Mwitikio wa Wananchi juu ya Mlipuko wa Mabomu Gongo la Mboto

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Matukio ya mabomu ya Gongo la Mboto jana usiku yametugusa wengi tulioko mikoani kutokana na watanzania wenzetu kupoteza maisha kutokana na uzembe wa jeshi.

Mpaka sasa ningetegemea TV zetu ziwe eneo la tukio kuwahabarisha watanzania kinachoendelea ila cha ajabu wanatuanonyesha vipindi vya nje ambavyo hatuhitaji kuviona kwa sasa mpaka. bunge lenyewe limehairishwa kutokana na suala la mabomu lakini bado tu TV zetu haziko flexible kubadili vipindi walivyopanga. Hivi TV ziko kwa ajili yao au watanzania.
Leo tungekuwa na Aljazeera yetu tungekuwa tunaona matukio ya Gongo la Mboto live. Ninaomba TBC1 watutendee haki tulioko mikoani kujua kinachoendelea badala ya kusubiri saa mbili usiku watusomee taarifa habari.
Jifunzeni kutoka TV za nje au mnafikiri habari ni zile tu mlizo rekodi? tunahitaji kujua sasa kinachoendelea kwani vipindi vyenu hivi vya kilimo cha marekani na mambo mengine ya ovyo ni upuuzi mtupu wakati hatujui hatma ya ndugu zetu DSM
 
Hii vita ya Milipuko inaenda kwa zamu ilianza na Mbagala jana Gongo la Mboto kesho ni Lugalo keshokutwa ni Kunduchi!!Maana hii serikali haitambui Hazardous zilizopo katika nchi yake hivyo usishangae ukasikia tena milipuko mingine kwenye vikosi vya jeshi nilivyovitaja!!Ni Hofu hofu mashaka tele!!Walinunu mabomu yaue adui yetu sasa yanaua wananchi wake!
 
TV stations zote wamewekwa mfukoni na mkono uliofichama..hawako huru!
Wana shida ya pesa, hawafuati tena maadili ya kutumikia jamii!
Jana badala ya kuonyesha matukio, wanamwonyesha KOVA Akiwaambia watu watulie hapohapo walipo, ili wamalizwe na mabomu!
Coverage nzuri tutaziona BBC na zinginezo za nje!:hungry:
 
Jamani mimi ni mdau wa fani ya usanifu majengo,ktk mengi niliyojifunza kwenye kozi yangu ni pamoja na ushawishi kwa ma-client...kuna hawa ndugu zetu wa mpango mji ambao najiuliza km wamefanya jitihada zozote kuishauri serikali kuhusu umuhimu wa kupangilia maeneo kwa matumizi mbali mbali...ni tusi kwa taaluma yetu kwa mambo yanavyotokea sasa nchini!
 
tv stations zote wamewekwa mfukoni na mkono uliofichama..hawako huru!
Wana shida ya pesa, hawafuati tena maadili ya kutumikia jamii!
Jana badala ya kuonyesha matukio, wanamwonyesha kova akiwaambia watu watulie hapohapo walipo, ili wamalizwe na mabomu!
Coverage nzuri tutaziona bbc na zinginezo za nje!:hungry:
nchi haina viongozii hii
 
wanatia hasira sana hawa,

station za TV kwa sasa zipo nyingi ila ovyooooooooooo kabisa, kwa sasa wanannchi tunahitaji/ tunashauku la kujua kinachoendelea gongo la mboto na wala si vinginevyo.
 
Ilianza mbagala, sasa gogolamboto then inakuja Ubungo, kwa hiyo watu wote mliopo External, mabibo hostel, kibangu mjiandae kwa mabomu... hii nimeitoa kwa rafiki yangu mmoja mwanajeshi kutoka kwenye kambi hiyo, anasema hawajui mabomu yatalipuka lini.:sad:
 
mie basi tena ni Dar es Salaam itazama kama watu hawatakuwa makini... hela ya Dowans tutafute watu wenye akili zao za kutegua mabomu waje wayategue maana sisi tumeshindwa hata Mpwa wa Kijeshi wamechakachuliwa wamechanganywa na mbegu ya Mpwa koko... i need a break
 
nataka kuondoka dar maana nasikia kuna kambi zingine nyingi tu zipo underground sasa hakuna wa kupona hapa mi nasepa naona kikwete anataka watu wakimbie ili wasipate nafasi ya kuandamana
 
Station za TV zote ni za kifisadi mkikumbuka mwaka jana kwenye uchaguzi ndio utajua TZ hakuna Station za TV zililikuwa busy kumuonyesha mgonjwa wa kiharusi (FISADI KIKWETE) kutangaza uongo wake:coffee:
 
Unajua umeongea kitu kilichonichanganya akili asubuhi. Nlikuwa naenda kunywa chai studio,nkakutana na mtu alievaa full sare/kombat akasema ni Mwanajeshi wa Lugalo akiwa anafungiwa kitafunwa kaunta,akapayuka akasema,namnukuu, "...sisi tumeshaushauri uongoz mpaka imeshindikana,iweje tuendelee kutunza mabomu na risasi za wakoloni? Yan yale ya Mjeruman tunayo store! Mi nilitegema tuanze kulipuka sie Lugalo,sasa aya ya Gongo la mboto yameamua kutangulia. Subirini muone faida ya kutunza vyuma chakavu. Mi nko tayari kufa.." Yan watu wamebaki midomo wazi! Kiukweli mi hata hamu ya chai iliisha nkaisi kichwa kimeyeyuka! Wakuu,tusubiri tuone vita ya amani,tunajitakia wenyewe.
 
Hebu tukae chini na kujiuliza, KWA NINI TUENDELEE KUKUMBATIA UOZO WA HAWA VIONGOZI WETU, kuna ndugu yangu mmoja aliniambia nimpe sababu kuu tatu kwa nini watanzania sio wajinga nikashindwa kumjibu, sasa napata majibu.
 
bom2.jpg bomu1.jpg bom3.jpg
Ilianza mbagala, sasa gogolamboto then inakuja Ubungo, kwa hiyo watu wote mliopo External, mabibo hostel, kibangu mjiandae kwa mabomu... hii nimeitoa kwa rafiki yangu mmoja mwanajeshi kutoka kwenye kambi hiyo, anasema hawajui mabomu yatalipuka lini.:sad:

haya hii ni leo asubuhi Huko Gongo la mboto
 
Ilianza mbagala, sasa gogolamboto then inakuja Ubungo, kwa hiyo watu wote mliopo External, mabibo hostel, kibangu mjiandae kwa mabomu... hii nimeitoa kwa rafiki yangu mmoja mwanajeshi kutoka kwenye kambi hiyo, anasema hawajui mabomu yatalipuka lini.:sad:

mkuu inawezekana kabisa kabisa nimetoka pale NGOME MJINI Jamaa ananiambia na sisi tujiandae ......
wa hapa mjini nkamuuliza kwa nini akasema nakupa tu kainfo ...na wewe uaekaa tankibovu unaweza athirika mara mbili .....,nkamuuliza kiutan kwa nini ..akasema tumechoka ..,mmh nkasema kazi ipo kaka
 
Daah kama vipi si tufanye kwenda saka mechi tu na nchi za jirani...mbona tunakaa na kufanyana vibaya wenyewe kwa uzembe wetu?
 
Nadhani Lugalo ndo itakuwa ya kwanza kusambaritisha wasomi wa chuo kikuu chetu cha Dar, chuo cha Ardhi, Chuo cha Maji Rwegarulila, wakazi wa Mwenge kwa Kakobe na vinyago...nk?
 
Back
Top Bottom