Mzee Hassan Nassor Moyo: Kauli yake juu ya Muungano na hatma ya Uanachama wake ndani ya CCM

Huyu Moyo anatumia Masaburi kuwaza...hivi nikiwauliza wazenji Tunawanyonya Kitu gani nyie?????

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
uwe na heshima na watu waliokuzidi umri, hilo ni tusi.sasa ngoja na wewe tukujibu
labda unawanyonya dhakkar.
 
Huyu Mzee wetu na yeye MUAMSHO nini?

waswahili bwana, kila mwenye mawazo tofauti ana kasoro...bara ataitwa MUAMSHO na Znz ataitwa HIZBU!!!

ni lini watu watajadili issues na si mitazamo ya watu??!!!!
 
waswahili bwana, kila mwenye mawazo tofauti ana kasoro...bara ataitwa MUAMSHO na Znz ataitwa HIZBU!!!

ni lini watu watajadili issues na si mitazamo ya watu??!!!!
Ni pale tutakapokuwa na demokrasia ya kweli tukianza na demokrasia ndani ya suala zima la Muungano; ni pale ambapo tutakuwa na uvumilivu wa kuthamini mawazo ya mtu bila ya kumpachika jina la dini, itikadi ya kisiasa au jimbo; ni pale ambapo tutaanza kujadili na kushughulikia maendeleo badala ya kulalamika. Kwa vile siku hivyo bado, sio Mzee Moyo, Mtanzania yeyote ambae ana mawazo tafauti na ya wengine, atasakamwa na kupachkwa majina ya kila namna.
 
ni wazi sasa kuwa kuvunjika kwa muungano kutaanzia Zanzibar kama ulivoanzia huko kwa wazo la Karume
 
Ni pale tutakapokuwa na demokrasia ya kweli tukianza na demokrasia ndani ya suala zima la Muungano; ni pale ambapo tutakuwa na uvumilivu wa kuthamini mawazo ya mtu bila ya kumpachika jina la dini, itikadi ya kisiasa au jimbo; ni pale ambapo tutaanza kujadili na kushughulikia maendeleo badala ya kulalamika. Kwa vile siku hivyo bado, sio Mzee Moyo, Mtanzania yeyote ambae ana mawazo tafauti na ya wengine, atasakamwa na kupachkwa majina ya kila namna.

Well said...

Lakini si ni kweli hatua huanza na moja??? vinginevyo ni kipi kinakufanya uone siku hiyo haijafika na kama ni kweli kuwa haijafika ni kipi kitakujulisha kuwa siku hiyo imefika....na kama maswali hayo hayatoshi, ni nani wa kutuonyesha njia ya kuelekea katika siku hiyo mpaka iwe..............

......Kwa vile siku hivyo bado, sio Mzee Moyo, Mtanzania yeyote ambae ana mawazo tafauti na ya wengine, atasakamwa na kupachkwa majina ya kila namna.

Nadhani wewe, mimi na yule tusiwe ni miongoni mwa wenye sifa hizo za kupachika watu majina.....it should begin with us, otherwise, who else???
 
Huu ni UDHAIFU wa ccm na Viongozi wake, sasa huyu moyo na hawa vijana wasomi wa UAMSHO, wanakumbatia za nini Kadi za ccm kama si unafiki wa nataka sitaki?
 
MAMMAMIA hapa tulipo fikia tuiache Zanzibar iamue mstakabali wake. Wiki iliyopita niliposoma hotuba ya Alli Ameir nilitambua kwamba analalilia Muungano kwasababu zake binafsi siyo kwa maslahi ya Zanzibar.

Ni Msomi Zanzibar iko chini ya Usawa wa Bahari; Na Global Warming is threatening small Island kwahiyo anataka

Ardhi kwa Wazanzibari; Wengi Hawataweza kuogelea Mpaka Oman Salama
 
Well said...

Lakini si ni kweli hatua huanza na moja??? vinginevyo ni kipi kinakufanya uone siku hiyo haijafika na kama ni kweli kuwa haijafika ni kipi kitakujulisha kuwa siku hiyo imefika....na kama maswali hayo hayatoshi, ni nani wa kutuonyesha njia ya kuelekea katika siku hiyo mpaka iwe..............

