Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM

Huu mkoa wa Zanzibar naona nao umezidi kelele, mbona wa mkoa wa Mwanza na kwingine kama Iringa, Mbeya wapo kimy tu, tunakalea kila siku lakini haka choki kudeka na kulalamika, aaaah, kama kamekua si kaende kakajitegemee bwana, kasehemu kenyewe kadogo, wilaya ya Mufindi kubwa!!!!
Mkulu alikuwa swaumu imemkubali au aliteleza ulimi?
"...Kwa ujumla tumeridhika kuwa utekelezaji umekuwa mzuri kwa upande wa mamlaka zinazohusika na usafirishaji majini yaani SUMATRA, Zanzibar Maritime Authority na mamlaka za Bandari za nchi zetu mbili. Ushirikiano baina ya mamlaka hizo sasa ni mzuri ....."
Source: hotuba ya mkulu. link nchizetumbili

je mikoa iko miwili? Mkoa wa Tanganyika na mkoa wa Zanzibar?

Let Zanzibar go! Au tunasubiri UAMSHO uwezeshwe na US na NATO? Sasa imekuwa kawaida kwa wababe hao kutafuta mwanya wa kuzichafua nchi zetu.
 
..huyu anapoteza muda wa watu tu.
Kaka, hii ndio typical example ya kitu ambacho nimekua nikikisema: Akitokea Mzanzibar anaedai Muungano uvunjwe Wabara - hata wale ambao hampendi Muungano - mnamshambulia. Tunakosea baba!

Pointi yangu ni kwamba, kwangu mimi chochote alichokisema huyu Mzee mwisho wa siku lake la langu letu moja, kuvunja Muungano! Sijui unanielewa? Kwamba, unapoanza kuwashambulia watu kama huyu unadhooshifa lengo au azma nzima ya kuvunja kwa Muungano.

Mimi nam support no matter what jibberish he may spew, as long as anataka tuvunje Muungano.
 
Taso,

..mimi nataka muungano uvunjike kabisa.

..sitaki habari ya muungano wa mkataba, kwasababu hata huu wa sasa hivi Karume na Nyerere walisaini mkataba.

..mwanzoni ilionekana kama vile wa-Znz wako serious na suala la kuvunja muungano, but recently wameanza ku-backtrack na kuja na hoja za "muungano wa mkataba", mara "muungano wa Uswisi," pamoja na ubabaishaji mwingine.
 
Bw Nguruvi3, siasa ni "game" kila mzanzibari ameshaangalia hatua mbili zaidi ya hapa tulipo. Muungano mtauvunja nyinyi wenyewe (watanganyika) kwa kiburi , dharau na jeuri yenu. Mkataba ni chambo tu, mkitaka mtakula hamtaki mtaacha. LET ZNZ GO ! hii mtawakomoa wale vingunge wa CCM sio wazanzibari wa kawaida.
Huu ni mwanzo wa mwisho...
Mkuu Takashi, kila siku tunasikia serikali 3 WZNZ wanadai. Tunasikia mkataba na kichekesho mwanasheria Mkuu wa SMZ akasema muungano wa Uswiss.

Tumeuliza hapa mara 1000, hebu tuambieni serikali 3,Tanganyika, Zanzibar na Muungano, hiyo ya muungano wenzetu mnaweka nini mezani kuiendesha? Maana hii iliyopo mnaweka 0 mnapata kiasi kizuri tu cha asilimia 7 na zingine za pembeni.

Tumeuliza huo mkataba ni wa mambo gani ? kwasababu ZNZ wanabendera, wimbo wa Taifa wanataka kiti UN na EAC, wanataka kujiunga na OIC sasa hapo kuna jambo gani tutakaloshirikiana?
Tungeweza kushirikiana nishati kama umeme lakini wenzetu kuanzia maskani hadi Ikulu hamtaki kulipa.

Au mnataka ushirikiano wa ulinzi na usalama msiokuwa na bajeti nao! Maana ZNZ haina bajeti ya ulinzi ingawa ina amir jeshi!

Tungeweza kusema tushirikiane katika bunge, wenzetu mnawatuma watu kwenda Dodoma bila kuwapa nauli au malazi.
Tungesema tushirikiane katika utamaduni, wenzetu wenu ni wa kiarabu
Tungesema tushirikiane elimu, wenzetu mnatuma watoto waje kusoma bila ada au matumizi.

ZNZ haihitaji Tanganyika irudi ili muungano uvunjike, inahitaji Tanganyika ili iweke mirija pale pagumu.
Umewahi kusikia Watanganyika wangapi wanasema mkataba au serikali 3.
Siku hizi wanasema LET THEM GO! LET ZNZ GO! Maana yake ni kuwa ZNZ ikiondoka hewala, ikibaki basi itulie kimya kama 'koloni'.Choice ni yenu.

Mkuu Chama unachosema ni kweli Mzee Moyo hana nauli, sasa anapiga story za nani alikuwepo siku ya mapinduzi.
Takashi hakuwepo, je hiyo inamfanya asiwe MZNZ. Mzee Moyo kachanganyikiwa kuwa nje ya ulingo kama alivyochanganyikiwa Maalimu Sefu.

Mwisho, ukisikiliza maoni ya WZNZ mbele ya tume wote wanasema wanataka muungano lakini.... Haaa! sasa Takashi anasema wanaona hatua mbili mbele, yaweza kuwa wanaona mbele kitakachowasibu muungano ukikatika.

LET ZNZ GO! We have nothing to lose! absolutely nothing
 
Namuunga mkono Mzee Moyo. Ila kwanza tuuvunje huu muungano kero ili kila mtu chukue chake halafu baada ya hapo tukutane kama nchi mbili huru kujadili huo mkataba wanaousema hawa akina Mzee Moyo. Tunaweza kuendelea na ushirikiano na wazanzibari katika "framework" ya jumuiya ya Africa Mashariki na sio katika huu muundo popo wa muungano.
 
Watu wengine bana sasa kama anataka kudai Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanini asirudishe kadi tu ya CCM na kuasisi chama kitakachodai Jamhuri hiyo? Tena kutokana na uzoefu wake angeweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaotaka Zanzibar itokwe kwenye Muungano.

Wala hahitaji kuanzisha chama ili kuendeleza vuguvugu la kudai Zanzibar huru. Tayari kuna vuguvugu la uamsho ambao unaungwa mkono na wanachama wa CUF na CCM. Yeye angejitoa CCM na kujitambulisha rasmi na vuguvugu la Uamsho ili awongezee nguvu katika kushinikiza kupatikana kwa jamhuri huru ya watu wa Zanzibar.
 
Huyu Mzee Moyo ana mke Tanga na Mtwara huu muungano ukivunjika si atakuwa na kazi ya kuuomba viza kila siku kuwatembelea hao wake zake?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kwa umri wake hivi sasa hana cha kupoteza hata waarabu wa Oman wakiamua kuitawala upya Zanzibar!
 
This is the folly of mankind; we can not appreciate something till it is no more!! Wazenj wataulilia muungano na kusaga meno pale utakapokuwa haupo tena!! wanaviona vinaelea wanasahau viliundwa?! jamani hata Hassan nassoro Moyo tena?! kweli mfadhili mbuzi waweza kumla nyama lakini binadamu atakuudhi.

Mzee Moyo sio wa kwanza kutoa msimamo wa kuwa na muungano wa mkataba, kama ulimsikiliza vizuri mama Karume alipokuwa anahojiwa na waandishi wa habari ,yeye pia alikuwa na msimamo kama huo wa Moyo!! Kama mama Karume ana msimamo wa UAMSHO je itakuwa sio sahihi kuhisi kuwa hata mwanae Rais Mstaafu wa Zanzibar ana msimamo kama huo?
 
