Mwongozo Chadema baada ya uchaguzi mdogo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
images
images
images

Uchaguzi mdogo wa madiwani ulikamilishwa na wapiga kura nchini Jumapili October 28, Chadema kimepata funzo kubwa lenye kutoa tafsiri kadhaa zenye kuleta matumaini kwa wenye moyo mkuu au kufifisha kwa wenye moyo mchache.

Kauli ya Freeman Mbowe yazaa tunda la kwanza
Mwenyekiti wa Chadema miezi michache iliyopita alitoa kauli ya kuwaasa vijana wasomi na wengine kujitokeza na kuchagua maeneo ya kugombea nafasi mbalimbali zikiwemo za uwakilishi ili waandaliwe. Wengi tulipongeza kwa utashi huo, kwa bahati nzuri katika uchaguzi huu mdogo wa Madiwani uliomalizika, kuna kijana mmoja msomi ambaye ameamua si kusubiria nafasi ya kugombea ubunge, bali ameamua kuanzia nafasi ya udiwani naye si mwingine bali ni diwani mchaguliwa wa kata ya Mlangali katika wilaya ya Ludewa ndani ya Mkoa mpya wa Njombe. Tunampongeza kwa kujituma, kutetena azima yake na kushinda. Kwa wengi haikuwa katika picha kwamba Chadema yaweza kupata kiti cha udiwani huko kuliko ngome ya CCM miaka nenda rudi kwa akina hayari Horace Kolimba, ni dalili kwamba mipango ikifanyika kwa umahiri na kumsimamisha mwenye sifa yawezekana, na imewezekana. Ni dhahiri Chadema imeshafunguliwa mlango Ludewa.

Diwani mchaguliwa ametoa mwanga kwa vijana wengi ambao pengine kwa kutokuwa na ujasiri wa kuthubutu wanahofia kitu wasichokuwa na hakika nacho kama watashinda au la, lakini kwa uchaguzi huu tumapata jibu kuwa wananchi wengi wanatuhitaji vijana katika kuleta mabadiliko katika jamii na maendeleo ya taifa letu. Chadema zoezi hilo limefana sana, wana mfano wa kuwafunda vijana wasomi wengi wajitokeze.​

Kutofanya vizuri uchaguzi huu chadema sababu kusimamisha wagombea dhaifu
Maeneo mengi ambayo nguvu kubwa ya Chadema imetumika tumekuja kushuhudia kutoambulia hata kiti kimoja. Unaweza kujengeka utetezi wa aina mbalimbali, lakini kubwa zaidi ni Chama kuwaandaa wagombea wanaofaa ndio tatizo. Chama kisitegemee tu jina la Chadema limpatie mgombea kura, ila auzike na wapiga kura ndipo waridhie. Tatizo kubwa ambalo naona wagombea wengi wa Chadema kula mwanguko wa mende ni kukosa sifa kulinganisha na wagombea wa CCM. Eneo hilo linatakiwa kufanyiwa kazi na Chama.​

Mbinu za Chadema kujitanua zibadilishwe kuendana na upepo unavyovuma.
Yale maandamano na mikutano ya hadhara inaonekana kutokuwa na nafasi kubwa kwa watanzania leo, kwani kama kuwasikia Chadema tumewasikia sana tu na jina la Chadema linalia masikioni mwa wengi kama mwangwi wa mlima Kilimanjaro. Tabia ya kinyonga kujibadilibadili rangi kuakisi mazingira yanayomzunguka ndiyo inayohitajika kwa Chadema sasa hivi.

Pendekezo kwa Chadema ni:


  • [*=1]Kuachana na maandamano kwani yanachelewesha watu kuwajibika katika kujenga uchumi wa nchi
    [*=1]Kupunguza mlolongo wa mikutano kwani inapoteza nguvu na rasilimali za chama wakati chama sera zimeshafahamika.
    [*=1]Kuanza mkakati wa kupeleka wajumbe vijijini na mitaani kwa kusaka wafuasi watakao kuwa wanachama hai nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa hapo uchaguzi ujapo Chadema itakuwa na uhai wa kura kuanza kuhesabu wanachama hai walio nao kama CCM ifanyavyo, la sivyo watabaki kuvimbisha mishipa usoni majwakwani na kuambulia patupu kura zipigwapo.
    [*=1]Zoezi la kuwapata wanachama mijijini liwe endelevu na kuimarisha kuwa na wajumbe wa nyumba kumi wenye kuhakiki wanachama kwa kulinda na kuhamasisha uhai wao chamani.
    [*=1]Chama kuweka msingi vijijini na kuwa na wanachama ni mtaji mkubwa kwani ndiko kwenye wapiga kura wengi na majimbo mengi ya uchaguzi.
    [*=1]Chambo cha mawasiliano kitaifa iwe ni radio au TV ili harakati na sera za chama ziweze kuwafikia wengi badala ya kutumia tu blog kwa njia ya online ambayo mwenye kufikiwa ni Candid Scope badala ya walengwa wapiga kura walio wengi wa vijijini.

Posho za watumishi wa matawini
Kufanya kazi kwa ridhaa kuna madhara yake. Mfano, unaposikia Katibu Mkuu wa Chadema analipwa Tsh. 7,000,000 huku watumishi wa matawini, katani, mikoa na wengineo wakifanya kazi kwa ridhaa huathiri utendaji na ukuaji wa chama. Chama kiwe na mkakati maalumu kuwapa posho walao kidogo kinachowezekana hawa watumishi.

Ruzuku inayopewa isielekezwe kwenye mikutano na maandamano tu, bali watumishi wa mawawini, katani, mkoani na wengineo wafikiriwe ili wafanya kazi kwa moyo wa matumaini zaidi. Pengine ongezeko la wadiwani sasa hivi litapandisha dau la ruzuku, hivyo ongezeko hilo bora lingeelekezwa kuwapa posho watumishi hao kila mwezi kila inapowezekana ili kupunguza manung'uniko ya hapa na pale na hivyo kuathiri utendaji na uwajibikaji wao. Kumbuka CCM inatumia mwanya wa ukata wa vyama vya upinzani kuwarubuni wapiga kura.​

Kuandaa wagombea nafasi mbalimbali wenye sifa
Jitihada kubwa zinatakiwa kuwekwa katika kuandaa nguvu ya kutosha katika kuwaandaa wagombea katika chaguzi mbalimbali zijazo kwa kipindi kirefu kutosha. Isitumike ila ya zima moto. Kama alifanikiwa Nasari wa Arumeru mashariki kwa mtindo wa zima moto tusitazamie mtindo huo huo utatumika kufanikisha chaguzi nyingine, kwani wagombea wanatakiwa umma uwafahamu kwa kipindi cha kutosha na hivyo wanatakiwa kuwa karibu na maeneo yao wanakotegemea kugombea mara kwa mara.​

Kuunganisha nguvu za upinzani
Mwenyekiti wa Chadema ambaye ni mbunge na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, mara baada ya uchaguzi mkuu uliopita alisema kuungana kambi ya upinzani wapate muda kwanza kwa sababu ya majeraha ya uchaguzi. Hilo lilieleweka. Sasa majeraha ni karibu yamepona labda kama yapo ambayo yamegeuka kuwa donda ndugu.

Viongozi wa Chadema kitaifa wanatakiwa wataremke kutoka pale walipo ili wawafikie wenzao na kupika na kula meza moja chakula kinakuwa kitamu zaidi. Unyenyekevu ni siri moja kubwa katika kujiwekea malengo ya mafanikio. Ushupavu umewaweka wengi katika hali ya kubakizwa isolated. Ukiwa na mtoto jifanye kama watoto wafanyavyo, kwa wachezaji utajifanya mwanamichezo, wasomi utaongea mambo ya kisomi nk. Ndilo linalotakiwa Chadema wawaone wenzao vyama vya upinzani ni hazina katika kubuni, kupanga na kufanikisha mikakati ya kuikomboa nchi. Kura nyingi katika uchaguzi mdogo uliomalizika utakuta kama wangeunganisha nguvu CCM ingetelekeza viti vingi zaidi, sasa bora lipi? Kuthoofisha nguvu za CCM kwa kunyang'anya himaya yao kuwa chini ya umoja wa upinzani au kubaki na unyonge wa mwenye kiti kimoja abaki kivyake na wenye viti vingi wajisikie kujitutumua huku kuchukua dola ikibaki ndoto za kufikirika?​

