Nakupenda mwalimu

BIN BOR

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,013
407
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mtendeni alipiga picha ya pamoja na wanafunzi wote wa shule yake, akasafisha kopi kibao na kuhamasisha watoto wote wanunue. Akapiga debe akisema:-

"Hebu fikiria, mtakapokuwa wakubwa mtaangalia picha hii na kusema 'ona, huyu ni Juma, sasa ni waziri wa elimu, ona, huyu ni Pendo, waziri mkuu' kwa hiyo nataka wote mnunue nakala ya picha hii kama kumbu kumbu."

Mtoto mmoja akagoma kununua na akamwambia mwalimu, " Mimi siwezi kununua kwa sababu nakupenda mwalimu. Wakati tutakapokuwa tunaoneshana mawaziri na wakurugenzi, wengine watasema' Ona, huyu ndiye mwalimu mkuu wetu, sasa ni marehemu........"

Mwalimu akadondoka, akazimia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom