‘Mwombeeni JK aepuke mapepo yanayomfuata Ikulu’ - Siamini kama kauli hii anaitoa waziri nchini!

Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,136
na Nasra Abdallah

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.

Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?

Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.

Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.

Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.

Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.

Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.

Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.

"Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.

Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.

Chanzo: Tanzania Daima

Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????

na Nasra Abdallah

amka2.gif
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.
Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?
Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.
Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.
Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.
Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.
Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.
Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.
“Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.
Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.

Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????

Hata mimi siamini kwa sababu zifuatazo:
1:"MAJINI" ni neno tata na ina Maana "Subjective";
Kama vile:
a."VIUMBE WA AJABU WASIO ELEWEKA(Oxford Dictionary)
b."VIUMBE WABAYA SANA,MAPEPO AMBAYO YAKIKEMEWA KWA JINA LA YESU HUTOWEKA:(WAKRISTO.)
Kwa WAISLAMU maana ni
"VIUMBE HAI VYA AJABU VILIVYO GAWANYIKA Sehemu MBILI,Wema na wabaya"
-MY TAKE:
:SI VYEMA kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kuambiwa neno "JINI" na KUTOA MAANA bila kufikiri kwa makini.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Lukuvi ni mtu tunayemtegemea kujenga uchumi imara! nadhani kauli hii angeitolea katika nhi ya Irseal, basi kesho yake angeamka na kashfa ya kulopoka matusi gazetini.
 
Hivi LUKUVI si ndio yule ambae MSEMAKWELI alisema hana elimu rasmi ya shule (kama ZUMA) ila ana vyeti vya diploma vya kugushi?, mambo ya uchumi kayajulia wapi?, msamehe bure!
 
..lakini nchi hii imekuwa ikiombewa kwa muda mrefu sasa, na hali inazidi kuwa mbaya.

..ila kama huyo naye ni Waziri ktk serikali ya JK then it is not suprising kwamba nchi imekwama kiasi hiki.
 
sishangai kwani lukuvi alitetea sana KIKOMBE CHA BABU WA LOLIONDO.
Ni waziri anayeabudu ulozi ulozi sana.
 
Kama ni hivyo tusubiri kumwona kwa Ka-tortoise au kwa T.B. Joshua! Yaelekea ya Sheikh mambo magumu!
 
Muangalie kwa makini sana lukuvi anapoitetea serikali, pepo kamili!!!!
 
serikali muflisi utaiona tu.yaani hawa jamaa wamechoka kwelikweli
 
Muangalie kwa makini sana lukuvi anapoitetea serikali, pepo kamili!!!!
Hata huo utetezi anaoutoa unaashiria ubabaishaji tu. Anasema kupigika kwa tanzania kunatokana na economic turndown, kwani mataifa tajiri ambao ni soko hawana hela. Sasa Tanzania tunauza nini cha maana huko nje hadi nasisi tujifanye tumeathirika na economic turbulence??Kupigika kwetu ni vyema tukakutenganisha na muanguko w kiuchumi labda kama angesema wale tunaowaomba misaada sasa hivi hawana hela za kutupa hapo ningemwelewa. Tanzania inapaswa kuongeza production waache kudanganya wananchi.
 
Kama hii kweli ni kauli ya Waziri wa nchi na kama kweli ndiyo imani waliyo nayo huko Ikulu, ninamsikitikia Raisi mpya atakayechukua madaraka 2015. Haitakuwa tofauti na kungia kwenye mapango ya wachawi basi! Loh!
 
JK hawezi kuchanganya waganga wa kienyeji na Mungu. Ili aweze kuombewa na kupona inabidi aachane na mambo ya kina wanajimu na tunguli zao
 
Back
Top Bottom