Mkoba wa Mama
Senior Member
- May 5, 2021
- 113
- 45
Mwaka wa tatu wanaomaliza fani za afya ngazi ya stashahada matokeo yao yanachelewa sana kutoka hivyo kupelekea wahitimu wanaohitaji kuendelea na vyuo vikuu kushindwa kupata udahili kwa mwaka huo na hivyo kusubiri takribani mwaka mzima ili waje kuomba mwaka unaofuata.
NACTVET wabadilishe utaratibu huu, ni kero na kikwazo kwa wahitimu wanaotarajia kuunganisha moja kwa moja na elimu ya juu, lakini pia kuwachelewesha watu na malengo yao.
Naomba hili suala liwafikie NACTVET, Wizara ya afya, wizara ya elimu na wote wanaohusika. Wanaweza kufanya yafuatayo;
Mwaka wa tatu wawe wanaanza mitihani yao ya mwisho mapema zaidi ili matokeo yao yaandaliwe na yatolewe mapema kabla ya udahili wa vyuo vikuu kufungwa.
Au kama rasilimali za kufanya hivyo hazitoshi, basi mitihani inapomalizika, mitihani ya mwaka wa tatu iwe inaanza kusahihishwa kwanza kabla ya mwaka wa pili na wa kwanza ili matokeo yake yatolewa mapema zaidi ili wanaohitaji kuunganisha na elimu ya juu wapate fursa ya kuomba vyuo na kuwaepushia kero na usumbufu kwa kukaa mtaani mwaka mzima bila kazi ya kufanya.
La sivyo uwekwe utaratibu wa kufunguliwa kwa dirisha maalumu la udahili kwa wanafunzi waliomaliza stashahada pindi matokeo yanapotoka, ili kusiwepo na kikwazo kwa wale wanaohitaji kuunganisha chuo kikuu.