yaani mtu wa pwani wee acha tu.si unaona rekodi ya marehemu dr omer ali juma and hivi sasa ya dr ali mohd shein.
Siyo vizuri kulaumu. Ingekuwa vizuri ukapendekeza mtu au watu kutoka Zanzibar ambao wanauwezo sawa au zaidi. Hatuwezi ku compromise kwa sababu anatoka sehemu fulani.
mkuu mbona kuna vichwa vikali tu zenji viloenda shule,tena sio shule PUMBAVU za kugaiwa vyeti,mkuu kule kuna watu wapo SMZ wamekula HARVARD etc na wana first class CPA,masuala ya BANKING ndio wanayatesa kinoma plus working experienced.
Kweli yakhe haki wanayo lakini ukumbuke BoT ilikuwa sio part ya muungao, si unajuwa muungano wetu wa usanii sanii. Visiwani kuna Peoples Bank of Zanzibar iliyokuwa ikishughulikia mambo hayo yanayofanywa na BoT huku bara. Mpaka recently ilivyosambaratishwa. Kwa hiyo BoT si muda mrefu sana toka iwe inashughulikia mambo ya visiwani pia. Lakini, nadhani jengo la BoT pale Zanzibar lipo tayari na lazima litakuwana ofisi ya gavana kwa hiyo ni mwanzo mzuri.Watanzania wa Visiwani wana haki kuuliza juu ya haya mambo- tusitoke kwenye hoja Visiwani ni sehemu ya Muungano!
Kama kuna wanaotoka Visiwani na wanaqualify- hoja ni kwa nini tangu 1966 tangu BoT kuanzishwa hajateuliwa gavana yoyote toka Visiwani?
Mimi naona ni hoja yenye nguvu! Tusitoke nje kwa kuwa na maneno ya kejeli kwa hii hoja unecessarily!
Majibu ya kihuni ya hii hoja- not fair? We can argue better!
Kweli yakhe haki wanayo lakini ukumbuke BoT ilikuwa sio part ya muungao, si unajuwa muungano wetu wa usanii sanii. Visiwani kuna Peoples Bank of Zanzibar iliyokuwa ikishughulikia mambo hayo yanayofanywa na BoT huku bara. Mpaka recently ilivyosambaratishwa. Kwa hiyo BoT si muda mrefu sana toka iwe inashughulikia mambo ya visiwani pia. Lakini, nadhani jengo la BoT pale Zanzibar lipo tayari na lazima litakuwana ofisi ya gavana kwa hiyo ni mwanzo mzuri.
Pia nakumbushia tuu, mboni smz inawasahau sana wa pemba kwa nyadhifa mbali mbali hapo visiwani? tena ukikumbuka kwamba wa pemba ni vichwa yaani wengi wamesoma sana lakini ndio hivyo tena, hawatambuliki sijui au wanabaguliwa, ndio yale yale kama walivyo baguliwa wangazija wasomi ndio yanayojiri kwa wapemba hii leo.
mimi si mpemba yakhe, lakini ukweli ni huo, au system huijuwi wewe?
Tatizo la mishahara hewa lipo Zenj, na wizara yenye usugu wa suala hilo ni Wizara ya Afya...Mzalendohalisi,
Hata Z'bar kumejaa ufisadi. Juzi namsikia Mhe Karume akisema kumekuwa na malipo ya mishahara kwa watu ambao walishafariki miaka nenda rudi. Nani alikuwa anafaidi mishahara hiyo?
Rais Amani Karume nae ni fisadi kapora fukwe nyingi zenj....
Hii si kweli, imekaa ka hadithi za kijiweni, By the way Mwinyi Sadalah(Nipashe) yamemkuta kwa kushabikia hadithi kama hizi...
Kama unaona yupo mtaje!