Mzee wa Upako: Sina jirani, tunaishi kama majambazi

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,944
By Kelvin Matandiko Mwananchi,

Dar es Salaam. Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.

“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.

Lusekelo amesema Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake. Amesema magazeti hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpaisha ila Mungu pekee.

Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.

Alhamisi iliyopita, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani yake lakini mchungaji huyo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo ambalo lilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia mzozo huo, kuandika kwa kirefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Picha ya video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha mtu anayedaiwa kuwa ni mchungaji Lusekelo akijibizana na sauti ya mwanamke, ambaye haonekani, huku gari la rangi nyeusi aina ya Toyota Landcruiser likiwa limeegeshwa katikati ya barabara ya mtaani na kuzuia mengine kupita.

“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”

“Kwanini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani, matatani babu yako.”

“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza", amesema.

Mwanzo: Mwananchi
 
1480328687677.jpg
1480328701504.jpg
hata picha zake zinaonesha ya kuwa Mzee wa nyagi
 
Wajinga Ndiyo Waliwao
SHIDA ni kwamba jamii yetu haijajua kuwa hawa ni wajasiliamari. Wapiga deal tu. Umasikini wa mali na fikra ni shida.
Mtu anaondoka asubuhi nyumbani kwake hajui atakula nini, anaenda kanisani kupeleka sadaka na zaka eti abarikiwe zaidi. Huo si wehu uliopitiliza. Kama siyo wehu basi mtu huyo ana mtindio wa ubongo. Mungu wanayemtangaza kila siku howa tele-evangilists ni Mungu wa uongo tu. Wanamtumia huyo Mungu kuwaibia masikini. So sad
 
Back
Top Bottom