Mzungu Omba Omba ndani ya Dar

haha mi nakumbuka 2010 nipo mi taa ya far east Beijing ...kipindi cha Olympic kile, mtasha alinipiga mzinga alinipa story hizohizo .. ila yeye alidai kaibiwa .. sikumuamini but niliamua tu kumsaidia
 
Jana nilikuwa najipitia zangu,nilipita pale kwenye jengo la NSSF(AKIBA)nikasimamishwa na mzungu mmoja mtu wa makamo kavalia nadhifu ,akaniuliza samahani unajua kiingereza nikasema ndio ,loo ikawa nimechokoza nyuki akaanza kuniambia ana matatizo na dada yake ,hadi sasa kaishiwa hela anaomba nimsaidie hata elfu kumi au hata elfu tano nikasema sina hiyo hela mwishowe nikamuachia elfu mbili akasema mungu akubariki ,lakini nina wasiwasi na huyo mtasha asije kuwa muongo,lakini hii ni Bongo huenda nitaonana naye tena na akaniomba kwa sababu zilezile

Atakuwa mndengereko huyo si kila ngozi nyeupe imezaliwa ulaya
 
Yaa ok jamaa ameshakupata, anafanya research kuangalia umasikini wa kipato na ujinga wa walami wa kutokujua kuwa hawatakiwi kutoa hela kiulaini coz hawana.

Kwa hiyo hutaki kuamini kuwa wazungu katika mazingira fulani wanaweza kukosa hata mia?Kama inavyoweza kutokea kwa mtu wa rangi yeyote ile?
 
Mwekezaji huyo kafilisika wakati anasubiri Serikali imkopeshe mabilioni ndio anavuta vuta siku kwa kuomba omba pesa ya kula.
Kwaninia asiende ubalozini kwao?
 
Naomba niungane na wewe kumshangaa huyo barry!!
Watu wanatingwa! Mimi nimeshawahi kutingwa nikatembea posta mwenge..niliikubali hali ile na maisha yakaendelea. Nilitamani kuomba hata mia..ingetosha nauli wakati ule lakini nikakomaa!
Maisha bana!! Kulaleki maisha!
Kwa hiyo hutaki kuamini kuwa wazungu katika mazingira fulani wanaweza kukosa hata mia?Kama inavyoweza kutokea kwa mtu wa rangi yeyote ile?
 
Jana nilikuwa najipitia zangu,nilipita pale kwenye jengo la NSSF(AKIBA)nikasimamishwa na mzungu mmoja mtu wa makamo kavalia nadhifu ,akaniuliza samahani unajua kiingereza nikasema ndio ,loo ikawa nimechokoza nyuki akaanza kuniambia ana matatizo na dada yake ,hadi sasa kaishiwa hela anaomba nimsaidie hata elfu kumi au hata elfu tano nikasema sina hiyo hela mwishowe nikamuachia elfu mbili akasema mungu akubariki ,lakini nina wasiwasi na huyo mtasha asije kuwa muongo,lakini hii ni Bongo huenda nitaonana naye tena na akaniomba kwa sababu zilezile

Sasa ajabu hapo kitu gani?
 
Wabongo bwana,kila mtasha tunaona kama ni tajiri sana na amezaliwa ulaya,huyo atakua amezaliwa na machangudoa wa kule kinondoni makaburini mtasha alienda kutafuta dozi akampata mdada wa bongo mara mdada kapatakitu kazaa mtoto anafanana na baba yake,mtoto kawa mkubwa kaja nssf kakupiga bao ukampatia donge nono kwa sababu ya rangi yake.Baada ya hapo mtoto kaona kumbe kwa kuwa na ile rangi na ungenge kidogo anavuta hela kilaini.Kweli rangi za wazungu zinaeshimika.
 
Jana nilikuwa najipitia zangu,nilipita pale kwenye jengo la NSSF(AKIBA)nikasimamishwa na mzungu mmoja mtu wa makamo kavalia nadhifu ,akaniuliza samahani unajua kiingereza nikasema ndio ,loo ikawa nimechokoza nyuki akaanza kuniambia ana matatizo na dada yake ,hadi sasa kaishiwa hela anaomba nimsaidie hata elfu kumi au hata elfu tano nikasema sina hiyo hela mwishowe nikamuachia elfu mbili akasema mungu akubariki ,lakini nina wasiwasi na huyo mtasha asije kuwa muongo,lakini hii ni Bongo huenda nitaonana naye tena na akaniomba kwa sababu zilezile

Mi pia mitaa ya bamaga siku ya jumapili ya mechi ya manchester kupigwa 6 na man city, lakini alikua kavaa jinzi imechafuka kidogo na white sneakers akachukua tsh alfu tano. Inawezekana akawa ni mtu yuleyule?
 
yesu alikuja kuokoa wenye dhambi na wewe umeletwa kusaidia masikini ok!!uwe unajitahdi kujua kutoa kuliko kupokea na kwa msaada ukitoa ukaja kubwabwaja hapa aijalishi muhindi mzungu mhabeshi umemsaidia baraka zako kwishna bora usingetoa
 
Jamani ni vema kuhabarishana mambo kama haya,wapo watu ambao wanaomba wakiwa kweli na dharula, lakini wapo wengine ambao huomba kana kwamba wana dharula lakini hiyo ndiyo staili yao ya kuishi wala si dharula.

Binafsi nimewahi kupigwa mzinga na jamaa mmoja ambae wakati ananiomba na kunieleza kilichomsibu nilimsaidia, bahati mbaya kwake/nzuli kwangu ni kwamba nimemwona/nimepishana nae zaidi mara nne akiwa ameongozana na watu wale wale nafikiri alikuwa katika malengo yale yale.

Mbinu anayoitumia ni kukufanya wewe mwanaume mwenziwe umwonee huruma ili umsitili, husingizia kuibiwa kila kitu akiwa safarini (kwangu alisema ametoka Singida anakwenda Lindi) akiwa ameongozana na mwanamke mwenye mtoto mchanga na vibinti viwili,.

Huomba umsaidie chochote ili angalau familia yake ipate chai kwa muda huo ili akiendelea kusubili msaada kwa ndugu yake fulani ili aendelee na safari yake.

J2 majira ya saa 5.niliingia ubungo plaza Akiba Comm.Bank,wakati naingia kwenye gari jamaa akawa ananiita, brother, brother, akiwa na timu yake ile ile, nilimwitikia na kumuuliza vipi bado hujaenda Lindi ? Aliamua kunishit na kuendelea na safari yake akielekea Uelekeo wa Ubungo upcountry Bus terminal.

Kwa hiyo matapeli wapo tena idadi ya kutosha na wenye shida ya ukweli wapo japo ni wachache kuliko wale ambao utapeli wa kusingizia dharula ni sehemu ya ajila kwao.
 
Tehe tehe, umenikumbusha jamaa tulikuwa tunaangalia naye movie ya kizunu akasema ''du wazungu wana akili sana, yaani hata mtoto mdogo anajua kuongea kiingereza!!! Huku kwetu hadi tunazeeka kiingereza cha kubabaisha''. Ndio wewe jamaa unayeshangaa mzungu kufulia wakati kakueleza na matatizo aliyonayo.
 
Mimi nimeshawahi kutingwa nikatembea posta mwenge..niliikubali hali ile na maisha yakaendelea. Nilitamani kuomba hata mia..ingetosha nauli wakati ule lakini nikakomaa!
Siku nyingine ukikosa nauli usitembee hadi Mwenge, kuna umbali wa kutosha. Subiri daladala ifike, piga debe kuita abiria, halafu dandia mlangoni, konda atajua wewe ni 'staff' !
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom