Mwigulu Nchemba nusura azichape na Msigwa leo

Status
Not open for further replies.
CCM akili fupi.Sisi tunajua kuwa bunge linarejea Jumatatu maana wiki hii lilikuwa kwenye kamati ya matumizi.Nilimsikia Makinda akisema juzi hili ndilo bunge tulilolijua toka nyuma, wiki hii imekuwa kila kitu ndiyo na mipasho ya kusifia tu.Watazamaji tulikuwa tunakosa uhondo sana

Ana shida kubwa kichwani! Nashindwa kuelewa, hivi wanapo tembelea Mabunge ya nchi za wenzao hapa duniani, huwa wanajifunza nini? Au ni hizo posho za safari ndio muhimu kwao?

Hivi katika ulimwengu huu wa leo, kwa kiongozi kama yeye bado anawaza Bunge la Chama Kimoja? Nina hakika hata kiti anacho kikalia hajui hadhi yake.
 
Mwingulu bwana!!! Jana nilimuona kupitia VOA akiyatoroka maneno yake kwa kasi ya ajabu. Bahati yake ni kwamba Kamanda G. Lema hakuja hewaani...
 
Umeshika makalio ya nyani, unauliza tundu liko wapi?

Ahsante kwa taarifa ya moto moto.

Nadhani Mwigulu amburuze mahakamani kwa kuwa hawakuwa bungeni ambako kuna kinga. Hata ningekuwa mimi ningemukwida.

Kwa maana hiyo Msigwa anataka kutuambia kwamba Mwigulu ndoiye aliyesababisha mauaji huko Arusha?
 
Ila sometimes mimi naona hawa Wabunge wetu wamezidisha bifu za kijinga! Sioni wa kumtetea hapa!
 
Mwigulu anajua chimbuko lake kweli..Ajitafakari na hazina ya uongozi wa baadae..Asije kimbia nchi tu
 
Hakuna mtanzania anayeiogopa tena ccm leo, wamepoteza uwezo wa kuongoza wametumia vitisho navyo vimekwama sasa wataanza kukimbia wao....

Ngoja nitaleta barua yangu ya MMS ya kumchumbia Mamndemenyi nipunguze mawazo huku kwenye siasa kunaweza nipunguzia umri wangu wa kuishi bure.
 
Katika tukio lililotokea
leo kwenye ukumbi wa St.Gasper Dodoma ambako wabunge wote wapo kwenye
semina ya masuala ya ukimwi ambayo inaendelea kumetokea mtifuano na
nusura Mwigulu arushe ngumi baada ya Mch.Msigwa kumuita kuwa ni muuaji
na hivyo atubu kutokana na damu za watoto wadogo na wakina mama wa
Arusha ambao amekatiza maisha yao kwa sababu ya ukatili ambao hauwezi
kuendelea kuvumiliwa kamwe.

Tukio hili lilifuatia baada ya wabunge wa Chadema ambao wameanza kurejea
Dodoma kwenye Semina hiyo walipokuwa wakiwaambia wabunge wa CCM kuwa
Bunge linarejea jumatatu kwani sasa limeshamaliza kukaaa kama kamati ya
matumizi , hivyo litarejea kwani wabunge wa Chadema watakuwepo hali
iliyozidisha hasira za wabunge hao ambao wengi wanaonekana kuwa na hang
over za jana ktk kumuaga Sitta.

Mwigulu alinyanyuka kwenye kiti na kumfuata Msigwa na kumshika kifuani
ila wabunge wenzake walienda kuamulia ugomvi huo na hali bado iko tete,
semina inaendelea .

faida za kuwa Jf ni kupata habari za moto moto.

Huyu Mwigulu nimetoka kuwasiliana naye kwenye Fikra Huru na kuonekana makini sana,alionekana kujitambua sana na wala hatukwaruza pamoja na mm kuonyesha msimamo wangu kichama? au sio yeye?
 
kweli hapa wametuibia,semina ya ukimwi kwa wabunge,WHAT?.
Hujui kuwa tunaelekea mwisho wa mwaka wa fedha za Serikali sasa zikibakia huwa sijui zinapelekwa wapi maana bajeti mpya imeshasema vyanzo vya mapato ya mwaka huu na hakuna mahali waliwahi kuonyesha mabaki ya fedha za mwaka uliopita .......
 
Ahsante kwa taarifa ya moto moto.

Nadhani Mwigulu amburuze mahakamani kwa kuwa hawakuwa bungeni ambako kuna kinga. Hata ningekuwa mimi ningemukwida.

Kwa maana hiyo Msigwa anataka kutuambia kwamba Mwigulu ndoiye aliyesababisha mauaji huko Arusha?

Kama si Mwigulu anayehusika na mabomu, sasa ni nani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom