Mwl. Nyerere alisema kama mnampenda Kikwete kanyweni naye chai - Sasa tunayaona!!

Sikia bibie halaf usiniite kijana, nina umri sawa na Babu yako, ukweli lazma usemwe serikali ya ccm inakandamiza sana maisha ya mwananchi wa kawaida na sio kutuleteeni data zenu za kuhadaa raia. Naamini wewe ulipo unalia kivulini hebu jaribu uishi uswazi japo kwa mda mfupi ndo utaelewa ni vipi wananchi wanataabika.

Sikiliza Mzee, data zipi zaidi uzitakazo ambazo unaona hazikuhadai? Pata hii:

Tanzania kwa miaka yote 44 kabla ya Kikwete, Mtanzania hajawahi kuishi chini ya dola moja kwa siku, leo wakati wa kikwete tumelipita hilo kwa zaidi ya asilimia 100 kwa miaka 9 tu. Jiulize, wa kabla yake walikuwepo kwa miaka mingapi wakashindwa hilo ewe mzee?
 
lowasa%20na%20kikwete1995.jpg

BAADA ya kutuma mtandaoni uchambuzi mfupi wa nafasi ya Mwalimu Julius Nyerere katika kututafutia "mgombea safi" (Mr. Clean) mwaka 1995 nimejulishwa kwamba kuna utata, tatizo au walakini katika uchambuzi huo. Inasemekana siyo kweli kwamba Nyerere alihusika na kuhakikisha kwamba Benjamin Mkapa anamshinda Jakaya Kikwete. Kwa kuwa mimi ni muumini wa kuweka historia sawa, ningependa tujadili suala hili kwa kutumia vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha hatupotoshi historia au ukweli hasa mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu.

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 1995 nilikuwa nasoma Shule ya Sekondari ya Azania. Nyumbani nilikuwa nasaidia kukata vipande vya magazeti kwa ajili ya uchambuzi wa kisiasa. Kipindi hicho nilikuwa navutiwa sana na harakati za kisiasa za Kikwete na nilifuatilia sana msisimko uliotokea wakati yeye na Edward Lowassa walipopanda ndege ndogo ya kukodi na kwenda Dodoma kuchukua fomu za kugombea dakika za lala salama, lakini kwa sasa nimepata picha tofauti.

Hali kadhalika nilikuwa nafuatilia kwa karibu sana hotuba za Nyerere na vile vitabu vyake alivyovitoa kabla ya uchaguzi huo ambavyo, kwa uelewa wangu, kimsingi vilitumika pia, kwa namna moja au nyingine, kuhakikisha kuwa mwaka 1995 John Malecela hapati urais (hasa) baada ya lile sakata la OIC na G55.

Kwenye mjadala wa wanazuoni, mwaka 2009 kuhusu niliwahi kuandika maneno yafuatayo: "When Nyerere was asked that question, I am told, he responded by saying that he was unlucky, implying that two people in particulary that he groomed died prematurely: (Hussein Ramadhani) Shekilango (from whom we get the name of that road in Dar) and Edward Moringe Sokoine, another person that he groomed but, due to malicious campaigns, never became our President (The President who never was as Zitto Kabwe calls him) is Dr. Salim Ahmed Salim.

Now we are struggling with the legacy of a president Nyerere 'chose' for us in 1995 but if we look at what was in his mind as his 1995 book Our Leadership and the Destiny of Tanzania reveals, we will realize that his was a genuine attempt to make sure that the other folks that he groomed to be good leaders - and turned bad according to his standards - do not take over. Now should we blame him for who we become?"

Hayo maneno nimeyakumbuka kwa sababu wanaoona kuna walakini kwenye madai au hoja kuwa Nyerere alikuwa na 'mkono' katika kumzuia Kikwete kuwa Rais mwaka 1995, wanasisitiza - na nakubaliana nao kabisa - kuwa mgombea wa Nyerere alikuwa ni Dk. Salim. Lakini tatizo ni kwamba kwenye kile kinyang'anyiro cha 1995 hakuweza kuingia ulingoni kutokana na sababu ambazo nadhani sote tunazielewa. Hivyo, pia ni rahisi kuelewa madai au hoja nzito inayosema kwamba Nyerere alimpigia debe Kikwete aingie kwenye 'tano au tatu' bora ya wagombea wa urais kupitia CCM ili wagombea wote wasiwe wa dini moja, hasa ukizingatia kwamba 'nyufa za udini' zilikwishajitokeza katika medani ya siasa au kampeni na ilibidi azikemee mara kwa mara.

Lakini tukumbuke kabla ya kinyang'anyiro cha awali tunaambiwa Kikwete alienda kuonana na Nyerere nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam. Inasemekana aliitwa (aende) mwenyewe ila akaenda na Lowassa. Na kuna tafsiri kinzani kuhusu taarifa mbalimbali za wakati huo, zinazosema kwamba Nyerere aliona kuna tatizo na Lowassa japo pia tunaambiwa alibariki uamuzi huo wa Kikwete wa kwenda kugombea.

Baada ya hilo la Kikwete kuendelea kuwa pamoja na Lowassa kweli tunaweza kusema bado Nyerere alikuwa hajachagua 'amuunge' nani mkono kati ya Mkapa na Kikwete kwenye raundi za mwisho za kinyang'anyiro cha kuchaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama tawala pale Dodoma?

Kweli Nyerere alikuwa anaona ni sawa yeyote kati ya Mkapa na Kikwete akishinda hivyo hakutumia mbinu yoyote kuzuia Kikwete asishinde maana (eti) alikuja tu kugundua kuwa yeye na Kamati Kuu ya CCM 'wamepigwa changa la macho' mwishoni kabisa kabla tu ya kupiga kura ilipoonekana Kikwete amedhamiria kumteua Lowassa awe Waziri Mkuu iwapo atashinda nafasi hiyo?

Sasa kuna hoja nyingine ya msingi kabisa, kwamba kambi ya Kikwete ilikuwa haijasoma au haijaelewa vizuri katiba au kanuni za CCM kuhusu 'kutosha kwa kura' ila (eti) kambi ya Mkapa ndiyo ilikuwa inalijua suala hilo fika, hivyo, basi ikautumia mwanya huo kuhakikisha kwamba pamoja na Kikwete kupata kura nyingi zaidi kuliko Mkapa, kikanuni, kura zipigwe tena na hivyo kwenye raundi ya mwisho ya kinyang'anyiro Mkapa akamshinda Kikwete, baada ya wengi wa wale waliopigia kura wale wagombea wengine walioenguliwa mwanzoni au katikati kumpigia Mkapa.

Ni hoja ya msingi maana inawasaidia kutuonesha au kuthibitisha kwamba siyo Nyerere aliyemzibia Kikwete bali lilikuwa ni suala tu la kikanuni (na kampeni za kambi) lililosababisha kura zipigwe tena na zile zingine zihamie kwa Mkapa hivyo kumzidi mwenzake.
Lakini swali la kujiuliza: Ni kina nani hao waliokuwa kwenye hiyo kambi (ya kampeni) ya Mkapa maana kwa uelewa wangu walikuwa ni 'Wanyerere' ('Nyerereists') wakuu? Kama ni hivyo, wako upande gani leo hii hasa wanapoona Nyerere wao anatumiwa 'ndivyo sivyo' katika kampeni za uchaguzi wa wagombea urais?

Wajitokeze sasa basi kutusaidia kuiweka historia sawa hasa ukizingatia mwaka huu wa 2015 una mengi sana yanayofanana na yale yale mwaka 1995.

Chanzo:raiamwema
 
Wanajukwaa nawasalimu!

Kumekuwa na minong'ono ya mara kwa mara kuwa Hayati Baba wa Taifa alipata kusema kuwa Mh. Prof. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hawezi kuwa rais kwa sababu bado hajakomaa (inasemwa hivyo);

Lakini kilichotokea baadaye ni kuwa wanatanzania walimpa Kikwete urais wa JMT kwa kura zaidi ya asilimia 80 hapo ilikuwa mwaka 2005 na hadi leo bado ni rais wao!

Je, huenda Baba wa Taifa analishwa maneno? Najiuliza ni lini rais Kikwete amekomaa hadi kuwa rais wa JMT, na ni kwa nini wananchi walimkubali kwa zaidi ya asilimia 80?

Ni hayo tu!
 
Wanajukwaa nawasalimu!

Kumekuwa na minong'ono ya mara kwa mara kuwa Hayati Baba wa Taifa alipata kusema kuwa Mh. Prof. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete hawezi kuwa rais kwa sababu bado hajakomaa (inasemwa hivyo);

Lakini kilichotokea baadaye ni kuwa wanatanzania walimpa Kikwete urais wa JMT kwa kura zaidi ya asilimia 80 hapo ilikuwa mwaka 2005 na hadi leo bado ni rais wao!

Je, huenda Baba wa Taifa analishwa maneno? Najiuliza ni lini rais Kikwete amekomaa hadi kuwa rais wa JMT, na ni kwa nini wananchi walimkubali kwa zaidi ya asilimia 80?

Ni hayo tu!

ndugu that is puzzle which need to be answered,hapa watakupa very funny replies subiri uone
 
team lowassa = team rejected
nyerere aliona mbali sana alipomkataa lowassa kugombea 1995
hatudanganyiki
 
Hahahahaaa kura za Wizi zile......Kama huamini nipe matokeo ya uchaguzi Mkuu kwa Mkoa wa Dar es Salaam........................
 
mnajisumbua tu na hilo fisadi lenu watanzania tutakuwa wa ajabu sana kama tutakuwa na kiongozi aina ya lowasa tutakuwaje na Rais asiyeweza kupinga ufisadi hiyo ni aibu gani jamani.
 
Back
Top Bottom