Mwitikio wa Wananchi juu ya Mlipuko wa Mabomu Gongo la Mboto

Daah kama vipi si tufanye kwenda saka mechi tu na nchi za jirani...mbona tunakaa na kufanyana vibaya wenyewe kwa uzembe wetu?

Hiyo usiiombee ndugu yangu...madhara yake ni makubwa mno...tuache sisi tunaoendelea kuuguza vidonda ya vita ya Uganda tuuguze... Please never ever think of it anymore
 
Daah kama vipi si tufanye kwenda saka mechi tu na nchi za jirani...mbona tunakaa na kufanyana vibaya wenyewe kwa uzembe wetu?

Tusake Mechi ya nini ??? ya 1978-1979 (Nduli Amin Dada) mpaka leo hatujakaa sawa, na huyu aliyeshika usukani ndio kabisa yeye pekee ni mechi Tosha.......kazi ipo
 
Hebu tukae chini na kujiuliza, KWA NINI TUENDELEE KUKUMBATIA UOZO WA HAWA VIONGOZI WETU, kuna ndugu yangu mmoja aliniambia nimpe sababu kuu tatu kwa nini watanzania sio wajinga nikashindwa kumjibu, sasa napata majibu.


watanzania wengi hawalitaki hili, samahani hata wapinzani hawalioni hili kuwa hata wao ni wajinga, maneno mengi tu njaa imejaa tele! unafiki unaongoza, ebu waambieni wapinzani bara kama wanaweza leo hii kususa bunge ! HAWAWEZI NJAA KALI tumeliwa!!!
 
Dear lovers
Najua huwa pepo wabaya wanawaingiliaga ndugu hasa wakati wa urithi marehemu anapokufa nimeona tuwekane sawa kwa maana serikali imeamua kututoa kafara basi hata ndugu tutakaaowaacha uko nyuma wawe na amani....binafsi nimeona niwahabarishe walio karibu na Kambi za LUGALO,Ngome PALE MJINI UPANGA..ni vizuri ukaandika wosia na dadayangu ni mwanasheria mzuri tu naweza kukusaidia ukalipa just sh 1 ya tanzania ili unaowaacha wawe na amani..nilikuwa na oongea na rafikiy yangu hapa ngome kiutani akanipa ndugu yaani huko jeshin akufai...kama una ndugu wa karibu mjulishe mapema..ile shangigngi yako ..kwa maandishi haya mapepo ya ndugu kuingilia mali za marehemu shida tupu....,..,bada ya Gongolamboto ni

LUGALO


NGOME pale upanga


IKULU

Hizi n habari nyeti na wanajeshi wengi wanajua hili ..Mungu ATURUHEMU
 
Unajua umeongea kitu kilichonichanganya akili asubuhi. Nlikuwa naenda kunywa chai studio,nkakutana na mtu alievaa full sare/kombat akasema ni Mwanajeshi wa Lugalo akiwa anafungiwa kitafunwa kaunta,akapayuka akasema,namnukuu, "...sisi tumeshaushauri uongoz mpaka imeshindikana,iweje tuendelee kutunza mabomu na risasi za wakoloni? Yan yale ya Mjeruman tunayo store! Mi nilitegema tuanze kulipuka sie Lugalo,sasa aya ya Gongo la mboto yameamua kutangulia. Subirini muone faida ya kutunza vyuma chakavu. Mi nko tayari kufa.." Yan watu wamebaki midomo wazi! Kiukweli mi hata hamu ya chai iliisha nkaisi kichwa kimeyeyuka! Wakuu,tusubiri tuone vita ya amani,tunajitakia wenyewe.

Uuuhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, maisha yenyewe ni fimbo tosha, ndg zetu was mbagala bado wanaugulia na maumivu ya yale mabomu, sasa gongolambota na kwingine tena kunatabiriwa. Eeeh Mungu utunusuru
 
ipo kazi kama ndo ivo sasa!!
sasa kama jeshi "wameshachoka" wanamsubiria uyo mkwere apo asambaratishe nchi au?
 
Why are we buying these weapons if we can not handle them??? ni bora tubaki na mikuki na mishale ya enzi za babu zetu kuliko upuuzi wa kununua silaha and then zituuwe wenyewe!! dam it!!!
 
Ina maana wao ndio watumishi pekee wa serikali au? this is not fair.

Damu inahitajika muhimbili tafadhali tujitolee wandungu.
 
Why are we buying these weapons if we can not handle them??? ni bora tubaki na mikuki na mishale ya enzi za babu zetu kuliko upuuzi wa kununua silaha and then zituuwe wenyewe!! dam it!!!

Kwa kweli hazitusaidii badala yake zinatuuwa bila ya makosa,mungu tusaidie tusiongeze silaha nyingine na ahadi ya waziri wa ulinzi baada ya mbagala ni kuzihamisha silaha zote karibu na makazi,sijui anatuambia nini tena Gongo la mboto wamekufa na makazi kuteketea?:sad:
 
Kwa hali ilivyo sasa kuna haja ya kuandamana kushinikiza mabomu yote yateketezwe. Mibomu hiyi isha expire ati sijui wanayakumbatia ya nini? Bila hivyo Dar wote twafa ni kwa zamu tu. Mbagala tayari, G/Mboto tayari. Wakazi wa maeneo mangine yenye kambi tujiandae. Lets do something jamani maana serikali yetu inataka tufe kwa mibomu halafu wanadanganya idadi ya waliokufa. 2009 Ilikuwa mbagala, 2011 Gongo la mboto, 2012 Changanyikiweni, Lugalo, 2013 Kigamboni you can add to the list.
 
Ndg wanajf niwajuavyo viongozi wetu hawa wanasiasa watataka kujichukulia umaarufu usiyo na tija ili mradi tu wasingizie hiki na kile na pia watasababisha msongamano mkubwa wa magari wakati hakuna relief yoyote wanayoitoa kwa wananchi sasa je kweli tunastahili kuwa na viongozi wa aina hiyo?
Kwenu jamvini
 
Ndg naona analysis yako! Umesahau baada ya Dar, yanaanza kulipuka ya Morogoro...kufikia 2100, yanafikia Mwanza, siyo?
 
mmmmh!!nahisi next ni lugalo_OOHH LORD.

Mabomu hawaweki kwa wakubwa yasije kuwalipukia wanahifadhi hukooo kwa kina kajamba nani. Hapa ishu nikuandamana mpaka kieleweke watoe mabomu yote kwenye makazi ya watu wapeleke hukoooo nje ya mji kama Ruvu
 
Ndg wanajf niwajuavyo viongozi wetu hawa wanasiasa watataka kujichukulia umaarufu usiyo na tija ili mradi tu wasingizie hiki na kile na pia watasababisha msongamano mkubwa wa magari wakati hakuna relief yoyote wanayoitoa kwa wananchi sasa je kweli tunastahili kuwa na viongozi wa aina hiyo?
Kwenu jamvini

Na hivi sasa mchakachuaji ndio ameelekea huko. Kama ulivyobashiri, kasababisha foleni katika baadhi ya barabara ili kupisha msafara wake wa magari ya kifahari.

Ombi langu kwako: Rekebisha kichwa cha habari, mabomu ya jana yameripuka gongo la mboto sio mbagala.
 
Mabomu hawaweki kwa wakubwa yasije kuwalipukia wanahifadhi hukooo kwa kina kajamba nani. Hapa ishu nikuandamana mpaka kieleweke watoe mabomu yote kwenye makazi ya watu wapeleke hukoooo nje ya mji kama Ruvu

Unda tume Mpwa!
 
Kwa Invisble: Kama vipi mkuu post za kipuuzi kuhusu gomgo la mboto zifutwe zinatuhuzunisha sana wengine ambao tumeathiriwa na janga hili na ijulikane kuwa JF si sehemu ya kukandia tu au kufanya utani tu tuwaenzi wenzetu jamani! Kingine mkuu kuna post zingine za watu zinahusu gongo la mboto unaziunganisha kwenye ile thread kubwa sasa zinashindwa kufikiwa kwa urahisi! Naomba uziangalie umantiki wake kabla ya kuzichanganya na zingine uziache tu! Wengine JF ndo chombo cha habari sasa mkitulima hivi tunapoteza kujua tumeuliza nini kama post zetu zinainginzwa kwenye thread kubwa! Samahani mkuu kama niko wrong!

Kwa wana JF

Kilichotokea Gongo la Mboto sio kitu cha mchezo wala kucheka! Nadhani kama kwako halikupi homa ungenyamza ukasoma post tu, kuna wengine humu wamefiwa na ndugu zao na huenda usijue hata kuna wengine wameathirka au kufa kabisa i mean wanaJF wenzetu! Ombi: kuna watu wanapost thread za upuuzi sana ambazo hazioneshi kabisa huruma na mtazamo wa janga hili baya kabisa! Naomba wanaopost kama katoka usingizini waache! Kwa mtazamo wangu Mwiba angeotuomba msamaha wafiwa kwa kutoa post inayosema Kuwa kunauwezekano mkubwa kuwa mabomu haya ni njama za Chadema!
Nawasilisha.
 
naunga mkono hoja.... ni wakatis as tuwe sirias na mambo yanayohitaji seriousness
 
Back
Top Bottom