. In this model, management responsibilities are delegated to the private sector, while the titles in the land and assets remain with the government”.

Kwa kuwa, Azimio la kuridhia Mkataba wa IGA, kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari za Bahari na Maziwa Makuu ya Tanzania unakwenda kinyume na Sheria za nchi na unakinzana na Sera na Msimamo wa nchi yetu katika Mahusiano ya Kimataifa,

Na kwa kuwa, hakuna utafiti wala tathmini ya kina iliyofanyika kubaini mahitaji ya uwekezaji na fedha zinazohitajika kuboresha bandari zetu na kwa kuwa Mkataba huo haujaweka wazi kiasi cha fedha kinachokwenda kuwekezwa na pia jukumu la nchi ya Dubai halijawekwa wazi katika mkataba huu.
Hivyo Basi, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liazimie yafuatayo:-

(i) Serikali ya Tanzania ishauriane na Serikali ya Dubai ili kufanya marekebisho ya baadhi ya Ibara kama nilivyoanisha hapo juu ili ziendane na Sheria za nchi na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa taifa.

(ii) Kuvunja Mkataba wa IGA na badala yake Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World waingie HGAs ya uendeshaji wa Bandari Gati na. 1 hadi 7 na kwa ujumla miradi inayoainishwa katika Phase 1 Projects.

Nawasilisha.
……………………………………..
Luhaga Joelson Mpina (Mb)
Mbunge wa Jimbo la Kisesa
Source: Mheshimiwa Mpina ashauri makubaliano kati ya Tanzania na DP World
 
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO
Mpina haya yamefanywa deliberately kupiga hela, siyo kuwa haya mapungufu hawayajui, NEVER, wananjua fika kuwa wanauziana nchi yetu Tanganyika kwa mababu zao kwani Samia ni descendant wa waarabu wa Oman.

This is a well calculated move to sell our Tanganyika for the benefit of their families
 
Duh
 
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIU
Mbunge wa Jimbo la Kisesa
Source: Mheshimiwa Mpina ashauri makubaliano kati ya Tanzania na DP World
Naona hataki tena ubunge ifikapo 2025. Wale wote waliochangia 2025 lazima warudi mjengoni...wewe Mpina 2025 karibu benchi tusugue gaga Hadi 2035 Maana 2030 Mwenyekiti atakuwa bado NI yeye...na Mwigulu ndiye atapokea kijiti na Makamba ndiye Waziri Mkuu ajaye
 
Mpina haya yamefanywa deliberately kupiga hela, siyo kuwa haya mapungufu hawayajui, NEVER, wananjua fika kuwa wanauziana nchi yetu Tanganyika kwa mababu zao kwani Samia ni descendant wa waarabu wa Oman.
This is a well calculated move to sell our Tanganyika for the benefit of their families
Mbaya sana hii. Tuache hizi fikra mbaya za kueneza chuki za kibaguzi.🙏🙏🙏
 
Pamoja na kujua kuwa viongozi wa tanzania ni wajinga ila sikuwahi kudhani kuwa ni wajinga kiasi hiki,

Hakika tunatawaliwa na takataka zilizovishwa ubinadamu.

Ccm walishajua walishatulisha limbwata ni mpaka muujiza wa wakoma utokee otherwise yataendelea kutawala miaka nenda miaka rudi haya matakataka.
 
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA LA MWAKA 2023 (INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT – IGA, BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE EMIRATE OF DUBAI CONCERNING ECONOMIC AND SOCIAL PARTNERSHIP FOR THE DEVELOPMENT AND IMPROVING PERFORMANCE OF PORTS IN TANZANIA) BUNGENI TAREHE 10 JUNI 2023
Ningependa kufahamu kutoka kwa nguli wa huu mkataba (ingawa anasema hakuna mkataba ulioingiwa) bi FaizaFoxy, je anachokisema Luhanga Mpina kina mantiki gani kwa mustakabali wa Taifa?

Mpina yupo bungeni, ameona mapungufu kupitia hoja na mwenendo wa serikali juu ya mkataba uliopelekwa kwao waupitishe. Sisi tuliopo mtaani tunazodoana kuwa tunaohoji hatuna akili wala hatuelewi nini tunahoji. Je wabaoutetea tujue mnatetea kitu gani haswa? Mnatetea mkataba au makubaliano?
 
Naona hataki tena ubunge ifikapo 2025. Wale wote waliochangia 2025 lazima warudi mjengoni...wewe Mpina 2025 karibu benchi tusugue gaga Hadi 2035 Maana 2030 Mwenyekiti atakuwa bado NI yeye...na Mwigulu ndiye atapokea kijiti na Makamba ndiye Waziri Mkuu ajaye
Wewe ni Mungu? Nakutahadharisha kuwa hao unaowasema wengi Mungu atawaondoa kabla ya 2030
 
MCHANGO WA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) KUHUSU MAPENDEKEZO YA KURIDHIA MAKUBALIANO KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA DUBAI KUHUSU USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KIJAMII KWA AJILI YA UENDELEZAJI NA UBORESHAJI WA UTENDAJI KAZI WA BANDARI TANZANIA LA MWAKA 2023 (INTERGOVERNMENTAL AGREEMENT – IGA, BETWEEN THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND THE EMIRATE OF DUBAI CONCERNING ECONOMIC AND SOCIAL PARTNERSHIP FOR THE DEVELOPMENT AND IMPROVING PERFORMANCE OF PORTS IN TANZANIA) BUNGENI TAREHE 10 JUNI 2023
1. UTANGULIZI

Tarehe 28 Februari, 2022 Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilisaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Dubai Port World (DP-World) ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Kuhusu uwekezaji katika maeneo ya Bandari nchini. Aidha Tarehe 25 Oktoba, 2022 Serikali ilisaini makubaliano na Serikali ya Dubai (Inter- Governmental Agreement-IGA) kwa ajili ya ushirikiano wa kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari nchini.

Dhamira njema ya Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha kuwa nchi inapata manufaa makubwa kutokana na kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Bandari zetu nchini kama lango kuu la uchumi, jitihada hizi lazima ziungwe mkono na watanzania wote. Nchi yetu ina kiu kubwa ya maendeleo na hivyo ni lazima raslimali zake zitumike kikamilifu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

2. UCHAMBUZI WA MKATABA (IGA)

Nchi yetu iko kwenye mageuzi makubwa ya kiuchumi na inaendelea kuingia mikataba mbalimbali hivyo ni wajibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara na Taasisi zingine za Serikali kuhakikisha kuwa mikataba tunayoingia ina manufaa makubwa kwa Taifa na kamwe tusikubali kuingia mikataba mibovu itakayolinyonya taifa letu na kurudisha nyuma jitihada za kujiletea maendeleo.

Kuhusu Mkataba wa IGA, muda na masaa tuliopewa leo wabunge kupitia Ibara za Mkataba wa IGA na kushauri na baadaye kufanya maamuzi hautoshi kwa jambo kubwa kiasi hiki lakini ninayo maswali kama ifuatavyo:-

(i) Kwanini kama nchi tunaingia mkataba wa IGA katika shughuli za uwekezaji kibiashara katika raslimali za taifa?

(ii) Ni njia gani iliyotumika kuichagua nchi ya Dubai na Kampuni ya DPW katika kuboresha, kuendesha na kuendeleza bandari zetu nchini.

(iii) Kwanini Kampuni ya DPW inatumia mwamvuli wa IGA kuja kuwekeza kibiashara katika Bandari za Tanzania?

(iv) Ni kweli kwamba kama nchi hatukuwa na namna nyingine ya kupata mwekezaji wa kuwekeza katika bandari zetu bila mkataba wa IGA? Mbona hakuna IGA kwenye Mkataba mkubwa wa zaidi ya Tsh. Trilioni 80 wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG) na mikataba mingine mikubwa ya raslimali za nchi ikiwemo madini?

(v) Kazi kubwa ya Mkataba wa IGA kwenye biashara ya Bandari kati ya DPW na TPA ni nini wakati biashara inakwenda kutekelezwa ya HGAs?

(vi) Kampuni ya DPW isingeweza kuwekeza au kufanya biashara na TPA bila mkataba wa IGA?

(vii) Kwanini scope ya mradi haiko specific kwenye mkataba wa IGA inazungumzia maeneo yote ya bandari, bahari na maziwa makuu?

