Mwl amoni mtera is no more

mwanamilembe

Member
Apr 13, 2010
23
5
Kwa wale mliosoma Pugu Sekondari kati ya mwaka 1985 -'90's Headmaster Mwalimu Amoni Mtera amefariki dunia jana saa 12 asubuhi kwa kugongwa na gari akiwa pamoja na mkewe na jirani yake wakati wanaeleke Mwisho wa lami Gongo lamboto. kupanda gari kueleke mjini.

Marehemu pamoja na mkewe walifunga ndoa mwaka 1985 wakati wote wakiwa walimu wa Pugu.

Ex Pugu PCM class 1987
 
It is very sad,mkewe ambaye pia ni marehemu sasa anaitwa Mwl Edith Kabwoto
 
RIP Mwalimu weti AMON MTERA.
Haya magari haya, yatatumaliza mwaka huu..............Eee Mwenye enzi Mungu tuepushe na hili Jinamizi la Magari yarabialamina
 
Dah! Rest in peace headmaster wangu wa zamani. Nakumbuka sana ubunifu wako wa weekly test ambao ulituwezesha sisi wanafunzi wako kuzidisha bidii katika masomo na hivyo kufanya vizuri ktk mitihani yetu ya mwisho. RIP!

Ex-student 1984 - 87.
 
RIP Mwl Mtera
Hivi hajawahi kuwa mwalimu pale Tambaza kuchukua nafasi ya Mwl Mushi?
 
Jamani huyu alikuwa Mkuu wetu Kahororo pia. Alikuja kuoa akiwa mtu mzima huko Pugu maana aliondoka Kahororo akiwa mseja. Alikuwa mbunifu na aliisadia sana TISS kila mahali apopita kupata vijana wazuri wa idara hiyo.
RIP Mtera
 
R.I.P Mwalimu mwenzangu kwani nimefundisha nae,wakati nakaa ktk nyumba ile aliyekaa Mwal nyerere
 
RIP Mwl Mtera
Hivi hajawahi kuwa mwalimu pale Tambaza kuchukua nafasi ya Mwl Mushi?

Ndio huyu...alikuja Tambaza 1993/4 akitokea Pugu Secondary kuchukua nafasi ya Mwl Mushi baada ya Tambaza kusambaratishwa kutokana na mafujo fujo.

RIP Baba na Mama Mtera.
 
So sad jinsi maisha ya mtanzania yasivyo na thamani. Pole kwa watoto wao kwa kupoteza wazazi wao wote kwa mpigo. Mungu awape nguvu
 
Back
Top Bottom