Mwigulu Nchemba ataka msajili wa vyama kusitisha Operesheni Sangara za CHADEMA

mzinzi 1st class! Oh my Gosh where is my wife. Mama Esther, mama Esther, . . . . .
 
Mwigulu anaweweseka. Unacheza na DAMU ya Mtu. Tena Mtu ambaye Yuko Jimboni Kwako. Ile ya Igunga na Arumeru haiwezi Kumtesa. Hii ya Jimboni kwake Itamtesa kwa Sababu Kila atakapokuwa anakwenda atakuwa anawakumbusha watu MACHUNGU

Mwigulu Badilisha Strategis Hizi za MAUAJI Hazifai

Anafikiri stori anazotengeneza kwa kushirikiana na polisi na magazeti zitawadanganya hadi waliokuwepo eneo la tukio. Lengo lake la kauzuia operation sangara kwa gharama ya maisha ya mtu halitafanikiwa na kumbukumbu ya mauaji aliyosababisha itamgharimu ubunge wake. Wananchi wa ndago sio tu wameshuhudia kilichotokea bali pia wanaufahamu mpango mzima ulivyosukwa na kwakuwa mwenzao kawatoka, hawatamwangalia tu. Kila atakapopita jimboni watakumbuka machungu na kuzipandisha hasira zao juu yake..
 
Mwigulu Nchemba ni mtoto mdogo,
Katika masuala ya siasa,
Yeye anadhani anajijenga,
kumbe ni buffer ya wazee wa CC.

Kule NEC wanamvisha kilemba cha ukoka,
CC wanatoa baraka,
yeye anadhani yupo kileleni,
saa ikifika atajua maana ya kilemba.

CC ya CCM siku zote,
Ni lazima iteue,
Kondoo wa kafara,
This time kondoo,
ni Mwigulu Nchemba.

Si muda mrefu,
Watanawa mikono wote,
na kumwacha ajibu mwenyewe,
Ikibidi afe kisiasa,
na kuinusuru CCM.

Yeye hatakuwa wa kwanza,
wala hatakuwa wa mwisho.

Kila dhambi ina kafara yake.

Hajui afanyacho,kama Nape vile.
 
Katika kile kinachoonekana kutafuta mahali pa kujishika, Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba amemtaka msajili wa Vyama vya siasa nchini John Tendwa kusitisha mara moja operesheni Sangara za chama hicho kwa kile anachodai zinatishia amani ya nchi.

Mwigulu alisema baada ya mazishi ya kada wa chama chake hapo jana yaliyotokea huko Ndago atahakikisha anapambana kwa nguvu zote na CHADEMA ili kukomesha tabia yao.

Source:Habari Leo

My Take:
Wachunguzi wa mambo wanadai kuweweseka huku kwa Mwigulu ni kutokana na kutuhumiwa kama mhusika mkuu wa mauaji yaliyotokea kwa kile wanachodai alikodi vikundi vya vijana na kuwapa hela ili wakavuruge mkutano wa CHADEMA na ndipo wananchi walipozidi nguvu kikundi hicho cha wahuni na kuwatimulia mbali.

Hata hivyo mpaka sasa bado jeshi la polisi halijafanya mahojiano yoyote na Mwigulu ili kuchunguza madai hayo. Mwigulu amekuwa mara nyingi akitoa maneno ya hovyo na matusi dhidi ya CHADEMA hasa awapo bungeni na kwenye mikutano ya hadhara.

Tayari jimbo lake la Iramba Magharibi CHADEMA ina nguvu kubwa na kuna uwezekano mkubwa Mwigulu asirudi tena bungeni baada ya uchaguzi ujao.

yule chizi; si muda mrefu mtamkuta mirembe amefungwa mikono yote.
 
Mwingulu kumbe na yeye ameanza kutoa maagizo kwa tendwa!
Nilimwambia mwingulu hii laana ya mauaji haitamuacha sasa ameanza kuchanganyikiwa na kutoa maagizo na kuomba shughuli za bunge zisitishwe.

Sito shangaa mwingulu kuomba serikali hii fute cdm kwenye orodha ya vyama na hii laana itamtesa mwingulu mpaka atakapo kiri kusababisha mauaji!
 
Mwigulu imarisha chama baba, pigana na hao cdm muda si mrefu utashinda na Urais tutakupa
 
Kimsingi Mwigulu ndiye mhusika mkuu wa mauaji hayo kwa kuwa ndiye aliyewatuma, lakini mbona hakamatwi? tunakumbuka yale mauaji ya Arumeru baada ya uchaguzi, kiongozi wa chadema alichinjwa je nani alikamatwa? wabunge wa chadema mwanza walivyonusurika kufa nani alikamatwa? hayo ni machache tu yanayoonesha kuwa jeshi hili ya polisi ni kwa kwa ajili ya CCM
 
Kwa kawaida Mtu aliyetoa hela kuhamasisha fujo ndio mshukiwa numba moja wa mauaji!! Sasa iweje tofauti kwa Tanzania? Utawala wa sheria uko wapi? Baba Kikwete amka ndugu yangu Mkuu wa nchi!! Hawa akina Mwigulu wanakuaribia!! wewe ndio Raisi wa nchi hii!! Watu Wakifa watu watakusulubu kama anavyosulubiwa Hosni Mubaraka!! Ukumbuke Mubaraka Hakushika hiyo SMG Kuua!!
 
nilikuwa namkubali sana mwigulu before lakn tangu aanze kupewa umeja kampeni kaharibika kabisa, hata elimu yake haimsaidii, I HATE MWIGULU ataleta fujo na mauaji zaidi ya haya
 
Katika kile kinachoonekana kutafuta mahali pa kujishika, Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba amemtaka msajili wa Vyama vya siasa nchini John Tendwa kusitisha mara moja operesheni Sangara za chama hicho kwa kile anachodai zinatishia amani ya nchi.

Mwigulu alisema baada ya mazishi ya kada wa chama chake hapo jana yaliyotokea huko Ndago atahakikisha anapambana kwa nguvu zote na CHADEMA ili kukomesha tabia yao.

Source:Habari Leo

My Take:
Wachunguzi wa mambo wanadai kuweweseka huku kwa Mwigulu ni kutokana na kutuhumiwa kama mhusika mkuu wa mauaji yaliyotokea kwa kile wanachodai alikodi vikundi vya vijana na kuwapa hela ili wakavuruge mkutano wa CHADEMA na ndipo wananchi walipozidi nguvu kikundi hicho cha wahuni na kuwatimulia mbali.

Hata hivyo mpaka sasa bado jeshi la polisi halijafanya mahojiano yoyote na Mwigulu ili kuchunguza madai hayo. Mwigulu amekuwa mara nyingi akitoa maneno ya hovyo na matusi dhidi ya CHADEMA hasa awapo bungeni na kwenye mikutano ya hadhara.

Tayari jimbo lake la Iramba Magharibi CHADEMA ina nguvu kubwa na kuna uwezekano mkubwa Mwigulu asirudi tena bungeni baada ya uchaguzi ujao.

Tupo, Mwigulu harudi bungeni, hiyo sahau.
 
Sasa mwigulu kama ulikuwa utaki operation sangara ndo mpaka uuwe mtu???????????sa na wewe si uanzishae operation SAto
 
Utter gutter politician. Youth has been badly late down by Mwigulu, coz he's displyaing the kind of immaturity wrapped in egoism in a selfishness vehicle.
 
Hizi siasa za Tanzania mh, hii ngoma ya vyma vingi kucheza kwake kugumu, hasa pale mmoja anakuwa ndiye mtoa mareferees!
 
Mwigulu Nchemba ni mtu asiyemakinim kabisa kisiasa na anapenda sana sifa zisokuwa na msingi namkumbuka tangu akiwa pale UDSM.Reasoning yake ina mashaka kwani haizingatii mslahi mapana ya taifa ambayo ni kuwapa watu nafasi ya kuamua kiongozi wanayemtaka.Hivi huyo kiongozi wa CCM alifuata nini kwenye Mkutano wa CDM.Acheni kujifanya nchi hii ni yenu.Nawakumbusha nchi hii ni ya Wananchi na si ya CCM.TUWAAACHE WAAMUE.
 
Habari za uhakika nilizozipata kutoka Singida zinasema Mwigulu ndo chanzo cha machafuko kwa kugharimia vijana ili wafanye fujo mkutano wa CHADEMA, alafu bila aibu anataka spika asimamishe mijadala ya bunge ili bunge lijadili uhalifu ambao yeye ndo master mind. Aibu sana kuwa na viongozi kama hawa ambao hawawezi ku-foresee the consequences of their actions.
 
Back
Top Bottom