(viii) Tathmini na utafiti gani uliofanywa ndani ya nchi kubaini mahitaji ya uwekezaji katika bandari zetu kabla ya kutafuta mwekezaji?

Hata hivyo nimefanya uchambuzi mdogo katika ibara za mkataba huu na kubaini changamoto zifuatazo, Ibara ya 1, Ibara ya 2, Ibara ya 4 ya mkataba wa IGA ambazo zinaeleza scope ya mradi na uwekezaji unaotarajiwa kufanywa.

2.1 Changamoto katika ibara hizi

(i) IGA inahusisha maeneo yote ya bandari za Bahari ya Hindi na maziwa makuu, hapa IGA ilipaswa kuwa na eneo maalum la uwekezaji ambalo ni Phase 1 badala ya kuyaingiza maeneo yote ya bandari nchi nzima.

(ii) Aina ya uwekezaji unaokwenda kufanywa haujawekwa wazi kwani imeelezwa kiujumla kuwa ni kuendeleza, kusimamia na kuendesha Bandari hali inayoweza kutoa nafasi ya kubinafsisha bandari wakati wa kuandaa HGAs jambo ambalo haliruhusiwi kwa mujibu wa Sheria ya Bandari na. 17 ya Mwaka 2004.

(iii) IGA haijaonyesha Tanzania itanufaika vipi kutoka nchi ya Dubai badala yake inaeleza namna Kampuni ya DPW itakavyokuja kuwekeza kibiashara nchini. Na hapa binafsi nashindwa kuelewa sababu ya kuwepo IGA.

(iv) DPW ilipaswa kupewa kazi kwa utaratibu wa kawaida kupitia TPA na kwa Sheria za Public Private Partnership (PPP) Act na Public Procurement Act, no. 7 of 2011 badala ya kupitia mgongo wa IGA.

(v) IGA ilipaswa kuwa na makubalino ya Tanzania na Dubai pekee badala ya kujumuisha Kampuni ya DPW katika makubaliano ya IGA.

2.2 Changamoto za mkataba katika Ibara zingine.

(i) Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa shughuli za awali za kufanya upembuzi yakinifu na kufanya tathmini
itafanyika baada ya mkataba wa IGA kusainiwa. Upembuzi yakinifu ungebainisha mahitaji bayana na kujua ni mahitaji gani ya fedha yanahitajika na kuepuka kuingia mkataba tusiojua. Lakini pia kuanza kutekelezwa mkataba kabla ya kuridhia ni kinyume cha Kifungu cha 12 cha Sheria ya The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017)

(ii) Kwa mujibu wa Ibara ya 27 ya Mkataba nchi yetu itakuwa imejifunga na masharti ya nchi ya Dubai pekee katika kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya bandari zetu nchini kwani ibara hii inazuia mashirikiano na nchi zingine. Tanzania haitaweza kuingia kwenye mikataba mingine hata pale ambapo atatokea mfadhili mwenye masharti mazuri na nafuu na uwezo zaidi ya nchi ya Dubai.

Kwa kuwa scope ya IGA ni bandari zote nchini, Hali hii inaweza kutuingiza kwenye migogoro ya kiplomasia na nchi wahisani ambazo zimekuwa zikitoa misaada na mikopo katika shughuli za maendeleo kwa kuona baadhi ya njia kuu za uchumi tumeanza kuzibinafsisha na kubaguliwa nchi zingine washirika.

Nchi yetu ni kati ya nchi chache duniani zenye ushawishi mkubwa kimataifa tangu Uhuru kutokana na misingi imara iliyowekwa na Waasisi wa Taifa letu, Rais wa awamu ya Kwanza, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Aman Karume katika kulinda uhuru wetu; kujiamulia mambo yetu wenyewe bila kuingiliwa; kulinda mipaka ya nchi yetu; kutetea haki; kuimarisha ujirani mwema; na kutekeleza Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote kama dira na msimamo wetu kwenye uhusiano na nchi nyingine katika jumuiya ya kimataifa.

Ibara ya 20 kutokutumia Sheria za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro, usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules).

