Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

To yeye ,,,,najua tumekuwa na utani wa kimapenzi humu ndani kama kuitana wapenzi na makopakopa lkn kwa ajili ya kufurahi tu na mwisho siku inapita.

Kwa roho safi kabisa nashauri kubali kuolewa na huyo mwamba nahisi ana roho nzuri kama yangu, na kama anapenda watoto wako hiyo ni point kubwa mno

Wakati mwingine tunakosa mambo mazuri kwasababu ya hofu zisizo za msingi, ishinde hiyo hali kwa kuamini kila kitu kitaenda kuwa sawa

Kama unaamini he is the one basi usiuweke usiku olewa na huenda ukaja kufurahia maisha ya ndoa ambayo hukuyapata hapo kabla

Nimekupa baraka zangu zote

Mpenzi wako wa zamani wa jf
Etugrul bey
Ubarikiwe sana love
 
Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu
Yaani pointi moja kubwa sana! Ukiona ndugu wa upande mmoja hawakubaliana na ndoa yenu, hiyo ndoa haitadumu!! Kutakuwa na vita na uchonganishi sio wa nchi hii! Watahakikisha hiyo ndoa inakufa!! Take care!!

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Ndoa ngumu mkuu,Mwenyezi Mungu awapambanie sana.Asante sana
Hapa namjibu mtu aliyeuliza kuwa mliona red flags na bado mkaoana? Ni hivi: Mtu kama hajaingia kwenye ndoa hawezi kujua mambo mengi. Kuna viashiria unaweza kuviona kabla hamjafunga ndoa ukavipuuza lakini baada ya ndoa ndiyo vinakuwa dhahiri na unavikumbuka. BTW hata mimi ni me na nimepitia sokomoko kama ulizopitia hivyo nakuelewa sana. Ushauri wangu ni kuwa chukuwa muda kumsoma. Usiogope kuchewa. Bora hata muwe marafiki kwa miaka miwili ili kupimana.
 
Ni kweli Kabisa mkuu
 
Ukitaka udumu na huyo mchumba wako wa sasa hakikisha hao watoto wako uliowapata katika ndoa yako ya kwanza hawakai na nyie (mumeo na wewe).

Kwakuwa umri wako umesonga (naamini hivyo) kutokana na maelezo yako kuwa ulishaolewa ukatalikiana na x wako, basi tumia hili kama sehemu ya kujifunza na kujirekebisha kwa yale unayojua ni wazi hayafai kumfanyia mwenza wako.
 
Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu
Masingo maza nawaomba muachane na habari ya kuolewa, muendelee kuwa mali yetu sote. Tuendelee kuwafaidi zamu kwa zamu
 
Ukitaka udumu na huyo mchumba wako wa sasa hakikisha hao watoto wako uliowapata katika ndoa yako ya kwanza hawakai na nyie (mumeo na wewe).

Kwakuwa umri wako umesonga (naamini hivyo) kutokana na maelezo yako kuwa ulishaolewa ukatalikiana na x wako, basi tumia hili kama sehemu ya kujifunza na kujirekebisha kwa yale unayojua ni wazi hayafai kumfanyia mwenza wako.
Sikuzote sipo nao
 
Back
Top Bottom