Viongozi kitaifa watambue kasoro zisemazo wajitahidi kujirekebisha
Viongozi wa kitaifa Chadema yanayolalamikiwa na baadhi ambao wamewahi kufanya kazi nao na kisha kuamua kujitoa hayawezi kubezwa, kwani lisemwalo lipo kama halipo laja, na tujue hawa ni binadamu kama tulivyo wengi tulivyo na kasoro nyingi tu za kimaumbili, kimaadili, kifikra, kujikuza, kujiona baora, na kiutambuzi. Siyo kubeza tu, wanatakiwa kujitathmini, maana kuendekeza sana tabia binafsi na nafsi ya mtu katika uongozi ni hatarishi katika nyanja za siasa. Yalisemwa, yanasemwa, lakini kuyaacha yapite tu kama tunataka mageuzi ya kweli hatutakuwa wa kweli na kuwatakia mema.
Hulka ya kiaongozi katika jamii:​


  • [*=1]ushirikiano na ushirikishi,
    [*=1]unyenyekevu na ukakamavu,
    [*=1]uvumilivu na ustahimilivu,
    [*=1]hekima na busara
ni mambo ambayo yanamjengea heshima na mafakio katika utumishi. Maamuzi ya papo kwa papo ni hatari, majuto ni mjukuu kwani maji yakishamwagika hayazoleki.

Viongozi wanatakiwa kuondokana na kulewa sifa, kulewa umati wa wahudhuriaji mikutano. Wanaohudhuria mikutano ya Chadema walio wengi ni mashabiki ambao si wapiga kura tofauti na mikutano ya CCM ambayo wahudhuriaji ni wapiga kura. Mkutano wa CCM wahudhuriaji 75% ni wapiga kura wake wakati wahudhuria wa Chadema kiwango hicho hicho wahudhuria ni mashabiki tu kama inapotokea tukio fulani watu wanafurika isivyotegemewa ndivyo Chadema wanavyotakiwa kusoma mwelekeo huu unavyowalaza chali katika chaguzi. CCM inapobeba watu kwa malori ni wanachama wake si mashabiki wakati mikutano ya Chadema wanaofurika ni mashabiki wasio wapiga kura. Hii ndiyo hali halisi ya tathmini yangu.​

Diwani wa Mlangali, Ludewa ni changamoto na hasa kwa vijana wasomi
Vijana wasomi na wahitimu wengi vyuo vikuu tumekuwa na kasumba ya kuhangaika huku na kule huku tukilazimika kumaliza kandambili zetu kwa ajili ya kutembeza RESUME wakati tuna nafasi tele kama za huyu msomi mwenzetu kuelekeza nguvu huko matawini, vijijini, katani na wilayani kujenga msingi wa maisha. Ametufunza mengi, ametufunza mengi, wenye upeo wa masafa marefu wamempata, wenzangu mimi wenye kufikiria leo na kesho tu tutabaki kuchakaza kandambili kutembeza resume huku na kule.​

 
Hilo la kuwalipa posho watendaji wa chini nakubaliana nalo kabisa...

Napendekeza kuwa sie wengine ambao tumebaki kutoa hamasa kwa michango ya aina mbali mabali hasa hasa kwenye mitandao ya kijamii tujitolee walau pesa kidogo kuchangia eneo hili ili kuziba nakisi inayoweza kujitokeza kwa sababu ya ruzuku ndogo ambao chama kinapata.

Naamini Chadema wakijitahidi (ikianzia na kuandaa mipango na kuiwekea bajeti) kutekeleza suala la kujenga chama kule kwenye mashina na matawi kwa kuingiza wanachama wapya na kuwasajili, itasaidia kufanyamaandalizi mazuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa serikali kuu. Muda uliobaki ni mdogo sana na kazi hii inatakiwa ianze mara moja...
 
Mimi nashindwa kushauri kitu kwa sababu naona kama vile uongozi haushauriki au hawapiti mitaa hii siku hizi kukusanya maoni ya wadau.
 
Hilo la kuwalipa posho watendaji wa chini nakubaliana nalo kabisa...

Napendekeza kuwa sie wengine ambao tumebaki kutoa hamasa kwa michango ya aina mbali mabali hasa hasa kwenye mitandao ya kijamii tujitolee walau pesa kidogo kuchangia eneo hili ili kuziba nakisi inayoweza kujitokeza kwa sababu ya ruzuku ndogo ambao chama kinapata.

Naamini Chadema wakijitahidi (ikianzia na kuandaa mipango na kuiwekea bajeti) kutekeleza suala la kujenga chama kule kwenye mashina na matawi kwa kuingiza wanachama wapya na kuwasajili, itasaidia kufanyamaandalizi mazuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa serikali kuu. Muda uliobaki ni mdogo sana na kazi hii inatakiwa ianze mara moja...

Kuandaa nguvu ya mikutano na maandamano tu si suluhisho na hapa nakubalina nawe hata sisi tuwe tayari kuchangia uimarishaji wa matawi vijijini na hata chama chenyewe kiwe na bajeti hiyo kwani ni eneo ambalo lina umuhimu wa kwanza kwa sasa.
 
Mimi nashindwa kushauri kitu kwa sababu naona kama vile uongozi haushauriki au hawapiti mitaa hii siku hizi kukusanya maoni ya wadau.

Tusikate tamaa Matola kwa nchi ni yetu, ipo siku na siku imefika nategemea mioyo yao italegea tu kwani ishara za nyakati ni funzo tosha.
 
Tusikate tamaa Matola kwa nchi ni yetu, ipo siku na siku imefika nategemea mioyo yao italegea tu kwani ishara za nyakati ni funzo tosha.
Hapa nitarudi asubuhi, tumeshauri mengi sana sasa kama hawayasomi mimi nitashangaa sana, muulize kila mtu anaijuwa BAVICHA lakini ni nani anaijuwa BAWACHA? hivi watu wanashindwa kujuwa chama kinahitaji sana wanawake majasiri wa kwenda kuwaamsha usingizini Wanawake wenzao?

Maana Wasichana wasomi na wasio wasomi wote wako BAVICHA huku BAWACHA inaonekana ni maujanja dot com tu. ifumuliwe yote we need New reform for BAWACHA.
 
Hapa nitarudi asubuhi, tumeshauri mengi sana sasa kama hawayasomi mimi nitashangaa sana, muulize kila mtu anaijuwa BAVICHA lakini ni nani anaijuwa BAWACHA? hivi watu wanashindwa kujuwa chama kinahitaji sana wanawake majasiri wa kwenda kuwaamsha usingizini Wanawake wenzao?

Maana Wasichana wasomi na wasio wasomi wote wako BAVICHA huku BAWACHA inaonekana ni maujanja dot com tu. ifumuliwe yote we need New reform for BAWACHA.

Nakuunga mkono sana hili, kwani idadi kubwa ya watanzania ni wanawake, huku ukiweka ndoana kura nyingi zitopatikana, lakini sisikii kitu kuhusu umoja wa wanawake wa Chadema, wapo kwa jina tu au kisiasa tu?

Huenda tatizo ni ukata kwa kutowekewa bajeti, la sivyo wanasubiria tu ubunge wa viti maalumu ndipo tukatakapoanza kuwasikia.
 
Lazima ushauri huu umewafurahisha sana SiSieM. Eti waache kufanya mikutano! Maendeleo gani wananchi wanayapata wasipohudhuria mikutano? Eti CDM iunganishe nguvu na vyama vingine ambavyo karibu vyote viko affiliated na SiSieM! this is another joke. Hivi ni kweli wanaCDM wameisha sahau migogoro iliyojitokeza pale ilipoamua kushirikiana na vyama vingine?. Huu ni mkakati wa SiSieM kuhakikisha migogoro isiyo kwisha kwenye vyama, migogoro ya kugombea madaraka na kutoa matamko ya kumalizana. Mi nafikiri tuache kujiita wanaCDM tunapotoa mitazamo yetu.
 
Lazima ushauri huu umewafurahisha sana SiSieM. Eti waache kufanya mikutano! Maendeleo gani wananchi wanayapata wasipohudhuria mikutano? Eti CDM iunganishe nguvu na vyama vingine ambavyo karibu vyote viko affiliated na SiSieM! this is another joke. Hivi ni kweli wanaCDM wameisha sahau migogoro iliyojitokeza pale ilipoamua kushirikiana na vyama vingine?. Huu ni mkakati wa SiSieM kuhakikisha migogoro isiyo kwisha kwenye vyama, migogoro ya kugombea madaraka na kutoa matamko ya kumalizana. Mi nafikiri tuache kujiita wanaCDM tunapotoa mitazamo yetu.

Akili ni nywele na kila mmoja ana zake. Lakini pia naheshimu sana mchango wako. Haya ni maoni yangu binafsi nikichukulia mifano ya waliofanikiwa kwa kutumia njia hiyo kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Katu kidole kimoja hakivunji chawa.

Uhuru wa visiwa vya Zanzibar na Pemba vilivyafanikiwa baada ya vyama vya wazawa kuwa na umoja, na hivyo mapinduzi yalipangwa kwa pamoja, la sivyo mambo yasingewaendea kama ilivyokuwa.

Mwai Kibaki wa Kenya alifanikiwa kumng'a kisiki Daniel Arap Moi baada ya kutaabika mara kadhaa bila mafanikio, mwishoni aliamua kuteremka awakute wenzake kwenye kambi ya upinzani, alipounganisha nguvu ndipo dhoruba kali ya umoja wao ilimshinda nguvu Daniel Arap Moi.

Zambia tumeshuhudia mageuzi ya kisiasa yametokana na kuunganisha nguvu hizo pia.

Tanzania kabla ya uhuru kulikuwa na vyama vingi ambayo vingi vikiwa ni social clubs, lakini Nyerere akianzia na kile cha TAA alifanikiwa kuunganisha hata club za akina Kawawa huko makazini na kuwa na nguvu ya pamoja katika kudai uhuru na hivyo kuwa chimbuko la TANU.

Kama hali itaendeleea hivi hivi kwa kuwaweka kando wapinzani hapo CCM itakuwa imefanikiwa copy and paste ya mfumo wa mkoloni mwangereza ya divide and rule.
 
Mkuu Candid Scope ushauri wako wote nimekubalina nao isipokuwa huu wa kuunganisha nguvu na vyama vingine. Unataka tupore mke wa mtu (CUF) ni hatari sana kwa uhai wa chama au uungane na TLP ya sultani Mrema? Au UDP ya sultan Cheyo? Mkuu Hakuna vyama vya kuunganisha nguvu na CDM
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Candid Scope ushauri wako wote nimekubalina nao isipokuwa huu wa kuunganisha nguvu na vyama vingine. Unataka tupore mke wa mtu (CUF) ni hatari sana kwa uhai wa chama au uungane na TLP ya sultani Mrema? Au UDP ya sultan Cheyo? Mkuu Hakuna vyama vya kuunganisha nguvu na CDM

Dhana ya wasiwasi inaweza kujengeka hivyo, lakini tujue kwamba mtazamo wa wa visiwani na wa bara kunaweza kuwa tofauti pamoja na kuwa ni chama kimoja cha kisiasa, ndio maana tunaona mpasuko wa CCM visiwani kuhusu mstakabali wa katiba ya Jamhuri ya Muungano inayoendelea.

Kuna dalili nyingi ambazo vyama kadhaa vinaonekana kuonyesha nia, hata cha NCCR Mageuzi jinsi walivyomaliza mezani mashtaka yaliyofunguliwa kupinga ubunge wa Halima Mdee. Hiyo ni ishara tosha kwamba nia ikiwepo uwezekano upo. Kwa vyo vyote tahadhari hapana budi kuwepo na pia makubaliano endapo watashika dola ni jambo la msingi, cha maana kuunganisha nguvu kuiondoa CCM la sivyo kazi kweli kweli.
 
hii ni busara haswaaaaaaa lakini yahitaji jicho la tatu kuitambua kama ni busara ebu viongoz wa chadema tunaowaamini kuwa ndiyo wajenzi makini wataifa hili chukueni busara hii
 
Wadau,

Vichwa vya habari vya baadhi magazeti ya leo vimewanukuu baadhi ya viongozi wa ccm wakikibeza cdm eti kwa ushindi finyu wa uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika hivi karibuni nchini. Nimesoma pia humu jamvini maoni ya watu ambao inawezekana ama ni wanachama wa cdm au viongozi wa cdm wakitoa maelezo yanayodhihirisha kukatishwa kwao tamaa na matokeo hayo. Kwanza nianze kwa keeleza jambo moja ambalo ni bayana kwamba kuking'oa chama tawala siyo kazi ya lelemama na muda mfupi kama wengi wetu tunavyodhani. Ni kazi nzito na inahitaji nguvu kubwa na yenye mabonde na milima mingi. Kwa hiyo, inahitaji uvumilivu mkubwa sana. Binafsi, nakishukuru sana cdm kwa kutuonyesha watanzania kuwa ni chama kilicho na dhamira ya dhati ya kumwondoa mkoloni wa pili ambaye ni ccm. Vyama vingine viliibuka kwa nguvu hiihii na sasa vinaelekea kaburini au tayari vipo kaburini.

Waswahili wanasema siku njema huonekana asubuhi. Matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika nchini hadi sasa yanaashiria cdm ina-gain na ccm ina-lose. Ukichora graph ya ushindi wa ccm tangu mwaka 2005 bila shaka utabaini hiki ninachoandika hapa. Wakati upande huo wa ccm ukiwa hivyo, upande wa cdm unaendelea kuongeza ushindi yaani graph inapanda. Huo ndiyo ukweli na utaendelea kubaki kuwa ukweli.

Kwa wana ccm makini na wasomi kamwe hawawezi kufurahia matokeo ya kupoteza kata 4 na kuziacha ziende kwa wapinzani wao cdm. Hali kadhalika, kwa wana cdm makini na wasomi hawawezi kusikitika kupata ushindi kwenye kata chache ikilinganishwa na ccm wakati katika kata walizopata, 4 ni mpya.

Ndugu zangu wana cdm na wapenda mabadiliko, tafadhali msikate tamaa kabisa. Ushindi upo na endeleeni kuongeza bidii. Sumu iliyowekwa na ccm kwenye vichwa vya watanzania ni kali. Inahitaji utaalam na commitment ya hali ya juu kuiondoa na kuwakomboa watanzania.
 
Mkuu umesema vema though umeweka na vipropaganda kidogo....anyway ndo kujifunza na ndo mageuzi,,,,ni ukweli usiopingika kuwa vijana ndo chachu ya maendeleo na wanakubalika sana,,,mimi nina uhakika CHADEMA ikisimamisha vijana wengi 2015 mambo yataenda sawa,,,

Ni rahisi kumnadi kijana asiyekubalika kuliko Mzee asiyekubalika
 
Daftari la wapiga kura ni moja kati ya sababu kuu! fikiri vizuri, Mangine umeongea sawa ila kunasehem umepotoka kiasi.
 
Mengi yana ukweli ni kiasi cha kuyapa muda na kukaa chini kuyafanyia kazi. Sisi kama washika dau tutaendelea kutoa mchango wetu kwa minajiri ya kukisongesha mbele zaidi.
 
Back
Top Bottom