Nahisi nimetongoza jini

Hivi Jini , shetani na mzimu wa babu. Hivi ni vitu tofauti au vyote ni vimoja na viko wapi
 
Tumebadilishiwa mke saloon.hiyo ya jini afadhali yaweza elezeka.
 
Nazikubali sana horrors,oi mtoa mada hebu msogeze huyo shemeji atakuwa jini kweli ili nimuwekee playlist nyingine huku.Tutaanza na "The Teeth"
 
Kuna moja matata...
"The hills have eyes " hama sijakosea..... ni nouma
 
Me nadhani hapo hofu sio kung'atwa.Kikubwa asije akawa ni kidume kimejigeuza halafu baadae akugeukie afanye yake kwako.
 
Hakika kilikuwa kipindi kigumu sana ila alhamdulillah kimepita salama na sasa maisha yanaendelea.

Tuachane na hayo, tulijadili hili ninaloliwasilisha hapa jamvini.
Mwenzenu huu msimu wa uchaguzi umekuja na neema zake.

Licha ya kwamba jembe langu halijaingia mjengoni ila angalau nimepata cha kuipooza nafsi yangu na kunisahaulisha dhahma zote nilizokumbana nazo wakati huu mfupi.

Nimepata kigoli kimoja matata sana. Kimeumbika hakuna mfanowe, kina rangi ya mtume, hiyo sauti sasa mmh... mtoto jicho jicho, akinichumu utamu naona mimi.

Mtoto ametimia ndani na nje, mpole, mkarimu na zaidi ya yote mcheshi kwa kila mtu. Ila yote tisa kumi ni hili.

Huyu mrembo nashindwa kumuelewa kabisa. Ananitisha yaan naanza kumuogopa kwa kweli. Mambo yake yanastaajabisha. Ni mpenzi wa movie. Hilo si tatizo ila tatizo ni aina ya movie anazopenda.

Anapenda movie za kutisha tu. Mara watu wanachinjana, mara huyu kamnyofoa mwenzake koromeo, mara yule anatafuna gegedo la mwenzake, mara huyu kampasua mwenzake kichwa halafu anakunywa ubongo!! yaani taabu tupu.

Hivi hapa saa hizi anaangalia final destination amezipanga ya kwanza hadi ya tano, haogopi. Na kaniambia haimsisimui sana. Aisee!

Muonekano wake na aina ya movie anazotaka ni mbingu na ardhi abadani havifanani.

Huyu ilibidi awe anaangalia movie za kifilipino za akina Angelo, au zile za kizungu zile nyepesi nyepesi .

Muenendo wake unanitisha, nisije nikawa nimetongoza jini. Asije akaninyofoa uhai huyu.

Naombeni ushauri wanajamvi maana nimechanganyikiwa.

Picha pleez
 
Huyu mtu kama namjua hivi!!! yuko mkoa gani?
 
Back
Top Bottom