Hapa ifahamike kuwa nchi yetu ndiyo yenye raslimali na nchi ya Dubai na Kampuni zake wanakuja kuwekeza kibiashara hawawezi kupewa ulinzi wa kuvunja Sheria za nchi yetu, Kifungu hicho cha Mkataba kinakwenda kinyume na Kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017) ambapo Kifungu hicho cha Sheria tajwa kinaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia Sheria za Tanzania.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa Mnyaa aliridhia kipengele hiki cha mkataba na kusaini huku akijua fika kuwa Sheria za nchi hazimruhusu na leo analishawishi Bunge liridhie Azimio linalovunja Sheria za nchi yetu.

(iv) Ibara ya 23 (4) Mkataba huu ukisharidhiwa hakuna upande utakaoweza kuuvunja katika mazingira ya aina yoyote na hata ikiingiwa hasara ya aina gani, kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba.

Hapa ifahamike kuwa uwekezaji unaofanyika ni katika raslimali za Tanzania na sio Dubai hivyo kitendo cha kuweka zuio la kujitoa kwenye mkataba hata kama hauna tija atakayethirika ni Tanzania ambapo wakati huo atakuwa akinyonywa na hana la kufanya na hii ni kwenda kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act no.5 of 2017).

(v) Ibara ya 23 (1) ni jambo la hatari kwa taifa kukubali na kuridhia mkataba ambao hauna ukomo wa utekelezaji wake, kifungu kinaeleza kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika au muda kwisha wa HGAs. IGA hii inachukua maeneo yote ya bandari nchini kama ilivyofafanuliwa katika ibara 1, Ibara ya 2 na Ibara ya 4 hivyo ni jambo ambalo haliwezekani kutokuwa na ukomo. Hapa inawezekanaje kumpa Dubai mamlaka makubwa kiasi hicho katika raslimali za nchi yetu.

(vi) Ibara ya 22 inaruhusu marekebisho ya vipengele vya Mkataba baada ya kukubaliana pande zote mbili.
Ibara hii inaipa mamlaka nchi ya Dubai kukataa baadhi ya marekebisho tutakayotaka kufanya kama nchi ambao ndio wenye raslimali za Bandari na hivyo nchi kuendelea kupata hasara ikiwa haina la kufanya. Ndiyo maana nimeuliza mapema nini faida ya IGA katika uwekezaji wa Bandari zetu?

2.3 Kasoro katika utiaji saini mkataba wa IGA

(a) Mkataba wa IGA kutosainiwa kikamilifu, Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini Mkataba huu imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa lakini upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi aliyesaini mkataba kwa niaba ya nchi ya Dubai amepewa Mamlaka na nani jina na cheo havikuwekwa isipokuwa kuna saini pekee inayomtambulisha, H.E Ahmed Mahboob Musabih ( Chief Executive Officer of The Ports, Customs and Free Zone Corporation).

(b) Kwa upande wa Tanzania utiaji saini umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi badala ya kushuhudiwa na Mwasheria Mkuu wa Serikali. Lakini pia Katibu Mkuu aliyeshuhudia hakuweka jina lake kwa upande wa Dubai aliyeshuhudia mkataba huo hajatajwa jina wala cheo chake.

(c) Kwa upande wa Tanzania sehemu ya Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi imesainiwa na sahihi mbili kwa wino wa kijani na wino wa bluu jambo limeleta sintofahamu kubwa kwa watanzania.

Mkataba huu unakosa uhalali wa kisheria kwa mapungufu yaliyopo na hauwezi kuridhiwa na Bunge kwa kuwa haujaidhinishwa kikamilifu (Proper Authorization) na pande zote mbili za Tanzania na Dubai kwa mujibu wa Sheria za Mikataba (International Laws) na kama ilivyosema Ibara ya 28 ya Mkataba kwamba Mkataba unathibitishwa kwa kutiwa saini na Mamlaka za Umma zenye uwezo wa kisheria na zilizopewa Mamlaka na Idhini ya kufanya hivyo. Kukosekana kwa majina na vyeo vya wahusika inaweza kutuingiza katika migogoro ya kisheria katika utekelezaji wa mkataba.

