na Nasra Abdallah
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.
Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?
Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.
Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.
Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.
Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.
Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.
Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.
"Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.
Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.
Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.
Chanzo: Tanzania Daima
Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????