Nabii asiekubalika nyumbani

Yote tisa,namkubali Zitto na nafurahi umekiri kuwa anamapungufu,wengine wanamuona Mungu mtu. Na yeye anajiona hivyo.
Zitto kosa lake kubwa la kiufundi katika siasa zake ni kukisaliti na kujiona yeye ni bora kuliko chama baasi,mengine yote yamkini ni sahihi. Hii imesham-cost sana reputation yake alioijenga kwa miaka mingi na nguvu kubwa kama sio damu! Msalimie sana
 
Zitto pamoja hivyo vifursa c.c.m unavyo vipata ukweli ni kwamba umechuja kisiasa.
'willafrica'
 
Mimi namkubali sana zito ila haya maswali hayajapata majibu kichwani mwangu.
1.zito ni rafiki wa nimrod mkono na aliwahi kufanya kazi ofisini kwa mkono?
2.je wakati wa kifo cha chacha wangwe alipewa gari na mkono au alikodishiwa au aliuziwa?
3.je mkono amechota bil 52 tanesko na kesi iptl imeshinda?
4.je ugomvi wa mkono na muhongo una uhusiano na ugomvi wa zito na muhongo?
5.je majina ya uswis yapo?
6.je katika siasa za kibiashara za tanzania unaweza kupiga vita ufisadi wa viongozi walafi katika vyama vyote na bado ukanywa nao chai ukawa salama?
7.je ni mwanasiasa gani na aliwahi kutokea nchi gani kutoka chama cha upinzani aliwahi kutia mchanga kitumbua cha watawala na kuwa rafiki wa watawala na adui wa chama chake?
maswali haya yakipata majibu ya uhakika kwangu mimi zitto atakuwa zaidi ya nabii.
 
Wakuu,

JANA, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu Barani Afrika (AFROPAC) katika mkutano uliofanyika jijini Lusaka, Zambia.

Huu ni umoja mchanga kabisa ambao ndiyo uko katika mwaka wake wa kwanza. Kimsingi, uteuzi huu wa Zitto unamaanisha kwamba yeye ndiye atakuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za umoja huu mpya.

Atakuwa kiongozi wa Sekretarieti ya AFROPAC na hivyo atakuwa anasimamia waajiriwa wote wa umoja huo kwa sasa. Hii maana yake ni kwamba Watanzania watapata nafasi zaidi za kuajiriwa.

Ndiyo maana, nafasi hii ilikuwa ikiwaniwa na wabunge wengi kutoka katika mabunge mengine barani Afrika. Kwenye umoja kama AFROPAC, nafasi ya Mkuu wa Sekretarieti huwa na faida kwa wananchi wa nchi anayotoka Katibu Mkuu.
Huu si uteuzi wa kwanza wa Zitto ambao unaonyesha heshima anayopewa nje ya nchi. Ni Zitto huyuhuyu ambaye miaka michache iliyopita aliteuliwa na aliyekuwa Rais wa Ujerumani, Horst Kohler, kuwa mmoja wa viongozi vijana wanaochipukia barani Afrika chini ya mpango uliofahamika kwa jina la Africa Initiative.

Katika bara zima la Afrika, serikali ya Ujerumani iliteua vijana takribani 40 tu ambao walionekana kuwa tumaini la bara hili katika miaka ijayo.
Katika kitabu cha Global Corruption, Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Rushwa ya Transparency International (TI), Laurence Cockcroft, alimueleza Zitto kama kiongozi "makini, mwenye uelewa mpana na mpambanaji wa rushwa."

Ni Zitto ambaye amechochea vijana wengi kujiunga na siasa katika miaka ya karibuni. Miaka kumi iliyopita, Bunge lilikuwa ni taasisi ya wastaafu na wateule wachache waliodumu kwa miaka mingi.

Ni Zitto ambaye uwepo wake na ujengaji wake wa hoja ulifichua nguvu na upya ambao taasisi hiyo ilikuwa inatakiwa kuwa nao. Kama utaongea na wabunge vijana walioingia bungeni katika Uchaguz uliopita, nusu watakwambia kwamba Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini ndiye aliyewashawishikufuata njia hiyo ya uanasiasa.

[03:40, 14/05/2014] ZITTO KABWE: Mwanasiasa huyu ni mtoto wa familia isiyo ya kitajiri wala yenye historia yoyote na Tanzania. Ni Zitto Kabwe ndiye aliyewaonyesha watu kwamba unaweza kuwa mtoto wa masikini na usiye na uhusiano wowote wa damu au uswahiba na familia tajiri na bado ukawa na fursa.

Na tangu ameingia bungeni, Mbunge huyu amekuwa nyuma ya karibu matukio yote makubwa ambayo yametokea bungeni katika miaka ya karibuni.

Yeye ndiye aliyeibua suala la Buzwagi ambalo leo limetupa Sheria Mpya ya Madini ambayo walau ina manufaa kwa wananchi kuliko sheria iliyokuwepo kabla hajaingia bungeni.

Zitto Kabwe ndiye aliyependekeza kwa serikali Waziri Sospeter Muhongo Mabadiliko ya Sheria katika Nishati ya Gesi ambayo leo yataiingizia serikali mabilioni ya fedha kila makampuni ya gesi yatakapokuwa yanauziana hisa yenyewe kwa yenyewe.

Kabla Zitto hajaingia bungeni, makampuni haya yalikuwa yakibadilisha majina au kuuziana hisa pasipo Tanzania kufaidika na lolote. Nchi hii imepoteza mabilioni ya shilingi kwa mtindo huu.

Leo hii, Mbunge huyu anafuatilia Ufisadi katika Ulipaji wa Kodi unaofanywa na Makampuni Makubwa si Tanzania pekee bali barani Afrika kwa ujumla.

Makampuni haya yanakwepa kulipa kodi au kulipa kodi kidogo kwa serikali kwa kutumia njia ambazo zilikuwa hazijabainika huko nyuma. Kama serikali itaanza kukusanya kodi yake stahili na kuzuia ukwepaji huo wa kodi, Zitto atakuwa amesaidia katika hilo.

Kodi hii ndiyo ambayo itasaidia kununua dawa katika hospitali zetu, madawati katika shule zetu, kuzuia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kujenga barabara na miundombinu mingine.

Mara zote, Zitto amefanya haya pasipo kutukana wala kugombana na watu. Siku zote amekuwa ni mtu wa kujenga hoja na amekuwa na marafiki karibu katika vyama vyote ambavyo viko hapa nchini.

Ni vigumu, vigumu sana kumlinganisha Zitto na Mbunge yeyote kijana katika Bunge la sasa… Binafsi, naamini kwamba huyu ndiye Mbunge wa muhimu zaidi kuliko wabunge wengine wote waliopo katika Bunge la Tanzania.

Na hii ni kwa sababu ya rekodi zake nilizotaja hapo juu. Badala ya kubishana kuhusu umuhimu wake, ni vema watu wakakumbushana na kueleza ni mbunge yupi amekuwa na mchango mkubwa bungeni kuliko huyu wa CHADEMA.
 
Tatizo watu wanapomzungumzia Zitto wanazungumzia uwezo wake kiakili ambao ni kichaa pekee anaweza kupinga hilo......lakini watu hao ni vipofu wa matatizo ya msingi ya Zitto kisiasa.....Zitto kichwa chake kinafaa maeneo maalum lakini si uongozi wa maswala ya kisiasa......hasa yeye asipokuwa kiongozi mkuu........kama wote tungesimamia ukweli kuhusu Zitto leo tungekuwa na mwanasiasa anayeelekea kutwaa dola kupitia CDM.....ingewezekana hata kama nani asingependa.......lakini endeleeni kumpa kichwa..........zitabaki hadithi kama hizi za Ezekiel Kamwaga...........Tuache unafiki......Zitto aache ubinafsi.........umma unaeweza kukuweka unapotaka bila kuhitaji ujanja ujanja.........

Huu ndio ukweli mchungu kwelikweli......na hautabadilika hadi atakapobadilika hata akiwa huko ACT.........
 
Nabii wa intarahamwe! Ila bahati mbay unabii wake haukutimia!
 
Hakuna nabii mwizi. Billion ngapi za walipa kodi wa Tanganyika alizopelekewa Ujerumani? Halafu kuchaguliwna kwake kulikuwaje? Walishindanishwa? au ampendekezwa na hao anaowatumikia kuharibu demokrasa nchini?
 
Back
Top Bottom