3. CHANGAMOTO ZA KIUJUMLA ZA MKATABA HUU

(1) Ifahamike kuwa IGA inayoingiwa ni kwa ajili ya kuwekeza katika Bandari za Tanzania na sio makubaliano ya uendeshaji wa Bandari za Tanzania na Bandari za Dubai hapa jukumu la nchi ya Dubai halijafahamika bayana ukiondoa makampuni yake yanayokuja kuwekeza nchini. Hivyo kinga inayopewa Kampuni ya DPW kupitia makubaliano ya IGA inaweza kutumika kunyonya raslimali za nchi ya Tanzania kama ulinzi ulitolewa na Ibara ya 7, Ibara ya 8, Ibara ya 20, Ibara ya 22 na Ibara 23 ya Mkataba nk.

(2) Pale nchi ya Dubai ikitokea imekumbwa na migogoro na kuwekewa vikwazo na Jumuiya za Kimataifa nchi yetu itarithi matatizo hayo na kuingia moja kwa moja kwenye matatizo makubwa tusiyohusika nayo.

(3) Suala la kuingia mkataba wa nchi ya Tanzania na nchi ya Dubai ni jambo kubwa ambalo haliwezi kufanywa kwa dharura, linahitaji ushirikishwaji mpana wa wananchi na wabunge kuanzia hatua za awali. Serikali ilipaswa kuleta MoU ambayo iliweka wazi vipengele vinavyokwenda kuandika mkataba badala ya kulishirikisha Bunge wakati mkataba umesainiwa. Mikataba inayohusisha uvunaji na utumiaji wa raslimali na Maliasili za Taifa ni lazima iwe na ushirikishwaji mpana kabla ya kuingiwa.

4. HITIMISHO

Nchi nyingi duniani zinajenga Bandari zake na kushirikiana na sekta binafsi kwa kupangisha na uendeshaji wa bandari huku umiliki wa ardhi na raslimali zingine zote kubaki kuwa mali ya nchi husika.

Taarifa ya Benki ya Dunia kuhusu ripoti ya PPPLRC Public Private Partnership Legal Resource Centre inaeleza kuwa katika kuchagua njia ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari nchi nyingi zinahusisha sekta binafsi katika upangishaji na uendeshaji huku ardhi na miundombinu yote ya Bandari kubaki mali ya Serikali nanukuu “Different port management structures are used worldwide but in the majority of large and medium sized ports the landlord port model is used. In this model, management responsibilities are delegated to the private sector, while the titles in the land and assets remain with the government”.

Kwa kuwa, Azimio la kuridhia Mkataba wa IGA, kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Bandari za Bahari na Maziwa Makuu ya Tanzania unakwenda kinyume na Sheria za nchi na unakinzana na Sera na Msimamo wa nchi yetu katika Mahusiano ya Kimataifa,

Na kwa kuwa, hakuna utafiti wala tathmini ya kina iliyofanyika kubaini mahitaji ya uwekezaji na fedha zinazohitajika kuboresha bandari zetu na kwa kuwa Mkataba huo haujaweka wazi kiasi cha fedha kinachokwenda kuwekezwa na pia jukumu la nchi ya Dubai halijawekwa wazi katika mkataba huu.
Hivyo Basi, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liazimie yafuatayo:-

(i) Serikali ya Tanzania ishauriane na Serikali ya Dubai ili kufanya marekebisho ya baadhi ya Ibara kama nilivyoanisha hapo juu ili ziendane na Sheria za nchi na kuleta manufaa makubwa zaidi kwa taifa.

(ii) Kuvunja Mkataba wa IGA na badala yake Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World waingie HGAs ya uendeshaji wa Bandari Gati na. 1 hadi 7 na kwa ujumla miradi inayoainishwa katika Phase 1 Projects.

Nawasilisha.
……………………………………..
Luhaga Joelson Mpina (Mb)
Mbunge wa Jimbo la Kisesa
Source: Mheshimiwa Mpina ashauri makubaliano kati ya Tanzania na DP World
Dah kama haya yote yapo ilikuaje waziri akasaini kwa haraka sana ivo kama hana agenda binafsi yakizungumzwa mambo ya zanzibar inaweza kuonekana ni ubinafsi na watu wanaroho mbaya ila kiukweli wanatukosea sana
 
Back
Top Bottom