Mzee wa upako: CCM ya Kikwete ni mbaya kuliko rais Gaddafi

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Mzee wa upako amejitokeza hadharani na kuishambulia CCM na viongozi wake,

  • Amesema maendeleo ya CCM ndani ya miaka 50 ni sawa yapo mbali sana na kuyafananisha na mtu mzima kuvaa nepi.
  • Amesema CCM imekuwa inalindwa na vombo vya dola na usalama wa taifa ndio unaohusika na kuiweka madarakani!
  • Amesema bila watu wa usalama wa taifa mtu hawazi kushinda!

Source : Gazeti Nyakati leo

Miezi iliyopita mzee wa upako alihubili kanisani kwake akisema kuwa viongozi wa juu CCM wana viroboto kichani na kwamba wasipobadilika muda mfupi ujao atawaroga!

Watafiti wa mambo ya kisiasa wanasema mzee wa upako amekuwa kampeni manaja wa rais kikwete katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini baada ya dhana ya kujivua gamba yeye alimshauli kikwete asifanye hivyo lakini hawakukubaliana.

Kutokana na mgogoro huo mzee wa upako akaamua kumuunga mkono Lowassa na sasa yupo kambi ya Lowassa. Kambi ya Lowassa inamhusu askof Thomas Laizer, Askof Mgullu Kilimba, askofu Mokiwa na wengine

Mpaka sasa Lowassa amefanikiwa kupata mtandao ndani ya makanisa kupitia viongozi hawa wa dini.

Ziara za Lowassa makanisani zinaendelea na wiki hii alipanga kwenda mkoa wa Mara lakini wana CCM wamepiga kelele na ziara yake kuahirisha ambapo itaendeshwa na mh. Kabaka .

Ukweli ni kwamba baadhi ya wachungaji wanapokea pesa za anasiasa kwa maslahi ya uchaguzi 2015.
 
Kuna kitu hakipo sawa kichwani kwa mtu huyu.
Eti maombi ya kupata magari.
Kibwetere huyu
OTIS
 
mmmmm!kaaaazi kwelikweli
kikwete achelewi kumfanya mzee wa upako kama alivyo mfanya mama lwakatare
yetu macho nakumbuka mwimbaji wa injili mnishi a.k.a malebo aliimba siasa na injili ni sawa na maji na mafuta
 
Si ndo huyu aliyesema kikwete ameletwa na mungu? Imekuwaje sasa hivi huyu mteule wa mungu ajae viroboto kichwani!
 
Hao watu wa gazeti la nyakati leo, nao ni wanafiki. Nadhani nao ni wanamtandao wa Lowassa. Inakuwaje wanakurupuka kuandika habari controversial kama hii? Wangekuwa na akili wangegundua kuwa lazima wasomaji wao watahiji juu ya huu msimamo wa askofu vs msimamo wake wa kumtetea na kumpaka mafuta Kikwete mwaka jana. Wangemuuliza hilo ili kubalance habari..
 
Duh, Ewe Mungu wa kweli uliyeumba mbingu na nchi iokoe TZ na watu wake. Tunaangamia kwa kukosa maarifa. Washindwe wenye nia mbaya na TZ kwa Jina la Yesu.
 
mmmmm!kaaaazi kwelikweli
kikwete achelewi kumfanya mzee wa upako kama alivyo mfanya mama lwakatare
yetu macho nakumbuka mwimbaji wa injili mnishi a.k.a malebo aliimba siasa na injili ni sawa na maji na mafuta

Mkuu,,mama Lwakatare JK kamfanya nn? Tafadhali kwa tusiojua
 
Mwacheni mzee wa upako atoe maoni yake kama anavyotaka,ww maoni yako ni yapi nasi tukuchambue.
 
viongozi wa dini wamekuwa waropokaji sana-si watu wa kuamini sana hawa-ni vigeugeu
 
Na muheshimu Mzee wa Upako katika hili kwa kuwa sio la kibibilia nachelea kusema, UMEANZA KUPOTEZA MUELEKEO. Angalia ulipodondokea ukatubu imetupasa kutii mamlaka zilizoweka dunia hata kama ziliingia kwa njia isiyo sahihi kwani hata Isaka alipata baraka kwa njia isiyo sahihi
 
Kwa kweli nchi hii ni ya kusifiwa na hasa JK. Watu hawa wana uhuru wa kuongea lolote kutokana na uhuru waliopewa na serikali yetu. Ndo maana mwendawazimu yeyote hata huyu aliyejivika uaskofu anaweza kuongea lolote, hasa wakati huu ambao mdudu ufisadi na ukosefu wa maadili kama kutakasa mafisadi na kuuza mihadarati vimejipenyeza katika nyumba za ibada.

Wacha atumikie mabwana waliomkodi, lakini sisi tunaendelea kujenga nchi, siyo hao wanaotapeli na kuwaweka utumwani watanzania wanaodhani kwamba hawa kweli ni watumishi wa Mungu.
 
Na muheshimu Mzee wa Upako katika hili kwa kuwa sio la kibibilia nachelea kusema, UMEANZA KUPOTEZA MUELEKEO. Angalia ulipodondokea ukatubu imetupasa kutii mamlaka zilizoweka dunia hata kama ziliingia kwa njia isiyo sahihi kwani hata Isaka alipata baraka kwa njia isiyo sahihi

Mkuu ulikuwa hujamjua tu, Alishapoteza muelekeo siku nyingi kama yule mwenzake wa round about ya kuelekea chuo kikuu cha mlimani.
 
Back
Top Bottom