Wazanzibari hawajielewi hawataki kusoma na kufanya kazi wanajenga misikiti tu matatizo yao ya kijamii na kiuchumi wanatupia serikali ya muungano wao wana rais wao, wanabaraza lao la mapinduzi, wanamawaziri, wana makamu wa rais wawili, uwanja wa ndege, na bandari si wasolve matatizo yao? sisi ndo tunaotakiwa tulilie Tanganyika yetu wamekaa kupiga domo tu. ukifika wakati wa uchaguzi wanaenda kwenye masanduku ya kura kuchagua wabunge wa muungano na raisi wa Muungano kama hawautaki si waache kuchagua viongozi katika ngazi hizo mbili tujue moja hakuna mwakilishi toka znz katika bunge? mihadhara haitawasaidia kama kuchagua rais wa muungano wanachagua wenyewe. wanafiki wakubwa hawa watu.
 
Kama utaangalia jawabu yangu hii ambayo umeniuliza maswali, utagundua kuwa kwanye badiko langu la #2nilitumia neno MUAMSHO kwa kejeli kutokana na tabia iliyozuka hapa ya kuwapachika jina hilo wale wote wanaotetea mabadiliko ya Muungano, hata kama wanatoka ndani ya GNU au wanachama wa CCM, jambo ambalo sio kweli na ninalipinga.

Na ndio maana nikasema kuwa hatuna uvumilivu wala demokrasia ya kukubali hoja ya mawazo ya wenzetu. Ni aibu kuwa kila jambo tunalisukuma kwenye dini na itikadi za vyama na kusahau maslahi ya nchi kwanza.

nimekusoma...tuko pamoja!!!
 
Mkuu Takashi, kila siku tunasikia serikali 3 WZNZ wanadai. Tunasikia mkataba na kichekesho mwanasheria Mkuu wa SMZ akasema muungano wa Uswiss.

Tumeuliza hapa mara 1000, hebu tuambieni serikali 3,Tanganyika, Zanzibar na Muungano, hiyo ya muungano wenzetu mnaweka nini mezani kuiendesha? Maana hii iliyopo mnaweka 0 mnapata kiasi kizuri tu cha asilimia 7 na zingine za pembeni.

Tumeuliza huo mkataba ni wa mambo gani ? kwasababu ZNZ wanabendera, wimbo wa Taifa wanataka kiti UN na EAC, wanataka kujiunga na OIC sasa hapo kuna jambo gani tutakaloshirikiana?
Tungeweza kushirikiana nishati kama umeme lakini wenzetu kuanzia maskani hadi Ikulu hamtaki kulipa.

Au mnataka ushirikiano wa ulinzi na usalama msiokuwa na bajeti nao! Maana ZNZ haina bajeti ya ulinzi ingawa ina amir jeshi!

Tungeweza kusema tushirikiane katika bunge, wenzetu mnawatuma watu kwenda Dodoma bila kuwapa nauli au malazi.
Tungesema tushirikiane katika utamaduni, wenzetu wenu ni wa kiarabu
Tungesema tushirikiane elimu, wenzetu mnatuma watoto waje kusoma bila ada au matumizi.

ZNZ haihitaji Tanganyika irudi ili muungano uvunjike, inahitaji Tanganyika ili iweke mirija pale pagumu.
Umewahi kusikia Watanganyika wangapi wanasema mkataba au serikali 3.
Siku hizi wanasema LET THEM GO! LET ZNZ GO! Maana yake ni kuwa ZNZ ikiondoka hewala, ikibaki basi itulie kimya kama 'koloni'.Choice ni yenu.

Mkuu Chama unachosema ni kweli Mzee Moyo hana nauli, sasa anapiga story za nani alikuwepo siku ya mapinduzi.
Takashi hakuwepo, je hiyo inamfanya asiwe MZNZ. Mzee Moyo kachanganyikiwa kuwa nje ya ulingo kama alivyochanganyikiwa Maalimu Sefu.

Mwisho, ukisikiliza maoni ya WZNZ mbele ya tume wote wanasema wanataka muungano lakini.... Haaa! sasa Takashi anasema wanaona hatua mbili mbele, yaweza kuwa wanaona mbele kitakachowasibu muungano ukikatika.

LET ZNZ GO! We have nothing to lose! absolutely nothing
I love this line...
 
wazanzibari hawajielewi hawataki kusoma na kufanya kazi wanajenga misikiti tu matatizo yao ya kijamii na kiuchumi wanatupia serikali ya muungano wao wana rais wao, wanabaraza lao la mapinduzi, wanamawaziri, wana makamu wa rais wawili, uwanja wa ndege, na bandari si wasolve matatizo yao? Sisi ndo tunaotakiwa tulilie tanganyika yetu wamekaa kupiga domo tu. Ukifika wakati wa uchaguzi wanaenda kwenye masanduku ya kura kuchagua wabunge wa muungano na raisi wa muungano kama hawautaki si waache kuchagua viongozi katika ngazi hizo mbili tujue moja hakuna mwakilishi toka znz katika bunge? Mihadhara haitawasaidia kama kuchagua rais wa muungano wanachagua wenyewe. Wanafiki wakubwa hawa watu.
sawa ! Lakini unajua maana ya unafiki? Unasema wazanzibar hawataki kusoma unazo takwimu au tukusaidie? Mm naona unaporojo tu zisizo mashiko!
 
..huyu anapoteza muda wa watu tu.

..muungano wa mkataba ndiyo kitu gani?

..mbona Nyerere na Karume walisaini mkataba??

si nasikia huyu mzee wakati mjadala terms za muungano zinajadiriwa na nyerere na karume - yeye alikuwa saloon ananyoa nywere na ndevu, au bado ana hasira hizo, anataka kukomoa?
 
Taso,

..mimi nataka muungano uvunjike kabisa.

..sitaki habari ya muungano wa mkataba, kwasababu hata huu wa sasa hivi Karume na Nyerere walisaini mkataba.

..mwanzoni ilionekana kama vile wa-Znz wako serious na suala la kuvunja muungano, but recently wameanza ku-backtrack na kuja na hoja za "muungano wa mkataba", mara "muungano wa Uswisi," pamoja na ubabaishaji mwingine.
Wewe unaetaka Muungano uvunjike kabisa , mimi na wewe na Uamsho, Nguruvi3 ni kundi moja. Lakini kila mtanganyika na mzanzibari ( individuals ) wana haki ya kua na maoni tofauti na yako wewe... Wazanzibari wote wanataka Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Tunatofauti katika uhusiano gani baina ya Tanganyika na Zanzibar uwe? Wapo wachache wanaolipwa na CCM , kulazimisha mfumo huu uliyopo sasa uendelee.

Wapo wanaotaka mkataba na wapo wasiotaka kabisa wale niliowataja hapo mwanzo.
Mwisho wa yote suluhu itapatikana kwa kura ya maoni. Na hicho ndicho ambacho mpaka sasa watawala bado wanakiogopa. As for myself , I truly like your slogan ( let znz go !) ha ha ha...
 
Huyu Mzee Moyo ana mke Tanga na Mtwara huu muungano ukivunjika si atakuwa na kazi ya kuuomba viza kila siku kuwatembelea hao wake zake?

Chama
Gongo la mboto DSM

Wanzanzibari wameowa hadi Japani, Marekani na Ulaya ...sasa kuna ugumu gani kwenda Tanga na kurudi?
 
Mwanangu Ali Nasor Moyo mnafiki. Mbona alipokuwa akila vinono vya muungano alipopewa uwaziri kwanini hakuyasema haya anayosema? Njaa wakati mwingine ni ugonjwa tena wa akili.

Amestaafu na kuona uzee unazidi huku hana heshima wala pa kuchuma ameamua kujiingiza kwenye makundi ya kihuni! Kumbe wakati mwingine ni ukweli kusema mtu mzima hovyo. Moyo akiregesha hiyo kadi ya CCM haitakuwa kitu.

Heri angeshauri watu wakae kistaarabu na kudurusu hoja na historia za muungano. Kwani zanzibar kuna waanzilishi wa muungano kama wanavyojiita au mwanzilishi ni mmoja tu Karume aliyetaka kuepuka kupinduliwa na washenzi wa kiarabu?
 
Back
Top Bottom