Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM

Hivi jamani hadi hii leo bado kuna baadhi ya watu kiswahili kinawapa tabu kiasi hichi yaaani kinawapa mashaka kukifahamu? Mzee Hassan alisema kama hivi ifuatavyo ... ikiwa atamuwa kurejesha kadi yaani kwa hiyari yake basi atampa Mzee piusi msekwa kwani ndie aliyebakia muasisi mwenziwe wa CCM (kumbe kulikuwa na haja ya kuweka kiswahili kuwa lugha ya taifa)

ahsante kwa kuliona hili watu tunachangia mjadala bila kusoma na kuelewa
 
Anachokiongea Mzee Moyo ni kujibu yale mapigo ya kina Nape walipoanza kuwatisha watu wazima warejeshe kadi zao, kajibu hoja kiungwana kwamba wakumchallenge katika kudai kadi yake ni wazee wenzake walioanzisha chama sio Nape na genge lake. Unaweza kutafautiana nae katika hoja zake juu ya muungano, huo ndio uhuru wa utoaji hoja, kila mtu anamtazamo wake.

Tuje katika suala hili na threats zinazotolewa za kuwafukuza chamani wenye kutoa maoni tafauti na imani ya chama hususan katika jambo linalolihusu taifa na kuundiwa kamati huru kwa kila mwananchi kutoa maoni yake juu ya katiba tuitakayo.

Ikiwa vitisho juu ya wanachama wa CCM wenye maoni tafauti na itikadi ya chama vitaendelezwa basi zoezi zima la ukusanyaji wa maoni halitakuwa na uzito wowote kilogic hata kisheria. Tukichukuwa statistics za uchaguzi wa mwaka 2010, CCM ndio chama kilichoungwa mkono na wananchi waliowengi. Kundi kubwa la walioipigia kura CCM ni wanachama wake na wapenzi wake, ushindi wa asilimia 60 (kama sikosei) ni mkubwa na kuwanyima uhuru wapiga kura hao wote ambao ni wafuasi wa CCM uwezo wa kutoa maoni yao juu ya katiba ya nchi (sio ya chama) ni kutoifanyia haki katiba ya nchi.

Vyama vinatakiwa kutoa uhuru wa wanachama wake katika masuala yanayohusu katiba ya nchi kutoa maoni yao kwani katiba haitakuwa ya chama fulani wala haitawekwa kwa misingi ya kuifanyia upendeleo chama kimoja kwani ni katiba ya nchi na wananchi wote. Utamkuta kiongozi tena kijana akiwashutumu na kuwatisha wenzake watu wazima waasisi wa hiyo katiba tunayoirekebisha kutotoa maoni yao kwa sababu ya policy za chama huku akijinadi kuwa ndio mwanademkorasia wa leo wanaowawakilisha vijana akisahau nguzo kuu ya demokrasia ni katiba huru kwa wananchi wote.

nchi imegubikwa na genge la wasanii, wafitini na mafisadi walio tayari kuzuia kila harakati zenye misimamo ya demokrasia ya kweli kwa kuhofu nafasi zao na future ya matumbo yao. Wakati wa kutishana si wa sasa, uhuru wa maoni ya wananchi inevitable la si hivyo utakosa legitimacy ya kuitwa mtawala halali.
 
Well done Mzeee Moyo kwa kuonesha ujasiri mkubwa nina imani na hao akina vibaraka wengine watafanya kma ufanyavyo...zanzibar kwanza mambo mengine baadae
 
Au Msekwa akifa je?Huyu mzee Moyo anang'ang'ania unyasi anajua zake zimeshawadia.

Aache longolongo, na anajua fika akiondoka tu CCM mafisi watamla live.
 
Mkuu kumbe wenye kadi namha 1 hawawezi kurudisha kww kuwa kutakuwa hakuna wa kumrudishia? Katika vyama ama jumuiya zozote ukikubaliwa kua mwanachama basi unakuwa na haki sawa na manachama namba 1 ama namba 100,000.

Wakuu naomba hiyo Kadi No. 1 iwe "special reserve" na isizungumziwe kwenye mijadala ya kijuha kama hii. Kama ni lazima sana basi izungumziwe kwenye issues na sio upuuzi kama huu wa nani anamdai nani kadi, sitairudisha kwa fulani, n.k. Hiyo ni kadi ya kipenzi chetu, mwasisi na Baba wa Taifa letu; Jemadari na Kamanda Mkuu wa nyakati zake, Mwl. Julius Kambarage Nyerere (RIP).
 
Mzee Msekwa si yupo?!! Kwa nini basi asimkabidhi hiyo kadi? Anyways, ni aidha serikali moja au Zanzibar muende zenu.
 
Kwa nini Balozi Iddi au yeyote anayehisi ana maamuzi ndani ya CCM Zanzibar wasiwafukuze tu ndani ya chama wale wanawaona wanakwenda kinyume na msimamo wa chama, badala ya kutoa maneno ya vitisho na kubembelezana?
 
Mzee wangu Nassor Moyo ktk hili unachemsha wala sii kidogo.. CCM uloijenga wewe sio hii tena maana nakumbuka enzi zile hata msingefikia muafaka na CUF kutokana na historia ya Hizbu. Mambo mengi sana yamebadilka na Wazanzibar wamefikia mahala kuwa wamoja hivyo kuunda umoja wao baada ya kuweka tofauti zao pembeni na wewe kama Mzanzibar umetoka ktk msimamo wa CCM chama kilichowaunganisha ASP na TANU.

Hivyo ingekuwa jambo jema sana kama utajitoa kabisa CCM hii na kuwashauri Wazanzibar hatua inayofuata ni kuunganisha vyama hivi wanaCCM (visiwani) na CUF visiwani ili mpate chama kimoja cha Wazanzibar ambacho kisheria kitagombea Uongozi wa Zanzibar. Hii ndio dawa pekee kwa Wazanzibar kujitenga kisheria na kilaini kabisa maana chama kitawakilisha mawazo yenu wote..Bila shaka chama hiki hakitakuwa na mshindani maana CCM pasipo support ya Baraza la Mapinduzi haiwezi kushinda Zanzibar..

Swali langu kwako Je, hilo baraza la Mapinduzi liko tayari kurejesha dhamana hiyo kwa Wazanzibar wote pasipo kujali historia ya Mapinduzi?. Mambo mengine mepesi sana kuyasema ama kuyadai wakati njia zipo rahisi kabisa undeni chama kimoja na safari inazie hapo. Ni jambo zuri sana kuzungumzia serikali tatu japokuwa haitatosha maana ukweli unatakiwa kuzungumzwa ya kwamba Bara na Visiwani hawana mapenzi wala undugu wa dhati bali tumelazimishwa ktk ndoa hii na fikra zenu wenyewe kuhusu Pan Africanism. Hivyo, maadam leo imebainika kwamba Pan Africanism haiwezekani kama tulivyoshindwa UJAMAA basi bora kabisa tujitenge na kila mtu ajue lake tukutane AU na OAU lakini kwa fikra hizo hizo wafikirieni pia hatma ya Wazanzibara...
 
[h=3]
IMG_1450.JPG
[/h] Muasisi Mkongwe Hassan Nassor Moyo

Na Husna Mohammed

WANANCHI wametakiwa kujali maslahi ya nchi kwanza na baadae chama, kwa lengo la kuweka mustakabali mzuri wa nchi.

Hayo aliyasemwa jana na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo, wakati akizungumza katika mjadala kwa vyombo vya habari kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika hoteli ya Mazsons Mjini Zanzibar.


Alisema wananchi na hata baadhi ya viongozi wamekuwa wakinasibisha muungano na chama jambo ambalo wamekuwa wakiwapotosha wananchi kujua ukweli wa mambo na hivyo kuwakosesha fursa muhimu ya kudai maslahi ya nchi yao.


Alifahamisha kuwa yeye kama muasisi wa muungano hakubaliani na uamuzi huo na kwamba iko kila sababu ya kudai maslahi ya Zanzibar pamoja na watu wake hasa ikizingatiwa kuwa makubaliano ya muungano hayako kisheria.


"Mimi nitakuwa miongoni mwa watu watakaoulizwa kesho mbele ya Mungu kuhusiana na mstakbali wa nchi hii kwa nini najua ukweli nisiwaeleze wasioujua, huu ni ukweli halisi na mimi kama muasisi nabeba dhima hii mpaka mbele ya Mungu," alisema.



Sambamba na hilo lakini muasisi huyo alisema ukiangalia kiundani muungano huo umetawaliwa na udugu zaidi kwa kuwa si wa kikatiba wala kisheria.


"Tangu mwanzo muungano huu hauna mambo mazuri kwa nini tunapohoji katika mambo muhimu yamekuwa hayatekelezwi labda kwa kuwa hauko kisheria wala kikatiba, sheria ya Zanzibar hakuna kitu kinachozungumzia muungano, pia mawazo ya muungano hayakuzungumzwa katika baraza la Mapinduzi wakati huo, wakati umefika sasa kufanya mabadiliko kwa maslahi ya nchi yetu na vizazi vyetu," alisema.


"Kuna sehemu alitakiwa Mzee Karume kutia saini lakini hakuweka saini hiyo na sisi wakati huo tulikwenda Tanganyika kudai baadhi ya mambo hayati Nyerere alisema bado wakati wake, sasa wakati umefika vijana kudai …… tumieni mwanya wa katiba mpya," alisisitiza.


Akijibu suala aliloulizwa kuhusu kurudisha kadi au kujitoa katika chama cha Mapinduzi, Mzee Moyo, alisema yeye hawezi kufanya hivyo, na hakuna mtu wa kumlazimisha kurejesha kadi ya chama hicho.


"Kwa taarifa yenu mimi ni mwanachama halisi mwenye kadi nambari 7 ya chama hivyo hakuna mtu yoyote atakaenihoji kurejesha kadi yangu kwa kuzungumzia maslahi ya nchi yangu," alisema.
"Wazanzibari Muungano wanautaka lakini ni lazima kufanywe mabadiliko na hivyo wanavyosema uamsho mara nani hataki muungano hiyo ni kuwapotosha wasiojua nasema hivyo kwa maslahi ya nchi yangu," alisisitiza.


Nae Profesa Abdul Sharif, akiwasilisha mada juu ya wajibu wa dhima ya vyombo vya habari katika kuripoti habari za Muungano, alionesha wasiwasi wake kwa mambo yatakayofikiwa katika katiba mpya kama yatakubaliwa sambamba na kutekelezwa kwa maoni ya watu wa Zanzibar.


Sambamba na hilo pia alisema kuna uwezekano wa kutopatikana majibu muafaka kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na uelewa kueleza bayana juu ya maslahi ya Zanzibar katika mchakato wa kutoa maoni ya katiba mpya.


Akizungumzia kuhusu mambo ya kisheria yanayopitishwa bungeni, Profesa Sharif, alisema mambo mengi yanayopitishwa kisheria bungeni yamekuwa yakiwanyima fursa wabunge wa Zanzibar kwa kuwa wao ni asilimia 20 na Tanzania Bara ni asilimia 80, hivyo uwakilishi wa kuamua mambo unakuwa ni mkubwa kwao.


"Hata kama watakataa wabunge kutoka Zanzibar basi si kitu kwa kuwa utaratibu umeonesha hivyo sheria ya bunge inahitaji marekebisho kwa kuwa mambo mengi yamekuwa yakifanyika kwa maslahi yao," alisema.
Kwa upande wake Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, alisema kimsingi mambo yaliyokuwepo sasa ni vichekesho kwa kuwa hakuna uthibitisho wa mambo ya muungano hasa ukizingatiwa kuwa hakuna katika katiba wala sheria.


Alisema Mwanasheria wa mwanzo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hakupewa nafasi yake ya kuweza kuhoji mambo ya muungano, hivyo dhana ya mambo matatu muhimu katika muungano hayapo tena ikiwa ni kwa Serikali ya Zanzibar, Tanganyika na Serikali ya Muungano.



"Kwa kuwa mkataba ni jambo la hiyari baina ya pande zote mbili hivyo ni lazima kukubaliana na kuridhiana baina ya pande hizo, kutokana na hilo dhima ya Zanzibar ikishindikana ni kupigwa kura ya maoni," alisema.
Nae mwandishi wa habari wa siku nyingi Enzi Talib Aboud, alisema Baraza la Mapinduzi limeshakaa mara mbili kutaka kufanyiwa kazi baadhi ya mambo muhimu lakini upande mmoja unashindwa kutekeleza.


Enzi aliwataka waandishi wa habari kuijua historia ya Zanzibar hasa kwa masuala ya muungano jambo ambalo litawawezesha kuhoji na kuuliza kuhusu mambo muhimu ya Zanziba na watu wake.


Mapema Ofisa Mipango wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) ofisi ya Zanzibar, Shifaa Said Hassan, alisema waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kuwaelimisha wananchi juu ya muungano.


Alisema lengo la mjadala huo ni kuona kuwa vyombo vya habari vinafanya wajibu wake katika kuzungumzia muungano kwa umma, hasa kwa kuwa mijadala kama hiyo imekuwa ikizungumzwa siku zote.

Mjadala huo umetayarishwa na Baraza la Habari Tanzania, ofisi ya Zanzibar ambapo uliwakutanisha waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali pamoja na wadau kutoka sekta ya serikali na binafsi.


Imewekwa na MAPARA at 8:56 PM
 
Bonyeza kumsikiliza Muasisi wa Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo Part 1,2 na 3

VIDEO- MUUNGANO NAUJUWA KAMA JINA LANGU ‘HASSAN NASSOR MOYO’ | Mzalendo.net

www.mzalendo


Kuna siri gani hasa wabara wakawa vingaganizi ukiwatajia Muungano? hushangazwa na kusema kauli zisizo na mandiki eti tukiiwacha Zanzibar kujutawala wenyewe watakufaa njaa ,jee Zanzibar na Tanganyika si zilikuwa nchi mbili tafauti? na kama udugu na ujirani Tanganyika si imebakana kimipaka ya Land na nchi nyingi .
 
Kuna siri gani hasa wabara wakawa vingaganizi ukiwatajia Muungano? hushangazwa na kusema kauli zisizo na mandiki eti tukiiwacha Zanzibar kujutawala wenyewe watakufaa njaa ,jee Zanzibar na Tanganyika si zilikuwa nchi mbili tafauti? na kama udugu na ujirani Tanganyika si imebakana kimipaka ya Land na nchi nyingi .

Nani kakuambia wabara tunaung'ang'ania Muungano?! CCM ndio wanaung'ang'ania Muungano. Kama waznz hamuutaki Muungano just go. Si BLW lipo? Au BLW haina meno? Na kwa nini wale wabunge wenu wanaoingia Bunge la JMT wasilete hoja binafsi kuvunja Muungano na nyinyi kuwa huru. Kelele za mtandaoni hazisaidii kitu bila hatua za kivitendo. Chukueni hatua ama sivyo basi zitakuwa kelele za bata tuu, paaah paaah paaaah!
 
waasisi wa muungano waliobaki ni wawili kwa mujibu wa maelezo ya viongozi wa ccm Zanzibar kwanini bado mnampa cheo cha uasisi nassoro moyo si mueleze tu hoja zake kama zilivyo
 
DSC_1558.JPG


Muasisi wa Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo
Bonyeza Sauti

video-muungano-naujuwa-kama-jina-langu-hassan-nassor-moyo-4
 
Kakke, takashi, Nguruvi3, abdulahsaf,

..naona hawa waheshimiwa wanapenda sana kulalamika.

..Jussa alikuwa mbunge ktk bunge la muungano, nini kilimzuia kupeleka hoja zake kuhusu kero za muungano?

..zaidi, Jussa ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, je, nini kimemzuia kuwasilisha hoja ya kutangaza mgogoro wa muungano?

..mimi nadhani hawa wameridhika na hii nafasi yao ya kuwa walalamishi siku zote.
 
Last edited by a moderator:
Kakke, takashi, Nguruvi3, abdulahsaf,

..naona hawa waheshimiwa wanapenda sana kulalamika.

..Jussa alikuwa mbunge ktk bunge la muungano, nini kilimzuia kupeleka hoja zake kuhusu kero za muungano?

..zaidi, Jussa ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, je, nini kimemzuia kuwasilisha hoja ya kutangaza mgogoro wa muungano?

..mimi nadhani hawa wameridhika na hii nafasi yao ya kuwa walalamishi siku zote.
Joka Kuu, mbona kuna mgongano! Jusa alisema muungano uvunjike, ghafla anataka serikali 3.
Maalim anataka serikali 3, Ahmed anasema zimepitwa na wakati anataka mkataba. Shivji anasema ili kuanza upya lazima mjitoe, umma wa wazanzibar unamjia juu tujitoe wapi!
Nasor Moyo anasema harudishi kadi atakujaje kuangalia nyumba zake msasani na Ukonga.

Sasa mkuu Joka, Jusa angepeleka hoja ya kuwa wazanzibar wanataka nini? Yeye mwenyewe hajui anataka nini, Ahmed anakwenda kasakazini Maalimu magharibi hoja itaandikwa vipi.

Hawa ni walalamishi wakiambiwa mbinu za kujitoa katika muungano wanasema fanyeni ninyi, tukikaa kimya wanasema ninyi wakoloni.

Mbinu nyingine rahisi tunawapa, tengenezeni passport za Zanzibar, kataeni viatmbulisho wa Tanzania!

Mkishindwa kufanya kitu, kaeni kimya, mfunge midomo msubiri maziwa na asali. Acheni kidomo domo, uzushi, uzandiki na fitna. Mnaiihitaji Tanganyika!
Mnonewa wakati mnataka mkataba. Mnaibiwa wakati mnataka serikali 3! Mnataka muwe huru wakati mnadai EU!
 
Back
Top Bottom