Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

Samahani si kwamba sielewi ila tu nauliza hizo pesa wanazolipwa fidia ni za kujenga nyumba nyingine mpya au kurekebisha mahali palipoharibiwa na mabomu? Mbona 168,000 ni ndogo sana kwa kujenga nyumba mpya?

kwa mujibu wa radio tumaini alfajiri ya leo nasikia kuna watu wamepewa hadi sh 30,000/=.nimeshtuka sana,ikawa kama ndo alarm ya kuniamsha.nikapiga maji nikachapa mwendi kibaruani!
NAOMBA UFAFANUZI KATIKA HILI
 
Mimi na wasiwasi sana kuhusu hizi fidia za wahanga wa mbagala. Siamini kama mambo yataenda kihalali pila kutokea mchezo mchafu wa hapa na pale. Siku zote, linapokuja suala la pesa Tanzania, lazima utegemee dhuluma na vitu kama hivi!

Watu walishaanza kuiba magodoro tangu mwanzoni wakati wa kutoa msaada. Hapa kuna watu wanatumia hii nafasi kujinufaisha na hizi pesa zitaenda mifukoni mwa watu na kuwaacha wenzetu kwenye majonzi, na si fidia.

Mimi nimesikia kuna watu wamelipwa hadi milion 70, huku wengine wamepewa Tsh 30,000... hivi ni nini hichi kama si mchezo mchafu?

Hivi ni lini watanzania tutakuwa na utu na roho ya upendo na kusaidiana kama tunavyoona kwa wenzetu? Inahuzunisha sana jamani!
 
aliyepiga picha ya mzee huyo,auwekee picha ya nyumba yake tuone ili tulinanishe,mimi nafikiri ni sawa,sasa kama mtu alikuwa na ibanda cha nyasi unafikiri alipwe kiasi gani
 
Samahani si kwamba sielewi ila tu nauliza hizo pesa wanazolipwa fidia ni za kujenga nyumba nyingine mpya au kurekebisha mahali palipoharibiwa na mabomu? Mbona 168,000 ni ndogo sana kwa kujenga nyumba mpya?

Mbona huyo mzee kapata nyingi kuna mwingine kapata 30,000/=
MJ1 hizo pesa ndo fidia ya kujenga au kukarabati nyumba zao inasikitisha sana ndo hapo utaamini viongozi hatuna unampa mtu fidia ya 30,000/= akafanyie nini? Atanunua mifuko 2 ya Cement alafu pesa kwisha.
 
Mbona huyo mzee kapata nyingi kuna mwingine kapata 30,000/=
MJ1 hizo pesa ndo fidia ya kujenga au kukarabati nyumba zao inasikitisha sana ndo hapo utaamini viongozi hatuna unampa mtu fidia ya 30,000/= akafanyie nini? Atanunua mifuko 2 ya Cement alafu pesa kwisha.

Fidel!

Hivi unashangaa nini? Tatizo la waTZ siku zote ni elimu na kutokutaka kujifunza. Wote ni wajinga na kwa mtaji huo usitarajie sisiemu kutoka madarakani mpaka kifo kitakapo tutenganisha yes nasema naomba masikio .Kwani wamepunjwa nini madiai yao uliwahi kuyaona tangu waanze kudai sijui kama kuna kitu wanachodi wao waliomba fidia na Lukuvi si amewapa akisaidiwa na Bunge zima?

Mungu apitishie mbali! Mimi ningekuwa mwadhirika wa mabomu Mbagala nisingefanya upuuzi na ujuha waliofanya wale ambao nyumba zao zlibomolewa/kuharibiwa na yale mabomu ikiwa ni pamoja na ambao ndugu zao walipoteza maisha RIP!!

  • Milipuko ya Mbagala ilikuwa ni uzembe wa serikali ya CCM!!!
  • Anayetakiwa kutoa fidia ni serikali ya CCM
  • Aliyefanya tathimini ya viwango vya kulipwa ni serikali ya CCM
  • Aliyehakiki tathimini ya fidia ni serikali ya CCM
  • Anayetoa pesa ni serikali ya CCM
  • Anayesimamia malipo ni serikali ya CCM
Ukijumlisha hayo hapo juu unapata ni kizungumkuti!! Walitakiwa nao wafanye tathimini kwa kuomba hata kama ni msaada kutoka kwa wanafunzi wa UCLAS kwa ajili ya kupata angalau mizania.

Endapo serikali ikiwa imewapunja au inakataa kuwalipa kwa dhamani ya soko ndiposa wafungue kesi mahakamani wakapambane mahakamani na ikichemsha kwani mahakimu ni wa serikali ya CCM sisi tuwaunge mkono na iwe cheche na chimbuko la mapinduzi ya umma.

Kwa sasa hawana jini wachukue hizo sente wakalilie kwenye yale mahame.

Wakipata akli wajaribu mapendekezo yangu vinginevyo imekula kwao!!

Tuache porojo na unafiki wajinga ndio waliwao!!!
 
Imefika wakati watanzania tuwe serious na mambo yanayohusu maisha ya watu. Watumishi wa umma waliofanya kazi hii ya kipuuzi ni watanzania lakini wanaona ni sawa tu kuumiza wenzao. Shillingi 30,000 hata kama ni nyumba ya nyasi utafanyia nini?

Wanaharakati wa sheria wasaidieni watu hawa kudai fidia mahakamani. Ni uzembe wa serikali lazima wawape haki yao.
 
Mchili!

Utawasaidia kama hawajaomba? Kama hawakuweza kujenga hoja kisayansi ili walipwe hao wanaharakati unawatafuta kutoka wapi! Kama sijakosea wewe na mimi who can see light at the end of the tunnel should join hands and help them yes! Ila kwa sababu wamezoea mambo ya kuomba haki badala kwa staili ya CCM yamkini imekula kwao! Katika falsafa ya mapambano ya kitabaka haki huwa haiombwi bali unajichukulia hata kama ikibidi ufe haki kamwe haiombwi!!! Take care!
 
Na huko Mbagala ndiko CCM ilizoa na itazoa tena kura zote bila ya mpinzani eti kushinda .Hivi hawa watu hawawezi kwenda Mahakamani kufungua kesi ? Mawakili wa kujitegemea hawako tayari kujitolea kusaidia hawa masikini ?
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Imetolewa na Ashura Mustafa
Naibu Mkurugenzi Uenezi na Mahusiano na Umma
Agosti 25,2009


CUF – Chama Cha Wananchi kinashangazwa na serikali ya Tanzania kwa kutowajali wananchi wake hasa pale wanapofikwa na majanga au wanapotakiwa kulipwa fidia kwa ajili ya upotevu na uharibifu wa mali zao au kwa ajili ya mafao yao ya uzeeni, hali hii iliyojitokeza Mbagala iliwatokea pia wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, alitangaza rasmi serikali itatumia zaidi ya bilioni 8 kwa ajili ya kuwalipa fidia zaidi ya nyumba 9,000 zilizokumbwa na athari za tukio la Mabomu April 29 mwaka huu, hii inaonyesha kuwa serikali ilifanya tathimini ya nyumba pamoja na mali zao kwa waathirika.

Hivyo basi, haileti maana nyumba yenye thamani ya milioni 13 mwaka 1993 leo hii ilipwe fidia ya milioni 4.3 bila kuzingatia kupanda kwa gharama za ujenzi. CUF - Chama cha Wananchi inaitaka Serikali ifanye tathimini ya uhakika na sio ubabaishaji na izingatie madhara yaliyowafika wananchi na iwalipe fidia ya mali zao kila mmoja na sio kuwalipa nusu harasa ya mali zao zilizoharibika au robo ya mali hizo.

HAKI SAWA KWA WOTE

Kwa mawasiliano zaidi
0777 727341


Source: GLOBAL PUBLISHERS LTD.​
 
Lukuvi amsaka aliyelipwa fidia ya Sh30,000

Minael Msuya na Aziza Athuman - Mwananchi​

SERIKALI mkoani Dar es Salaam inamtafuta mkazi wa Mbagala Kuu, Kaisi Salum aliyelalamika kupunjwa malipo ya fidia za waathirika wa mabomu baada ya kupewa Sh31,000 kwa ajili ya kuziba ufa uliotokea kwenye nyumba ambayo ujenzi wake bado haujaisha.

Mkuu wa mkoa, William Lukuvi, ambaye pia na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapa, aliliambia gazeti hili jana kuwa Kaisi aliyechukua fidia kwa ajili ya matengenezo ya nyumba namba 340, anatafutwa na polisi kujibu shutuma kwamba amepunjwa katika malipo hayo.

Kaisi alitengewa kiasi hicho baada ua nyumba yake kufanyiwa tathmini na kamati ya serikali ya maafa, lakini anadai malipo hayo ni madogo kwa kuwa hayalingani na gharama za Sh3 milioni alizotumia kujenga nyumba hiyo.

Lukuvi alisema jana kuwa uchunguzi wao umebaini kuwa nyumba hiyo ilikuwa bado iko katika hatua ya ujenzi na ilifikia kozi tano huku ufa uliosababishwa na milipuko hiyo ukionekana kuwa ni mdogo.

"Vyombo vya hahari vimeweza kupenyeza na kuipata nyumba hiyo ambayo inaonyesha kuwa na ufa mdogo ambao hata fidia aliyopewa ni kubwa kulingana na ufa ulioonekana," alisema Lukuvi akizungumzia Sh31,000 alizolipwa mkazi huyo, kiasi ambacho kinaweza kutosha kununulia takriban mifuko miwili ya saruji.

Alisema, polisi inamsaka Kaisi kwa kuwa mbali na kuishutumu serikali, alifanikiwa kuwashawishi waathirika wengine wa mabomu kugoma kuchukua fidia zao kwa madai kuwa ni ndogo.

"Mtu huyu ndiye mshawishi mkuu katika kukwamisha zoezi la kuwafidia waathirika wa mabomu kwa kuwa aliweza kuwashawishi wenzake wasichukue fedha za fidia," alisema Lukuvi.

"Huyu ni fisadi wa nchi kwa kuwa alitaka apate kiasi kikubwa cha fedha, bila kujali wenzake ambao hawana makazi ya kuishi kutokana na uharibifu uliojitokeza. Alitaka fidia itolewe kama ilivyotolewa kwa watu wa Tabata Dampo kipindi kilichopita, nyumba zao zilipobomolewa na kupewa Sh20 milioni bila kujali," alisema.

Mabomu yalilipuka kutoka ghala la silaha April 29 mwaka huu na kusababisha madhara kwa wakazi wa eneo la hilo, ikiwa ni vifo vya watu 24 askari sita na nyumba zaidi ya 9,000 kuharibiwa.


Serikali ya Tz ni kama fisi ambaye kwa ulafi wake,

anaamua kuvitafuna vitoto vyake.
 
Back
Top Bottom