Nilivyolazimika kuapa ili niweze kuachana na mchepuko

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,524
6,505
Lengo la kuchapisha habari hii ni kutahadharishana na kuachana na Michepuko ambayo huleta sintofahamu katika ndoa zetu. Haya mambo sio poa kabisa na tusi yaendekeze hata kidogo.

Kabla ya kuanza kupata nyuzi bin nyuzi daah msemo huu alikuwa anapenda Sana kuutumia mtangazaji maarufu Sana Julius Nyei Sanga au Anko J enzi hizo Redio Tanzania ilikuwa hatar Sana,,,,,

Hakikisha unapata 🍿🍿🍿🍿 za kutosha ikiwezekana na hii 🥤🥤🥤pembeni mambo yawe burudani kabisa!

Naam,,,, Ilikuwa Facebook katika group la Dini nikiwa miongoni mwa ma-Admin,,lilikuwa group kubwa Tu na members kibao,,nisingependa kutaja Jina la hilo group huenda kuna wadau humu wakaonganisha doti na kunijua ukichukulia kwamba nilikuwa natumia Jina langu halisi.

Member Mmoja akatuma post kwamba kuna binti mmoja anataka kubadilisha Dini aolewe na Mgalatia,akaomba tumpe ushauri nini cha kufanya,akaomba atume namba ya huyo binti Kwa Admin ili tuwasiliane nae,,,basi mara paap namba hii hapa,nami nikafanya Yale ambayo nilitakiwa nifanye,,,nikavuta waya binti kapokea nikajitambulisha na kumwambia nimepata namba yko Kwa Fulani na ameniambia kuna moja mbili tatu! Binti akasema ni kweli kuna Jambo kama hilo,,,,nikamtaka kujua kwanini amefikia katika uamuzi huo,je ni mapenzi yake au kuna sababu maalum? Binti akasema kuna sababu iliyomfanya kufikia maamuzi hayo.

Binti akafunguka kuwa huyo aliye Nipa namba yake ni bwana wake na walikuwa katika mahusiano Kwa Mda mrefu Tu ila wameachana,,,wale ambao tulipitia Cuba huwa tunajua tone hii inamaanisha bidada katemwa na si vinginevyo. Basi nikampa ushauri ambao hata kama angetaka kujiua basi angebadilisha uamuzi wake mara moja.

Kwangu Mimi sikutaka maongezi yaendelee baada ya pale coz nilitaka tuyamalize kwenye Simu na Maisha mengine yaendelee,,,lakini bidada alionekana anataka kukutana na Mimi,akawa ananicheki tuonane ili anifungulie mafaili zaidi.

Ikaja siku tukakutana,binti akanipa story nzima na jamaa yake,ikiwemo wakati binti anasoma mkoani boy wake alikuwa anaenda anakaa hata wiki nzima hotelini wanakula Maisha,,,binti aliniambia jamaa alikuwa njema Sana kifweza maana ukisema kifedha ni zakawaida Tu. Akanipa na mambo mengine kibao wala msomaji wangu huna haja ya kuyajua.

Naweza kusema ilikuwa ni kosa kubwa Sana kukutana na Yule binti,alikuwa amesimama haswaa mpaka nikajiuliza boy wake inakuwaje kamuacha mtoto mzuri kama huyu? Kibaya Zaidi ni binti kunicheki Kwa phone mara Kwa mara,sasa jinsi alivyokuwa mtamu Kwa muonekano na kunivutia waya Kwa kile kilichoonekana kunisalimia kilizalisha connection kutoka katika moyo wangu na kwenda kwake,ikapatikana chemistry moja sio ya inchi hii!

Siku moja Yule binti alienda kwao mkoani,lakini kiukweli Mungu ndio anajua,,,nilijikuta upendo kwake unazidi si kawaida yaani kama mtu ameniseti hivi mpaka mwenyewe nikawa nawaza hii mbona si kawaida,nikajikuta nawaza eti mke wangu afe nipate Uhuru wa kuishi na huyu kiumbe,haikuwa poa kabisa,unajua Yule binti alikuwa na boy mwenye fweza sasa akanikuta na Mimi nina usafiri Fulani hivi WA heshima,,,,najua ndo zile hapa Jf kila mtu ana ndinga wala msiwaze kuhusu Hilo nilikuwa natumia ndinga fulani ya kampuni yetu (family company) yaani kusimamishwa na traffic ni mara chache sana,wale wa town wanajua kuna zile ndinga fulani ukiwa Una drive unajua kabisa nipo loaded hata traffic anaona aibu kunisimamisha.
Nasema hivyo kwasababu binti alitoka Kwa mtu mwenye fweza so akinicheki nami nasukuma usafir WA heshima akajua nami nipo byee,huenda alienda Kwa babu kuniweka sawa coz si Kwa upendo ule yaani kama karatasi imefungwa mtiini so upepo ukija Ile karatasi inavyopulizwa nami moyo wangu utafikiri unatumia pump kusukuma maana ni ❤️❤️❤️ Kwa kwenda mbele.

Akarudi dar fresh Tu,Mda wa kwenda kituo chake cha kazi ukafika,so siku hiyo nami nikamchukua wife nikampeleka sehemu nikamwacha huko,then nikampitia yeye nikampeleka stand aende zake kituoni,nakumbuka nilikuwa na play Ngoma moja ya Diana Ross na somebody Richie inaitwa "Endless love" wapenzi wa hizi nyimbo laini watakuwa washaijua hiyo,basi siku ikaisha salama.

Kesho yake asubuhi napata chai na wife kabla sijaenda kwenye Mishe Mishe, binti anapiga Simu daah nikaichek Kwa sekunde kadhaa nikaona ukisikia mtu kapanda mtumbwi wa Vibwengo ndio Leo sasa! Wife akasema vipi mbona hupokei,,,ikabidi mtu mzima nipokee kinyonge binti akasema alifika salama ana shukuru Kwa kumsindikiza,daah kosa hilo,wife alisikia mazungumzo ya upande wa pili,,,unafikir chai ilinyweka tena? Wife akanishika mkono mpaka chumbani,akasema "Yaani Siti niliyo kalia Jana ndio hiyo hiyo ukampakiza Malaya wako?" Yakazuka ya kuzuka nikapiga sound ambazo Kwa asilimia 50% zilipunguza pressure kidogo.
Kumbe bwana nilikuwa na ishi na mtu ambaye alisomea Cuba wala Mimi sina habari,wife alifanya mambo yake kimya kimya akamtafuta Yule binti Facebook wakawa marafiki, wakawa karibu kiasi ambacho Yule binti akatuma picha zake, kuna movie moja inaitwa Mr & Mrs Smith imechezwa na Brad Pit na Angelina Jolie hatar,mtu na mume wake wote maspy lakini hawajuani shughuli yake sio mchezo,wanao jua hii movie ndo wanajua shughuli yake! So Mimi na wife wote tumepitia Cuba lakini sikujua,mwisho wa siku wife akaleta file mezani,akanionyesha picha za binti daah na kunichana mambo kadhaa,ndio nikajua kumbe tunaishi na watu hatar Sana.

Wife akachukua Simu yangu na kuvunja laini yangu ya Simu,ili siku nyingine nisilete zile habar za ujue Huyu mwenyewe ndio ananitafuta au kunisumbua,,,nilikuwa mpole Tu kama nimeshikiwa bastola maana nikibisha ni kama vile Nataka kuendeleza mawasiliano na Yule binti. Ikabidi nisajili laini nyingine lkn kabla uamuzi wa kuvunja laini haujafikiwa niliwahi kumwambia Yule binti kuwa awe Makini anachati na mke wangu Bila yeye kujua daah alishtuka Sana!

Na Kule Facebook nikatakiwa nimblock Yule binti nikafanya hivyo mbele ya wife,,wakati huo Facebook ndo iko juu haswaa! Sasa asichojua wife ni kwamba Ile namba IPO kichwani kwangu,,,,na Mimi bwana nipo vizur kwenye kuhifadhi namba,sijui hizi tarakimu nyingi kama za Kadi ya bank au ving'amuzi au namba ya luku daah nikiamua zinakaa kichwani ,yaani nikiambiwa umeme umeisha au kifurushi kimeisha naingia kwenye malipo namba zinatoka kichwani,ukiona siku kuna mashindano ya kuhifadhi namba nishtue nikishinda tunagawana pasu Kwa pasu! Nakumbuka siku moja narudi home napita mtaani kuna wadada wakawa wanapeana namba wako mbali mbali kidogo,basi mmoja akamtajia mwenzake yaani nikazishika fasta Tu nikajisemea Moyoni daah ningekuwa naendekeza mbususu huyu dada ningemtafuta lkn hayo mambo hayana maana ni ujinga Tu.

Sasa ikabaki Vita na nafsi yangu na kumbuka tangu nipate hii namba mpya sikumtafuta Yule binti so inamaana alinitafuta Kwa namba ya zamani hakunipata. Nikaona hapa nisipo fanya maamuzi magumu litazuka Jambo lingine na wife mwenyewe alipitia Cuba,lazima angeendeleza harakati zake.

Nikabakiwa na option moja Tu nijikabidhi Kwa Mwenyezi Mungu kwasababu Mimi mwenyewe siwezi kujizuia Kwa Yule binti ni lazima ningemtafuta Tu,,,sasa Mwenyezi Mungu anasema yeye hawatii hatiani wale watu ambao wanaapa viapo vya ovyo ovyo Tu, si unajua zile " haki ya Mungu tena nakwambia kweli siku danganyi " viapo hivyo Mola wetu hatutii hatiani Ila anasema anatutia hatiani Kwa vile viapo ambavyo tume vipa uzito hasa katika nyoyo zetu hivyo ndo anatuwajibisha navyo,nikaona ili nimshinde Ibilisi lazima nifanye kiapo kizito ili niwe salama.

Nikatia Udhu wangu fresh Tu,,hii ishu hata wife hajui ni Mimi na Mola wangu,nikachukua Msahafu nikaongea na Mola wangu "Ewe Mola wangu nimeshika Kitabu chako takatifu naapa kwamba nitaachana na Yule mwanamke na nikimtafuta tena naomba Laana yako iwe juu yangu" nikarudia mara tatu. Nikajisikia Amani Sana kwani nikajua nikizingua Tu imekula kwangu,na ni kiapo ambacho nilikitia nguvu Moyoni mwangu. Kuanzia hapo kila nikimkumbuka Yule binti nakumbuka na kiapo changu,,,mwisho wa siku nilimsahau kabisa,nashukuru Sana Kwa ule uamuzi nilio ufanya.

Ndugu zangu Michepuko haimuachi mtu salama,unaweza chepuka hata miaka ishirini (20) na watu hao walikuwepo lkn mwisho wa siku walijulikana,IPO siku Ibilisi atakusaliti Tu amini usiamini habar ndio hiyo. Mpende mkeo au Mume wako muwe na salama katika ndoa yenu,kama mapenzi hakuna tena katika ndoa Bora muachane na kila mtu aendelee na Maisha yake,na uanze na ndoa mpya ambayo itakufanya usichepuke na kuwa na Amani wewe binafsi pamoja na kuwa Msafi Kwa Mola wako,,kumbuka kuna Maisha baada ya kufa,mazuri Kwa watendao mema na mabaya Kwa wafanyao uovu,na uovu mmoja wapo ni ZINAA/UZINZI.

Ni hayo Tu.
 
Copied and edited ya uzi wa bujibuji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom