Nachingwea: Viongozi wa Serikali na Wachimbaji washirikiana kutorosha pesa za mgodi

May 4, 2020
32
37
Zaidi ya shilingi milioni 901 zimekusanywa na serikali kuu kupitia mrabaha na ada ya ukaguzi katika mgodi wa madini ya shaba uliopo katika kijiji cha Nditi wilayani Nachingwea.

Hayo yamesemwa na afisa madini mkazi Iddy Msikozi alipokuwa akisoma taarifa ya makusanyo tangu Septemba 28, 2022 hadi Disemba 31,2022 na kueleza kuwa, tangu mgodi huo uanzwe kuchimbwa mwaka 2020, zaidi ya tani 17 zimechimbwa zenye jumla ya shilingi Bilioni 12,850,725/= ambapo ofisi ya madini imekusanya jumla ya shilingi Milioni 901,341,000/=

Naye mkuu wa wilaya hiyo Hashim Komba amesema mbali na makusanyo hayo, baadhi ya wachimbaji kwa kushirikiana na viongozi wa serikali bado wanajaribu kuchepusha kodi hizo hivyo ameunda timu maalum itakayofuatilia risiti za malipo ya serikali ya kijiji pamoja na kuagiza magari yote yanayokwenda kuchukua mzigo kuanza kupimwa uzito katika ghala la Lindi Pharmacy kabla na baada ya kuchukua mzigo huku timu maalumu ikitakiwa kufuatia magari hayo mpaka katika mzani wa Mnazi Mmoja ili kujifunza zaidi na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote waliohusika kukwepa kodi.

c799e4ad-da66-4565-83e0-9c02166fd070.jpeg
 
Back
Top Bottom