Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

Mhanga ninavyojua mimi ni muathirika, kiingereza victim.

Nime confirm hapa kwenye kamusi project

http://kamusiproject.org/en/lookup/sw?Word=mhanga


mhanga , pl wahanga { English: victim, pl victims }
noun 1/2 [ photos: upload ]

Swahili Example: Harakati za kuwasaidia Wahanga wa gharika ya Tsunami iliyotokea kusini mashariki mwa Asia, Desemba 26 mwaka wa jana zinaendelea. [Erasto Mbwana, Radio Deutsche Welle]
 
Nature, Afande kuchangia wahanga milipuko Mbagala

03 May 2009
By Amour Hassan

Nyota wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature na Afande Sele wanatarajia kurekodi wimbo wa kulilia waliopatwa na maafa yaliyotokana na milipuko ya mabomu kwenye kambi ya jeshi iliyopo Mbagala, Dar es salaam na wamewataka wasanii kufanya onyesho la hisani kuchangia waathirika hao.

Rapa wa Morogoro Afande Sele amesema kwa njia ya simu jana kuwa alikutana na Nature juzi Ijumaa wakati wakitumbuiza kwenye sherehe ya kukabidhiwa mabasi kwa timu za Simba na Yanga na wakajadili juu ya uzito wa athari za milipuko hiyo.

``Nature ameniambia kuwa naye ni mmoja wa waathirika wa milipuko ile.

Ni jambo kubwa sana, watu wengine wanachukulia wepesi, lakini ni tatizo kubwa sana.

Watu wamepoteza maisha, wengine wameachwa na ulemavu wa maisha, wengine wameachwa wakiwa masikini kabisa hawana hata pa kulala, na viongozi wa nchi wasilichukulie poa suala hili ni zito kuliko wanavyofikiria.

``Kuna matukio mengi yanasababishwa na uzembe na yanawaathiri wananchi, hivi ni vitu vya kuchukuliwa hatua. Kwanini kambi kama ile isiende kuwekwa huko maporini? Kuna mapori mangapi hapa nchini?`` alisema.
 
Nature,ni haki yako kulalamika Pole sana...ila usiwe msemaji mkuu wa hasa mambo ya jeshi...maana wakati kambi hz zinajengwa kulikuwa pori tena kubwa sana by then was 1978.hapo ni kuitisha watalaam waone jinsi gani ya either kutoa zana nzito au kuhamisha kambi kabisa ila sasa hata kambi ikihamia pori la pande,au popote wananchi watafuata tu hata familia askari watahitaji shule,hosp etc...wananchi watafuata huduma za kijamii,umeme pia....upo??suala tuwaachie wataalam watuaidie ushauri.kambi zote za dar zinalinda mji wa dar na uvamizi wowote wa adui......
 
Jamani zoezi la kuyalipua mabomu huko Mbagala limekisha anza? Mlio karibu tufahamisheni jamani manake wengine tuka maghorofani. Hayakawii kupoteza mwelekeo!
 
ukishaona unashuka bila lifti ujue ndo imekubali hiyo
nadhani walikuwa wanatutega hakuna bomu lililosikika hadi sasa.
 
Mhanga ninavyojua mimi ni muathirika, kiingereza victim.

Nime confirm hapa kwenye kamusi project

Search Results for 'mhanga' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'mhanga' | The Kamusi Project


mhanga , pl wahanga { English: victim, pl victims }
noun 1/2 [ photos: upload ]

QUOTE]

BLURAY,
Najiunga na Kyakya kuhoji neno hili.
Umetoa rejeo la kwamba umethibitisha kutoka Kamusiproject.

Ni kweli kwamba kamusi project wameeleza hivyo, lakini si lazima wawe sahihi,.

Kwa mtazamo wangu, waathirika si wahanga.

Wahanga ni watu wanaojitolea kupoteza maisha yao ili kuleta maafa kwa wengine.

Tunapaswa kwauliza, mtu ajitoae mhanga yeye ni mhanga, au yule anyeathiriwa ndiye mhanga?
 
Mhanga ninavyojua mimi ni muathirika, kiingereza victim.

Nime confirm hapa kwenye kamusi project

Search Results for 'mhanga' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'mhanga' | The Kamusi Project


mhanga , pl wahanga { English: victim, pl victims }
noun 1/2 [ photos: upload ]

QUOTE]

BLURAY,
Najiunga na Kyakya kuhoji neno hili.
Umetoa rejeo la kwamba umethibitisha kutoka Kamusiproject.

Ni kweli kwamba kamusi project wameeleza hivyo, lakini si lazima wawe sahihi,.

Kwa mtazamo wangu, waathirika si wahanga.

Wahanga ni watu wanaojitolea kupoteza maisha yao ili kuleta maafa kwa wengine.

Tunapaswa kwauliza, mtu ajitoae mhanga yeye ni mhanga, au yule anyeathiriwa ndiye mhanga?

Wewe unabishana na kamusi sasa.Hakuna sababu kwa nini vyote visiwe sawa.

Anayejitolea kupoteza maisha yake si muhanga, bali "anajitolea muhanga" muhanga in this sense is self sacrifice, which is a different meaning.

Muhanga pia victim kama ilivyoelezwa na kamusi hapo juu.
 
Inaniuma sana ninaposikia habari kuwa wale wanaogawa misaada kwa waathirika wa mabomu waishio karibu na kambi ya jeshi - Mbagala, wanafanya kazi hiyo kwa upendeleo.
Wagawaji hao eti wanavaa T-shirt za CCM? Hivi tuna lengo la kusaidia wahanga hao au ndio fusrsa ya kukitangaza chama!!!? Pengie ndio, kama waswahili wasemavyo "kufa kufaana", lakini jamani huu si utu! Hapa nchini kila kitu tunakitazama kisiasa tu, na hii ndio sababu inayofanya taifa letu lisiwe na maendeleo, kwani kila kitu kinafanyika kisiasa. na kila mtu analinda maslahi yake binafsi.
Sasa kama ndio ugawaji wenyewe ni wa kibaguzi maana yake nini? Mtu anavaa kabisa 'jezi' ndipo anaaza kufanya ufisadi!!! Tunaelekea wapi watanzania?
Nikihamia upande wa pili, hawa wahanga wenyewe, baadhi wanafaya uhuni, kuorodhesha majina 'yasiyo' au ujanjaujanja wowote, ilimradi tu 'wawazunguke' wananchi wenzao. Utu, ni jambo la msingi, Tuwe na utu ngudu zangu!
Semeni wadau, kama ninawawazia vibaya hawa wagawaji wanaovaa T-shirts za CCM, ili nami 'konshes' yangu itulie.:rolleyes:
 
Last edited:
Wakazi wa Mbagala waandamana kumkataa Mkuu wa mkoa Dar

Jackson Odoyo na Fredy Azzah
Mwananchi

WATU zaidi ya 300 walioathiriwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Aprili 29 kwenye kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyo Mbagala, jana waliandamana kutaka mkuu wa mkoa wa Dar es Saalaam, William Lukuvi, aondolewe.

Milipuko hiyo iliyotokea kwa ajali kwenye ghala la silaha ilisababisha watu zaidi ya 26 kupoteza maisha yao, nyumba kuharibiwa na wengine wengi kujeruhiwa. Pamoja na JWTZ kuchukua hatua za kudhibiti mabomu zaidi yasilipuke, hali iliendelea kuwa mbaya wakati mabomu karibu matano yalipolipuka wiki iliyopita, siku ambayo jeshi hilo lilitangaza kuwa lingeharibu mabomu manne.

Na Lukuvi akawataka wakazi wa Mbagala kuzoea milipuko kama wenzao wa Kipawa, wanaoishi jirani na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, walivyozoea kelele za ndege.

Lakini kauli yake iliudhi wakazi wa Kipawa, na sasa wananchi wa Mbagala wanataka mkuu huyo mpya wa mkoa, aondolewe Dar es salaam na jana walidhihirisha uthabiti wa kauli yao wakati walipoandamana kutoka Mtaa wa Kizuiani hadi Mbagala Kuu.

Waandamani walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali zikiwa na maneno kama “tunataka haki yetu, tunataka haki yetu". Baadhi walichukuliwa na lori la JWTZ hadi ofisi ya Mtaa wa Kizuiani, takribani kilometa saba kutoka Mbagala Kuu.

Akizungumza na waandishi wa habari katikati ya kundi la zaidi ya wananchi 300 waliokusanyika katika ofisi ya mtendaji wa Kata ya Mbagala Kuu, kiongozi wa maandamano hayo, Mashaka Selemani, ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kizuiani, alisema Lukuvi hajielewi na kwamba aondolewe kwa kuwa mkoa umemshinda.

“Watu wanakufa Mbagala, yeye amekaa huko bomani anasema watu wayazoee mabomu kama watu wa Kipawa walivyozoeya milio ya ndege?” alihoji Selemani.

“Hiyo ni kauli ya kiongozi aliyeshindwa kuongoza. Tunaomba aondolewe kwa sababu ameshindwa kuongoza mkoa.”

Wananchi hao walimsifu mkuu wa wilaya ya Temeke, Saidi Mkumbo wakidai kuwa amefanya kazi kubwa.

“Lukuvi ndiye anayeleta siasa zake mpaka zoezi hili linaonekana kujaa mizengwe na kufanya watu waendelee kukosa misaada. Mkuu wa wilaya amejitahidi sana kufanya kazi kila siku tunashinda naye huku,” alisema Selemani.

“Kiongozi mzuri ni yule anayekuwa karibu na wananchi wake, wakati wa shida na uimara wake katika uongozi pia unaoneka wakati matatizo kama haya, lakini Lukuvi anakuja Mabagala kutoa takwim zisizo sahihi za mabomu,” alisema mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Makweya.

Makweya, ambaye ni mjumbe wa shina namba tatu lililo Mtaa wa Kizuiani alisema: “Lukuvi amekuwa mbali na wananchi wake huku akitoa kauli za ajabu na sasa kutoka na kauli yake ya kutukashfu... kwa kauli mmoja tunasema hatumtaki na hatumtambui kama mkuu wa mkoa huu.”

Hali ya ugawaji misaada iliendelea kutawaliwa na lawama na tuhuma na Selemani alisema kuna watu walioathirika ambao hadi leo hawajapata msaada wowote.

“Watu hawa hawajapata msaada wowote tangu nyumba zao zilipolipuliwa na mabomu hayo, ingawa misaada inafikishwa katika eneo hilo, lakini inagawiwa kwa watu wasiohusika,” alisema Selemani.
 
Lukuvi inabidi atengenezewe thread yake peke yake...yale madudu aliyozungumza kwenye msiba wa IDDI NYUNDO nikajua kuwa kazi tunayo watu wa Dar
 
Lukuvi ni reflection ya aliyemteua, kumkataa na kumbakisha aliyemteua kutasaidiaje ?
 
Hivi Mkuu gani wa Mkoa alikuwepo wakati mabasi yetu ya TATA kwa ajili ya wanafunzi wa Dar yalipokufa na kutufanya tuanze tenda kupanda Sai Baba na Chai Maharage?
 

Huwezi ukaripoti habari kuhusu kauli tata ya kiongozi bila kusema alitamka nini kwa maneno yake mwenyewe.

Yeyote yule anaejua alichokisema Lukuvi kuhusu kuzoeleka kwa milio ya ndege na akiweke hapa word for word.
 
Back
Top Bottom