Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Mkuu pole sana. Nmesoma uzi wako mara mbilimbili. Nimesoma kwa undani zaidi na kuelewa choice of words uuliyotumia. Nikiri : WEWE NI MWANDISHI MZURI SANA. pia unaonekana unakuwa so committed unapokuwa kazini.

Watu kama nyie huwa mnawaza kazi tu hamfanyi biashara nyingine.mnajituma na kuipenda kazi hata yenyewe isipokupenda. Ndo maana uliendelea kupambana ukiamini mngeshinda.

Lakini nimeona pia ambao wamekukumbuka ni watu wa chini ambao nadhani ni sababu ya jinsi ambavyo uliishi nao.

Marafiki ni wachache sana duniani.ila nakwambia kwa uzi huu leo hii unaweza pia pata marafiki ndugu.

Mimi ntaendelea kupambana nikutafutie kazi pia kwa lolote litakalowezekana. Usikate tamaa haya ni maisha. Tupambane. Naamini na wengine wataguswa kwa hili. Endelea kumpenda mkeo. Siku moja atakuja kuomba msamaha kama ana akili.
 
Kuna wakati unaweza ukamlilia Mungu sababu ya shida zako ila ukisikia ya wengine utajiona unakufuru
Pole sana mkuu, Mungu akupitishe katika hilo.

Jamani muwe wema na muwatende mema wake zenu mnapokuwa katika nyakati nzuri ili wasiwatenge katika nyakati mbaya pia.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Sodoku

Najua ugumu wa hali unayopitia, tazama wanao na kufikiria maisha yao ya baadaye. Ondoa fikra mbaya kuhusi uhai wako.
Yaone hayo anayokufanyia mkeo kama ufunuo kwa mengi uliyokuwa huyajui wakati familia ipo na neema.

Hakika nakwambia, huo ujumbe aliokutumia binti wa kazi una maana kubwa. Trust me, ukizingatia utakufungulia mwangaza mpya wa maisha.

Kingine, JF inawatu wa kila aina. Naamini post yako haitaondoka bure.

Keep your head up.
 
Pole.
Tunapowekeza mahali pamoja pakaticki tusijisahau kuwekeza na pengine tofauti tofauti.maana kimoja kinaweza anguka,kingine kikabaki na kukushika

Mkeo ni mjinga na hana busara,million sita ni pesa nyingi sana kuwekeza ya kaenda katafuta mteremko QNet kaliwa ni mjinga!.kapata kazi bado anakuumiza ilhali anajua kazi huna na unaumwa hana busara!
Kwanini usiuze vitu ulivyonayo baadhi vyenye thamani vikusongeshe kuliko vikikaa tu vinachakaa ukweni?
Ulisema mna nyumba mnamalizia kujenga kwanini usiuze angalau utapata hata million 20-40 uanze upya?
Ama uza hili gari kisha hamia nyumba mnayojenga ikiwa hata pagala juu bati madirisha ya nyavu muanze maisha huku unaendelea kutafuta kazi?


Ni ushauri tu maana huwezi jua Hiki kilio kitachukua mda gani..so ujiongsze kwanza.
Mi mwenyewe nashangaa mkuu yaani mke kapewa milioni 6 kapoteza kizembe then brother anapata taabu ye anaendelea kumumiza .

Hapa jamaa mke hana
 
Lakini pia wanaume huwa mnakosea sana kuamini kuwa kila mwanamke anaweza kufanya biashara kwamba akikosa ajira basi anaweza biashara. Biashara sio ya kila mtu jamani, mtu hajawahi kufanya biashara hata ya pipi akajua changamoto ndogo unampa milioni 6 bila plans za kueleweka!! Matokeo yake ndio hayo akaishia kutapeliwa.

Ingekuwa rahisi hivyo mbona wote tungekuwa wafanyabiashara! Na hii nafikiri ni kwasababu watu huwa hamsomani na kujuana vizuri, maana usingefanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani muwe wema na muwatende mema wake zenu mnapokuwa katika nyakati nzuri ili wasiwatenge katika nyakati mbaya pia.


Sent using Jamii Forums mobile app


Umesoma vizuri alimsaidia mke wake mtaji wa Milioni 6 ili akaanzishe biashara, hiyo haitoshi kuonesha wazi kwamba alimjali mke wake na alipenda kuona nae ananyanyuka kuongeza kipato cha familia pamoja na mahitaji yake binafsi?
 
To be honest, namshukuru sana Mungu kwa aina ya mke alie nipea.
Najua hajakamilika, lakini hakika ni wakipekee sana nikilinganisha na changamoto ambazo wengi wanapitia na wake zao.
Anyway, pole sana mkuu na hakika ningekua na connection ningekuunganisha kwa bidii zangu zote.
Ebu naomba namba zako PM
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom