Nakuuliza hivi Mheshimiwa JK...

Yamemkuta mepi, yakhe?

Kesi yake hii hapa ...

JALADA la kesi inayomkabili mwandishi wa habari wa magazeti ya ‘Nipashe’ na ‘The Guardian’, Mwinyi Sadallah, limerejeshwa kwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Mgharibi, Said Marekano.
Mwendesha Mashitaka katika kesi hiyo, Mgeni Jailan, jana aliomba mahakama iahirisha kesi hiyo, kwa vile jalada la kesi hiyo bado halijarejeshwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kutoka kwa Mkuu huyo wa Upelelezi mkoa.

Akijibu ombi hilo, wakili wa Sadallah, Hamid Mbwezeleni, alimwomba hakimu kupanga kesi hiyo kwa kuzingatia muda muafaka.

Baada ya kupokea maombi hayo, hakimu Rabia Hussein Mohammed aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 24, mwaka huu.

Mwandishi huyo amefunguliwa mashitaka pamoja na mkulima Ramadhan Mohammed Vuai, mkazi wa Kijiji cha Chwaka, Wilaya ya Kati Unguja.

Katika kesi hiyo, Sadallah, mshitakiwa namba moja, anatuhumiwa kuandika habari za uongo na kumkashifu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume.

Watuhumiwa hao wako nje kwa dhamana ya sh 300,000 kila mmoja na wadhamini wawili kwa kiwango kama hicho cha fedha kwa maandishi.

Inadaiwa kuwa Sadallah alitenda kosa hilo Septemba 22 na 24, mwaka jana, kinyume na kifungu cha 48 (1) (c) na kifungu cha 47 (1) (a) cha sheria ya usajili wa mawakala wa habari, Magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988.

Kwa upande wake, anakabiliwa na shitaka la kutoa maneno ya uchochezi kinyume na kifungu cha 48 (1) (b) na 47 (1) (a) cha sheria ya usajili wa mawakala wa habari, magazeti na vitabu namba 5 ya mwaka 1988. Watuhumiwa wote walikana mashitaka yao.
 
Hodi!

Naomba mtu atautajie majina ya mgavana waliopita, anatoka wapi, kabila gani, amesoma wapi, anajinsia gani n.k. Wengine hatuchunguzagi hayo hivyo hatujui!!
 
Aliyasema marehemu Julius Nyerere kwamba mkianza utanganyika na uzanzibari, mtaendelea hadi kwa upemba na uunguja, uDSM na uDodoma na hatimae mtaishia kwa ukabila.!!
Let us first fight our common enemy - ufisadi
 
Aliyasema marehemu Julius Nyerere kwamba mkianza utanganyika na uzanzibari, mtaendelea hadi kwa upemba na uunguja, uDSM na uDodoma na hatimae mtaishia kwa ukabila.!!
Let us first fight our common enemy - ufisadi
Mfano wa karibu wa dhambi ya ukabilia angalia hapo kwa jirani zetu, ama kuhusu Ufisadi, huo umebarikiwa na "Azimo la Zanzibar"
 
Mmekosa swali la kuuliza...Basi Hata Deleva wa Raisi Lazima Atoke Bara kwasababu alie Pita alikua Mzanzibari..
 
Mmekosa swali la kuuliza...Basi Hata Deleva wa Raisi Razima Atoke Bara kwasababu alie Pita alikua Mzanzibari..

Itakuwa heri akitoka Bara sasa,manake aliyetoka mpaka leo anadai mafao yake..
 
hilo ni tatizo la muungano wa serikali mbili!
zanzibar haiwezi kufananishwa na kinondoni japo kuwa ina watu wachache, kwa vile kinondoni haijawahi kuwa nchi, na zanzibar ni nchi iliyokuwa na serikali.

ukifananisha zanzibar na kinondoni sawa na kufananisha mzee mtu mzima aloa mke kijana, asimpe haki zake kama partner wake, amwambie wewe sawa na mwanangu mmoja kwa umri!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom