NACTVET Amkeni mnawachanganya watoto wetu

Jantisa

New Member
Feb 13, 2023
2
2
Habari wana jamvi,

Mimi ni mzazi wa mwanafunzi anasoma stashahada ya Pharmaceutical Sciences katika Vyuo vya Kati vya Sayansi Shirikishi. Changamoto ni kuwa matokeo yao ya semester iliyopita mpaka leo hayajatoka. Wakiuliza chuoni, wanawaambiwa mfumo wa NACTVET unasumbua.

Changamoto nyingine ni kuwa vyuo vinafungua kuanzia leo, na wanahitaji kufanya usajili kabla ya tarehe 23 mwezi huu. Hapo kuna zaliwa maswali: Je, kama mwanafunzi amefeli, atarudishiwa gharama zake za usajili?

Pili, je, kwa wanafunzi waliopata supplementary mitihani ya sup, wataifanya lini? Na je, inawezekanaje mwanafunzi ajisajili ilihali hajui matokeo yake ya semester iliyopita? NACTVET, amkeni! Elimu yetu mnaichelewesha.

Naomba kuwasilisha.
 
Ni jambo gumu mwanafunzi anaanza kusoma mwaka mwingine wakati hajui matokeo yake ya End of the semister. NACTVET walishughulikie hili swala
 
Back
Top Bottom