Dickson Mpemba
JF-Expert Member
- Jan 21, 2010
- 353
- 151
Nimepokea taarifa za baadhi ya wanahisa wenzangu wanaomba Dr Kimei aendelee kama Mkurugenzi Mtendaji kwa mshangao mkubwa na masikitiko.
1. Dr Kimei amekua mkurugenzi mtendaji wa CRDB kwa takribani miaka 20 sasa.
Yaani toka muhula wa kwanza wa Mkapa, mihula miwili ya Kikwete na sasa muhula wa kwanza wa Magufuli. Yaani toka Gavana Dr Idris Rashid, Mpaka Dr Balali, Mpaka Prof Ndulu na sasa Prof Luoga. Yaani toka wakati wa benki zisizo zaidi ya 10 mpaka sasa mabenki ya 57. Yaani toka wakati simu ni Tritel na TTCL mpaka sasa enzi za Mpesa, Tigo pesa na airtel money.
Hili sio jambo zuri kwa utamaduni wa kikampuni na utawala bora (Corporate Culrure and Governance). Kampuni hupaswa kua na utofauti wa menejimenti wa muda hadi muda kwa manufaa ya kibiashara na hata katika misingi ya utawala bora wa uendeshaji.
Nchi sio Benki. Lakini Hata katiba za nchi na taasisi mbali mbali kidemokrasia zinatambua hili. Hutoa nafasi kwa mtu kurudia uongozi mara kadhaa na kisha anapisha wengine. Ukomo wa muda katika uongozi flani na kuleta uongozi mpya kabisa ni kama kubonyeza refresh ama kuzima na kuwasha upya gari. Gari hili la CRDB kwa miaka 20 halijawahi kuzimwa ili tufungue mbele na tuchunguze vizuri chini ya boneti. Je? injini za mikakati na mauzo ziko sawa ama ni mbwembwe na uzoefu wa dereva unalolikongoja mbele. Je? breki za utawala bora na misingi ya usimamizi wa fedha zinafanya kazi ama ufundi na umahiri wa dereva ndio unatawala? Je hali ya ufanisi wa injini ni kama rangi nzuri za matangazo lukuki na nyimbo bwerere tunazoona kwa nje ya gari?
Bila kubadilisha uongozi wanahisa wenzangu tutajuaje kama kuna hizo shida na kuzitatua?
2. Bila kushangaza, na kwa kuegemea kabisa CRDB ni kati ya benki zimekua na viashiria vya kutokua na utawala bora mzuri. Jumla ya Mikopo mibaya ya CRDB peke yake ni TZS 459 Bil asilimia 14.54 ya mikopo yao yote. Hii ni juu ya kikomo cha asilimia 5 kilichowekwa na BOT. Robo ya mikopo isiolipika ya soko lote ni ya CRDB peke yake.
Misingi ya mikopo mibovu haichezi mbali na utawala bora wa mfumo mzima wa ukopeshaji. Leo tunashangilua uongozi huu uendelee zaidi?
3. Mkakati wa benki hii hauleweki eleweki. Baada ya mwanzo mzuri sana na mageuzi makubwa sifa na mafanikio haya yakazaa kubweteka na ubeberu. Zikaja EPA, Ikaja Mikopo ya mashaka kwenye kilimo hasa Pamba na matatizo mengineyo. Kwa sasa wapo kwenye kila kitu bila hasa mantiki thabiti ya ufanisi. Mara waje na bidhaa hii mara ile. Mara wajenge mabranch kisiasa na kuongeza mabranch kipindi wenzau wanapunguza. Mara wako china desk, mara hiki mara kile.
Ndugu wanahisa wenzangu wa CRDB bila shaka Dr Kimei ametuoa sehemu flani na kuchangia sana ukuaji na historia ya benki yetu. Neno kuu hapa ni "yetu", benki inapasa kuwa yetu na si yake (japokua inasemekana ana hisa kwa mbadala). Tunahitaji Kiongozi mpya mwenye mkakati mahiri zaidi kutupeleka mbele. Kama bodi ya CRDB 1998 ingekomaa na wakuregenzi hao hao kwa maslahi binafsi ama maono finyu tungeonja wapi matunda ya kazi za Dr Kimei. Na je CRDB isiwe na maisha baada ya Kimei, la hasha!
Sasa basi kazi yake nzuri au la iizinishwe na kujaribiwa kwa kutazamwa kutumia nyakati asiekuwepo yeye kama kiongozi.
Apishe na ajikite kutuletea jembe haswa. Si la kuficha maovu yake bali la kupeleka taasisi hii nyeti sana kwa maendeleo ya Tanzania Juu na juu zaidi. Akuze mitaji yetu wanahisa.
Nawasilisha.