philantrhopist
JF-Expert Member
- Jun 18, 2023
- 376
- 622
Naenda moja kwa moja kuhusu hii kazi ya kuajiriwa.
Nina shahada ya ualimu, nimetafuta kazi miaka mingi ni mizinguo kila kona, kwingine wanalipa 100,000 ukiangalia bajeti yaani hata hela ya vocha unaweza kukosa. Nikachunguza na maisha ya walimu si mazuri kiviile japokuwa kuna wachache waliotoboa na wana maisha mazuri tu.
Katika kupambana kwangu sasa nimeajiriwa duka la mhindi, yaani napelekeshwa sana yaani sipumui. Ukitaka hata kupumzika unasikia wewe (X) njoo fanya haraka sogeza.
Nikirudi usiku nimechoka ukilala ni usingizi wa pono.
Mshahara ninaolipwa ni 300k. Nina wadogo zangu wananitegemea pamoja na wazazi pia.
Nimetoka familia masikini, nimewaza hadi nimekonda.
Hela yenyewe nikiichukua sijui inakua na majini inaisha haraka hadi nashindwa kujiwekeza.
Nimefika sehemu nikasema sasa haya maisha ni kama hayana maana kabisa kwa sababu sioni ninachokifanya.
Enyi ninyi wenye koneksheni, au mliofanikiwa nipeni mbinu jamani na mimi nijiajiri kwa sababu kuajiriwa ni kazi. Unapelekeshwa, mishahara haitoshi, bosi anaweza kufanya chochote anachoweza kufanya.
Ee Mungu ni lini nitatoboa niachane hizi taabu. Umaskini wa baba na mama usiwe kikwazo cha kufanikiwa kwangu, nifanyeje?