Nadhani wewe, mimi na yule tusiwe ni miongoni mwa wenye sifa hizo za kupachika watu majina.....it should begin with us, otherwise, who else???
Kama utaangalia jawabu yangu hii ambayo umeniuliza maswali, utagundua kuwa kwanye badiko langu la #2nilitumia neno MUAMSHO kwa kejeli kutokana na tabia iliyozuka hapa ya kuwapachika jina hilo wale wote wanaotetea mabadiliko ya Muungano, hata kama wanatoka ndani ya GNU au wanachama wa CCM, jambo ambalo sio kweli na ninalipinga.

Na ndio maana nikasema kuwa hatuna uvumilivu wala demokrasia ya kukubali hoja ya mawazo ya wenzetu. Ni aibu kuwa kila jambo tunalisukuma kwenye dini na itikadi za vyama na kusahau maslahi ya nchi kwanza.
 
kadi ya ccm hata nape nauye alishaitupaga hata hakuirudisha hivyo huyo mzee hafanyi jipya saaana.ishu hapo ni huo msimamo wake kuhusu muungano na mustakbali wa zanzibar
 
Nyinyi Wabongo mtamlea nani wakati nyinyi wenyewe mnakufa na njaa? Au babu hujuwi kama Bongo ni nchi ya pili duniani kwa umasikini tizama kwenye orotha ya United Nations nchi masikini duniani halafu ndo useme kelbu we.
 
Mkuu, inapofikia mahali Mzee kama huyu naye anasema tu bila kuwa na ground, lipo tatizo.

Wznz wanataka sana muungano hawasemi tu ndiyo maana wamebaki kuzunguka mbuyu wakiimba serikali 3, mkataba, ushirikiano, mkataba wa Uswis n.k. Kelele zote za Vunja muungano sasa kimyaaa!

Wanajaribu kutikisa kibiriti, wamuulize Salimin Amour aliyekwenda Dodoma kwa mbwembe, baada ya kikao akarudi na kukuta kila kitu 'upside down' wakiwemo walinzi wake. Kuanzia siku hiyo hadi leo Komandoo Kimyaa.

Huyu Moyo mtoto wake si alitaka kugombea Ubunge Bara kama alivyokuwa wa Mwinyi n.k. Sasa analeta kelele mtoto wake atagombea wapi next time, maana Tanganyika inazinduka, hakuna kumuonea mtu huruma.

ZNZ semeni, mkataba unahusu nini?
Serikali 3 mtachangia nini kuendesha hiyo ya tatu?
Serikali 3, hiyo ya tatu itafanya kitu gani zaidi ya zile mbili?

LET ZNZ GO!

Bw Nguruvi3, siasa ni "game" kila mzanzibari ameshaangalia hatua mbili zaidi ya hapa tulipo. Muungano mtauvunja nyinyi wenyewe (watanganyika) kwa kiburi , dharau na jeuri yenu. Mkataba ni chambo tu, mkitaka mtakula hamtaki mtaacha. LET ZNZ GO ! hii mtawakomoa wale vingunge wa CCM sio wazanzibari wa kawaida.

Huu ni mwanzo wa mwisho...
 
Watu wengine bana sasa kama anataka kudai Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanini asirudishe kadi tu ya CCM na kuasisi chama kitakachodai Jamhuri hiyo? Tena kutokana na uzoefu wake angeweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaotaka Zanzibar itokwe kwenye Muungano.
 
Kwa kweli nakupongeza wewe ndo mbongo wa kwanza kukusikia angalau unataka hathi ya utanganyika wako. Jaribu basi kuwaelimisha ndugu zako kuwa bila ya utaifa basi wewe ni mtumwa tu labda watakusikia maana wenzio wako nyuma kweli kama vile duburi.
 
Si ufe huu muungano una maana gani kwetu watanzania bara? Kama hoja ya visiwa tunacho chetu Mafia jamani basi wasije wakaanza kutulipua mabomu Somalia haikaliki chanzo ni watu wa itikadi kama uamsho.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Watu wengine bana sasa kama anataka kudai Jamhuri ya Watu wa Zanzibar kwanini asirudishe kadi tu ya CCM na kuasisi chama kitakachodai Jamhuri hiyo? Tena kutokana na uzoefu wake angeweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaotaka Zanzibar itokwe kwenye Muungano.

Mwanakijiji;
Mzee kalosti kiana msaidie nauli ya kwenda Dar kurudisha kadi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom