Belinda nimekupata tatizo hapa ni moja tu kuwapata mods imekuwa kazi wao wangeweza kukusanya michango na kuipeleka pale Ofisi ya mkuu wa mkoa misaada itafika tu kwa walengwa.
Kwa Lukuvi,???? He he he
Anyway, njia rahisi mtumie ujumbe wa faragha Robot usikie ana lipi na kusema juu ya hili, naamini ameiona hii thread labda anafiria kitu.
PAMOJA mkuu..
@ nguli, hiyo thread ilianzishwa na game theory inaitwa 'picha itakayomsuta jk na wabunge wake mamilionea'...nimeshindwa kuweka link ila ipo jukwaa la siasa..kuna picha inawaonyesha wanafunzi wamekaa chini na sare zao za shule ( yaani ndo darasani kwao hapo kwenye mchanga).
@ fidel - imani ya watu kuchangia wana mbagala ipo ila jinsi ya kufaniksha hili zoezi ni gumu maana watu tupo sehemu mbalimbali na pia hupati uhakika kama walengwa watafikiwa na msaada wetu. Nikijua utaratibu, nitakujulisha na mie..
Siku njema!!
belinda nakushukuru sana, nina search nikipata nitakufahamisha na mchango wetu tukitoa katika hio shule tutakutumia picha katika private msg/mail....
Karibu mkuu, uta-update imekuwaje na hizo pic!..
Tumepata ile picha aliyoitoaga GAME THEORY tunaitumia kama supporting evedence kupata hela za kununua madawati au hata mabati ya ku-create shed ya muda wakati mipango endelevu kutoka kwa wakuu au taasisi zitakazo jitokeza...[/QUOTE]
Du umenimaliza nguvu kabisa, hadi msubiri hao wakuu wajitokeze watoto wataendelea kung'atwa na sungusungu kwenye makalio, serikali yao pia inasubiri wafadhiri. Hongera fidel kwa kuanzisha juhudi za kuchangia sisi wenyewe, binafsi sitoweza kuhangia hapa kwani nimekwisha fanya hivyo kwenye avenue nyingine.
Peter Masangwa na Salum Pazzy
SERIKALI imeahidi kuwalipa mafao kwa muda wa maisha yao yote, watu wote waliopata ulemavu wa aina mbalimbali kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea katika ghala la silaha la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Aprili 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Wiliam Lukuvi, alisema watu hao watalipwa fidia kulingana na madhara yaliyowapata.
Bw. Lukuvi alisisitiza kuwa Serikali ipo pamoja nao kwamba na itawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.
Alifafanua kuwa mafao watakayokuwa wakilipwa watu hao , yatajulikana baada ya wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa mchanganuo wa kile wanachostahili kuwa wanalipwa kulingana na aina ya ulemavu waliopata.
"Wizara ya Afya ndio inahusika na kufanya hesabu, nimewaagiza watuletee idadi kamili ya watu waliopata ulemavu wa kudumu pamoja na mapendekezo yao," alisema Bw. Lukuvi.
Alisisitiza kuwa taarifa hiyo itaambatana na ile tathmini ya maafa itakayotolewa Juni 13, mwaka huu.
Bw. Lukuvi alisisitiza kuwa yupo makini kwa kuwa anaguswa na maafa yaliyowapata wakazi wa Mbagala.
Kuhusu vurugu zilizotokea wakati wa ugawaji misaada kwa waathirika wa mabomu, Bw. Lukuvi alisema kazi ya kusimamia ugawaji wa misaada hiyo ameachiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Said Mkumbo.
Source:Waliopata ulemavu Mbagala kulipwa mafao milele
Msije kushangaa ikatumika sheria ile ile ya mkoloni...! Mara kila mhanga analipwa shs 20/- kwa wiki kama si kila mwezi.Usanii tu mwingine!!!! Je Tz ina walemavu karibu 10% ya Watz wote kwa data za WHO.. je serikali inawapa nini kwa sasa?
Walemavu ni sehemu ya jamii..05% ya nafasi kazi zote inabidi kutengwa kwa ajili yao..kama China! Usipolipa basi 10% ya faidi yako unatoa kusadia walemavu!
Pia inabidi tuwape pesa za kuishi na kuwalipa say 80,000 Tshs kila mwezi kwa kila familia yenye mlemavu!
Huu ndo uzalendo!