Katavi: Wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mpanda wailalamikia Serikali kushindwa kutatua mgogoro wa muda mrefu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462

Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Kiiji cha Dilifu kilichopo Kata ya Magamba iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wameulalamikia uongozi wa wilaya hiyo kwa kushindwa kutatua mgogoro baina yao, muwekezaji na kikundi kinachomiliki leseni ya uchimbaji madini katika eneo hilo.

Wachimbaji hao wamesema mbali na mgogoro kushindwa kupata ufumbuzi, kumekuwa na suala la wao kukamatwa mara kwa mara pasipo kujua sababu hali ambayo inaendelea kuwanyima uhuru katika shughuli yao.

Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Katavi, mhandisi Andrew Mwalugaja amesema sheria hairuhusu kutoa leseni kwenye umiliki wa kijiji na badala yake wajiunge kikundi ili waweze kuwa na sifa ya kupatiwa leseni ya uchimbaji.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf amesema katika mgogoro huo utatuzi ungekuwa umepatikana na kuridhiana isipokua Wananchi na wachimbaji wadogo hawakuridhika na maamuzi yaliyotolewa ambapo amesisitiza sheria kali zitachukuliwa dhidi ya mtu au kikundi kitakachoanzisha uvunjifu wa amani katika eneo hilo.
 
Back
Top Bottom