‘Mwombeeni JK aepuke mapepo yanayomfuata Ikulu’ - Siamini kama kauli hii anaitoa waziri nchini!

Kwani nani asiejua kuwa ikulu kuna mapepo? Pepo mkuu ni JK na huyo Lukuvi ni pepo!

Yani ikulu takatifu leo iwe na mapepo kweli? Imedumu miaka 50 pale ilipo, lakini leo mtu anatuambia kuwa rais wetu anatumiwa majini ikulu kweli inaingia akilini??

Ama kweli afae hutaja kila jina na mizimu na kuvirudia!
Hivi ccm si wana mbunge Kigagula ndugu Majimarefu, ameshindwa kuyatoa wakati Lusinde alisema huwachanja chale makalioni waheshimiwa?

Haya Dr Mnyaunyau kayatoe majini pale magogni
 
Hii inaonyesha ujinga uliokithiri wa viongozi wetu.Nilitegemea kiongozi kama Lukuvi awe na ufahamu wa hali ya juu kiasi cha kuweza kufafanua mambo yafuatayo:*Kanisa la ufufuo na uzima sio kanisa la kiroho kwa hiyo halina mamlaka juu ya mapepo.Kwa maana nyingine,sana sana litaongeza matatizo yaliyoko Ikulu*Shetani ukimpinga anakimbia.Hii ina maana kwamba matatizo ya mapepo ikulu ni ya kujitakia,na uwezekano mkubwa ni kwamba mapepo hayo yamekaribishwa kwa kazi maalum.*Kuwepo kwa gesi Mtwara si lazima kutusaidie Watanzanie.Na kwa kweli ushaidi wa mazingira upo kila mahali kwamba gesi hiyo haitatusaidie.Mbona alimasi,dhahabu,tanzanite,mbuga za wanyama nk.havijatusaidia?Anayo-ongea bwana huyu ni pumba tupu.
na Nasra Abdallah

amka2.gif
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.
Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?
Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.
Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.
Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.
Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.
Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.
Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.
“Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.
Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.

Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????
 
Hii ndo aina ya viongozi wa nchi hii, tusishangae sana maana bado kina Wassira, Komba, Mwigulu, Makala na hata Magufuli hawajatoa matamko yao! Yaani mawaziri wa baraza hili sijui hata kama wanachanganya na za kwao kabla hawalopoka, ukienda kwa kina Nundu ndo kabisaaaaaa! Bora 2015 ifike haraka
 
na Nasra Abdallah

amka2.gif
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.
Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?
Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.
Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.
Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.
Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.
Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.
Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.
“Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.
Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.

Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????
basi apumzike waje ambao mapepo hayawasumbue wafanye kazi kwa bidii ajiuzulu tu,kwani kapigiwa misumari hapo ikulu
 
anazungumzia yale mapepo yaliyofika ikulu baada ya mchakato wa kupata katiba mpya kupingwa na baadhi ya waheshmiwa bungeni.
 
Tangu enzi za Mwalimu wanasiasa wa bongo wanapokuwa hawana majibu ya kwa nini uchumi wa nchi ni mbaya wanajitetea kuwa Hali iko hivyo dunia nzima! HUU NI UONGO MKUBWA-WANASHINDWA kutuambia ukweli wananchi kuwa HAWAKO MADARAKANI KUWATUMIKIA WANANCHI bali WANANCHI KUWATUMIKIA VIONGOZI.

Ingekuwa hivyo MBONA NCHI ZINGINE TULIZOKUWA TUNAZIZIDI ama KULINGANA NAZO KIUCHUMI SASA ZIMETUACHA MBALI? Zenyewe ziko dunia gani-LUKUVI na MAGAMBA wenzake hawana mbinu ya kutukwamua kiuchumi!
 
Hakuna haja ya kumuombea hayo mapepo kama yanaweza hata kumtafuna yamtafune maana yeye na washirika wake wameshaitafuna nchi vya kutosha,watanzania leo wanaombea hata ingekuwa kesho siku yake ya kuondoka magogoni! Full usanii,
 
JK hawezi kuchanganya waganga wa kienyeji na Mungu. Ili aweze kuombewa na kupona inabidi aachane na mambo ya kina wanajimu na tunguli zao

Mhe RAIS ANATAKIWA KUBADILI DINI. THEN AMPOKEE YESU LA SIVYO HALI NI MBAYA; I FEEL SORRY FOR HIM. BY THE WAY JESUS SAVES
 
Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.
 
magamba ya CCM yenyewe ni pepo tosha so yaombewe yenyewe kwanza kwani ni papepo mengi yanayoligarimu taifa
 
kwa sisi wazee hiyo ni message sent kwa mkulu kuwa anaendekeza kukaribisha watu wachafu hapo magogoni na aache.
 
Amejuaje kuwa ana mapepo! basi amwambie aokoke! kiti cha majini hakisaidii tena......stupid!!!
 
na Nasra Abdallah

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amemuomba mchungaji kiongozi wa Kanisa la Saa za Ufufuo wa Uzima, Josephat Gwajima, kumuombea Rais Jakaya Kikwete, kumuepusha mbali na mapepo ambayo yamekuwa yakifika Ikulu kumjaribu.

Lukuvi alitoa ombi hilo jana wakati wa misa ya kuliombea taifa amani, iliyofanyika katika viwanja vya kanisa hilo, Kawe, jijini Dar es Salaam.

Alimweleza mchungaji huyo kuwa kama anahubiria watu takriban 100,000 na kati yao wengi wanaanguka kwa mapepo pindi anapowaombea, itakuwaje Rais Kikwete ambaye anaongoza watu zaidi ya milioni 40?

Lukuvi alisema ni wazi kwamba kuna mapepo mengi yamekuwa yakitumwa kwake ili kukwamisha malengo mazuri aliyonayo kwa Watanzania.

Akizungumzia kuhusu hali ya uchumi iliyopo sasa, Lukuvi aliwataka wananchi wasitupe lawama kwa uongozi kuwa ndiyo umewafikisha hapo kwa vile kuyumba kwa uchumi ni tatizo la dunia nzima kwa sasa.

Alisema hata nchi zilizoendelea ambazo zinategemewa kununua bidhaa za mataifa maskini kama Tanzania, nazo uchumi wao umetikiswa.

Kwa mujibu wa waziri huyo kumekuwepo na mipango mizuri ya kuboresha uchumi inayofanywa kwa sasa na kuahidi kwamba huko mbeleni mambo yatakuwa mazuri kuliko ilivyokuwa siku za nyuma.

Katika hili pia aliwataka wananachi kujenga tabia ya kujitegemea badala ya kubaki kuwa walalamishi na kulia hali ngumu ya maisha.

Akigusia suala la umeme, Waziri Lukuvi alisema tatizo lililopo sasa limetokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo zile mvua zilizokuwa zikitegemewa katika misimu yake kushindwa kunyesha.

“Lakini tunamshukuru Mungu, wakati akitunyima mvua, katunyooshea neema nyingine ya gesi ambayo imevumbuliwa pale Mtwara na mpaka ninavyoongea tayari mabomba yanatandazawa kutoka Mtwata hadi Dar es Salaam.

Naye Mchungaji Gwajima, alisema katika kanisa lake atahakikisha hakuna kiongozi yeyote fisadi wala mla rushwa anakanyaga, akidai kuwa wamekuwa ni watu wanaokula nchi bila ya huruma.

Gwajima alisema kazi yake moja iliyopo sasa ni kuliombea taifa amani na kumuomba Mungu awaumbue wala rushwa na mafisadi wote.

Chanzo: Tanzania Daima

Mtazamo: Kama waziri wa serikali anawaza kuhusu mapepo je mwananchi wa kawaida naye awaze nini? Nauliza tu????

Hivi Serikali inaamini uchawi kweli?,Kama habari ilivyo ndio hivyo sidhani Kama tutafika kwa aina hii ya viongozi kuamini uchawi/mapepo/ndio vinaikwamisha Serikali hii kusonga mbele,mapepo mapepo mapepo badala ya kuwajibika mnayasingizia mapepo!!!shame on u
 
Back
Top Bottom