sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,034
Makanisa ya mazingaombwe kipaumbele huwa ni kufanya mazingaombwe ambayo watu wengi wenye imani nyepesi huona ni miujiza, neno lina nafasi ndogo sana.
Wachungaji wa hayo makanisa wamegeuza imani nyepesi za waumini kujikusanyia utajiri wa kutisha, Mafuta ya kuitwa ya upako yanatengenezwa hapa hapa kwetu kwa mimea ya hapa hapa gharama za kichupa huwa ni elf 1 lakini waumini wapo tayari kulipia laki 1, Kumuona mchungaji laki kadhaa, n.k. ni wizi mtupu katika jina la imani dhaifu,
Mazingaombwe yanayofanywa ni script na kuna wakati yana hatari kubwa sana kupiga ramli chonganishi, kila kitu kipo well planned, nimewahi kushuhudia live kwa macho yangu kanisa flani ambalo mchungaji alikuwa jirani, mke wake na mdogo wale walikuwa wanajiunga kwenye timu ya kujitupa tupa ku act wana mapepo, waumini wapya wanadata na kudhani mchungaji yupo nondo.
Omba sana mkeo asianze kwenda aina hii ya makanisa, kama ni mchumba jiweke pembeni fasta sana muache, Watu hawa huwa wanajiweka nafasi ya kuonekana ni miungu watu, mwanamke akisazamia huko anaamini kila anachotaka huyo nabii wa mchongo inabidi kiheshimiwe automatically sio cha kupingwa, kuna mwezetu aliweka kisa humu kwamba mke wake anaacha mtoto anaenyonya nyumbani kwenda kanisani kisa tu mchungaji kasema awepo, mtoto hajanyonya lakini mama anamheshimu zaidi mchungaji.
Hata pale video za mchungaji chafu zikivuja ukifatilia utaona wanaomkingia kifua kusema video ime editiwa ni wale waumini wanawake, mchungaji kashawakamata imani zao huwezi waambia kitu.
Makanisani ukiona wanaume basi ni Dj, wapiga vyombo vya muziki, wale wanaokamata wanawake wanao act wana mapepo, n.k. ukiona wanaume wengine mara nyingi ni wale wanalazimishwa kwenda huko kwa shinikizo la wanawake sio kwa hiari yao, unakuta mmama analia kabisa nenda, basi mwanaume ananeda basi tu sio kwa hiari yake.