DavidsonM42
New Member
- Jul 29, 2022
- 2
- 0
Habari wadau,
Ninatumaini kuwa mnaendelea vyema na Majukumu.
Mimi ni Mhitimu wa diploma idara ya Umeme katika taasisi ya teknolojia Dar es salaam DIT Mwaka wa masomo 2021/2022.
Ninawaandikia thread kuomba msaada na kufikisha Malalamiko yangu kuhusu kucheleweshewa au kushindwa kupatiwa Award Verification Number (AVN) inayotolewa na NACTVET, baada ya kuthibitishwa Matokeo ambayo yanawasilishwa na Chuo husika ili kuniwezesha kuendelea na Masomo ya Shahada ya Kwanza ( Bachelor Degree).
Ni Mwaka wa pili sasa tangu nmehitimu mimi nikiwa mmoja wa Wahanga na baadhi ya Wahitimu wengine. na tumekuwa tukifatilia suala la kupata AVN lakini mpaka sasa Hatujafanikiwa na madirisha yote ya udahili yameshafungwa na vyuo vimeshafunguliwa kuanza mwaka mpya wa masomo 2023/2024.
Tumekuwa tukienda NACTVET tunaambiwa turudi chuoni kuwaambia wawasilishe Matokeo yetu ili yaweze kuthibitishwa ( Verification). ili tuweze kupatiwa AVN.
Tukienda Chuoni tunaambiwa NACTVET Wamefunga system hvyo hawawezi kuwasilisha Matokeo na tunaambiwa tuvute subira mpaka watakapofungua system.
Baada ya kuzunguka Mara kadhaa Kwenda NACTVET na Chuoni, NACTVET waliamua kutuweka wazi kuwa walifunga system kwa sababu Chuo (DIT), kilichelewesha kuwasilisha Matokeo yetu kwa ajili ya Verification.
Baada ya kuwauliza chuo idara ya Electrical walikiri kuchelewesha kuwasilisha Matokeo yetu NACTVET na kusema kuwa waliandika barua kuomba kufunguliwa system, barua ambayo mpaka sasa haijajibiwa na hawajui ni lini itajibiwa na wala itajibiwa au haitajibiwa.
Tukaenda NACTVET nao kuwauliza kuhusu hiyo barua, wakakiri kweli wameipokea hiyo barua ila wataamua wenyewe waijibu au wasiijibu. (Itategemea na watakavyojisikia).
Kiukweli tunakosa msaada hatujui tufanye nini, kosa la chuo lakini Adhabu tunabebeshwa sisi tusio na hatia yoyote.
Tunaomba Msaada katika hili, kiukweli linatuumiza sana tunabaki, tukiwa hatuna cha kufanya Mda unazidi kwenda bila matumaini yoyote, Tunaomba mtusaidie kufikisha malalmiko yetu Kwenye Mamlaka husika tuweze kupata AVN, Tuendelee na Masomo kama wengine walivyoendelea.
Tunawshukuru sana kwa muda wenu, na tunatumaini mtatusaidia kupaza sauti katika hili.
Kwa Niaba ya Wenzangu Ninatanguliza Shukrani zangu za dhati.
Ahsanteni Wadau
Mhitimu/Mhanga-DIT