Nakuwa na maamuzi ya kusitasita kuolewa tena tangu ndoa ya kwanza inishinde 2021

uasherati ni Kitendo cha kufanya tendo la NDOA nje ya utaratibu Yaani nje ya NDOA Kwaiyo aliposema isipokua kwa habari ya uasherati alimaanisha kwa watu ambao Bado hawajaunganishwa kwa NDOA takatifu mfano wa wachumba mmoja wao akitenda ngono hiyo ni halali kutengana Lakini sio kwa Wanandoa waliofunga NDOA takatifu
Hapo nadhani tafsiri hujaiweka sawa mkuu. Afanyaye uasherati ni yule aendaye nje ya ndoa, ilhali yuko na ndoa.

Na hili ni swali aliulizwa Yesu juu ya maswala ya talaka na jinsi watu walivyoishi chini ya sheria za Musa.

Ukiangalia hapo, kiimani mtu anayetengana na mke au mume, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, naye akaenda kuolewa/kuoa na mtu mwingine, basi yule aoae au anayeolewa anafanya zinaa/kuzini.
 
Yeah, nishawahi olewa lakini ndoa yetu ilikuwa ni nusu nichinjwe....ndoa ilikuwa na changamoto nyingi Kabla ya kuoana na baada ya kuoana.....

Kiufupi ilikuwa ni ndoa ambayo katika uchumba ilitupa ishara zote kwamba tunaforce.....(vipingamizi toka kwa ndugu...) lakini tukaangalia siye twapendana imetosha.(Kumbe tulikuwa tunajidanganya ndugu ni sehemu kubwa ya maisha ya ndoa).....hivyo hatukutoboa tukapeana, talaka maana ikawa vita sasa ya Israel na Ukraine.

Nina watoto wawili, nimepata mchumba mjasiriamali....sasa kufanya maamuzi ya kuingia tena ndani ya ndoa naogopa....si mchumba wa kwanza kumpata yaan wakifikia stage ya kwenda kujitambulisha lazima niingize chokochoko tugombane tutengane....naogopa mwenzenu....naogopa nilitaka kuuawa na mtu niliyemwamini....naogopa kumtumikia mume tena....naogopa ndugu wa mume watakuwaje katika maisha yetu....naiogopa ndoa ndugu yenu😭

Naomba ushauri nilee wanangu hawa niliopewa na Mwenyezi Mungu au niingie tena kwenye ndoa na huyu mchumba...kiufupi Kaka wa watu hana makuu...ni mtu mwema tu na anastahili.

Majibu yote napokea ndugu zangu🙏🏽
Tuanzie hapa.

Ugomvi na ndugu wa mume wako ulikuwa kisa nini?
 
Je sasa hivi mahusiano mapya bado unafosi kama yale ya awali?
 
Tuliiva ila ndugu hawakuiva hawakutaka Kabisa tuoane mkuu...tukaforce na ndoa ikafungwa
Hao ndugu sidhani kama ndio sababu ya nyie kutodumu , changamoto kama ulivyosema ilikuwa Kati yenu wawili, ndugu Wana mchango mdogo sana kwenye ustawi au anguko lenu, sehemu kubwa mlichangia wenyewe either kwa kujua au kutofahamu
 
Yupo jf??
Kama yupo mtag..

Nimefurahi sana kuona umeandika uzi leo ticha.

Hizi avatar zako bado naziunganisha kupata sura yako kamili, kesho badili uweke jicho jingine.
 
Yaani ndugu anavunjaje ndoa ya watu wengine? Hii kitu huwa nashindwa kuelewa kabisa.

Huenda huyo mumewe wa zamani hana misimamo thabiti badala yake ni mtu wa kusikiliza ndugu na kufanyia kazi maelekezo yao.

Yaani mpendane kabisa halafu eti ndugu wasababishe mpeane talaka?

Big NO. Hata nyie hamkuwa na upendo wa dhati ndiyo maana ndugu wakawasambaratisha kiwepesi.
💯
 
Back
Top Bottom