Mwenyekiti wangu CCM Jakaya Kikwete: Lowassa's buck stops with you!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,906
13,211
Seke seke la Lowassa kutaka kuutwaaa urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, kwa kutumia umaarufu wake wa fedha zake na"marafiki zake", limeanzakuchukua sura ambayo sasa inatishia uhai wa CCM kama chama chenye mshikamano.

Mshikamano uliozoeleka katika hafla tofauti za kitaifa sasa zimeanza kubinafsishwa kwakuwa na hafla binfsi zenye kuweza kutoa matamko mazito ya "Ndoto za safari za kisiasa".

Ni mjinga tu asiyeweza kung'amua kuwa ndoto hizo ilikuwa tamko rasmi ya Lowassa kujitangazia kuwania urais, nje ya utratibu wa chama chake cha CCM.

Tumeona jinsi hata wachaguliwa wa wananchi walivyoweza kutumika ku-endorse ndoto za Mheshimiwa Lowassa, tena bila aibu.

Tumeona vile vile wanasiasa wa rika mbali mbali walivyojitokeza kupinga tamko la ndoto hizo za Lowassa , nje ya utaratibu wa chama, na tmemsikia Nape,Makonda, Magula na sasa mzee Malecela, wote wakiwa viongozi waandamizi ndani ya CCM.

Suala la ndoto za Lowassa hazikuibuka kama jua la asubuhi, bali limekuja baada ya yeye "kutoa misaada" mingi sana makanisani, misikitini, na hivi karibuni makundi ya vijana wa boda boda jijini Dar es alaam.

Taratibu za kawaida ZIMESHINDWA kumdhibiti Lowassa kwa vile sasa ni dhahiri CCM imegawanyika, haina tena ule mshikamano katika kudhibiti suala la Lowassa.

Kisa hiki kimenikumbusha scandal moja huko Marekani, iliyohusu uuzaji wa silaha kwa wapinzani wa serikali moja ambayo Marekani hawakuipenda sana.
Mauzo ya silaha hizo na operation yenyewe ilikuwa kinyume cha sheria, lakini kuna watu ndani ya serikali walifahamu mpango mzima.

Siki ya siku walipobanwa kisawasawa, msaidizi mmoja wa Rais Ronald Reagan alikuwa na ujairi wa kusema, The buck stops here with me".
Na kwa kweli huyo jamaa akakubali lawama zote pamoja na kuwajibika.

Sasa suala letu la Lowassa, inaelekea viongozi wote hadi ngazi ya Naibu Mwenyekiti CCM-Bara, Nd Mangula, jamaa ameshindikana!

Binafsi siamini kama kamati ya Nidhamu ya Chama itatoa maamuzi ambayo yanaweza kumtia hatiani Mhe Lowassa.

Na hapo ndo naamini kuwa The buck stops at the CCM chairmans' door step, Pres. Jakaya Kikwete, the ball is in your court.
 
Unachochea mnyukano mkuu??!! Au upo kambi ya Urambo ft Joka la mdimu??!!
Ccm wangeacha mpaka wakati wa mchakato wa mgombea ndio wachinje mbuzi wao wa shughuli!!!
 
haha..kumbe uliona eh...?JK bahati mbaya kakoleza moto..kasema..Wadhibitiwe...kwa hiyo tutawasikia sana vijana wakiropoka..kwani wakubwa wate wanasubiri sauti ziwe nyingi sana ili wajifiche humo ndani...
 
Unachochea mnyukano mkuu??!! Au upo kambi ya Urambo ft Joka la mdimu??!!
Ccm wangeacha mpaka wakati wa mchakato wa mgombea ndio wachinje mbuzi wao wa shughuli!!!
Hapana mkuu lakini kwa suala lenyewe lilipofikia, mada hii nasema kwa kiswahili rahisi, mwamuzi wa hatima ya Lowassa ni Mwenyekiti wa CCM.
 
Hapana mkuu lakini kwa suala lenyewe lilipofikia, mada hii nasema kwa kiswahili rahisi, mwamuzi wa hatima ya Lowassa ni Mwenyekiti wa CCM.
Maamuzi ya ccm siyo kama chadema kwamba mbowe na mtei wakiamua mtu afukuzwe lazima afukuzwe ccm ni vikao hutoa majibu yote.
 
NIlitegemea hilo kutoka kwa JK, Ukimya wa EL utamponza sana, aeshindwa kujipambanua kuwa ni mtu safi kwa kukaa kimya wakati akitupiwa tuhuma nyingi sana
 
Mchelea mwana kulia hulia yeye, EL si ulidokeza hakuna ambacho Mwenyekiti alikuwa hajui??? umeshindwa kusema ukweli achana na ndoto za urais, utadhalilishwa zaidi, ana kama uko serious sema ukweli wote.
 
Ndani ya CCM hakuna msafi hata mmoja, mtachofanya labda ni kutafuta mmoja wenu mwenye uchafu kidogo...
 
Hapana mkuu lakini kwa suala lenyewe lilipofikia, mada hii nasema kwa kiswahili rahisi, mwamuzi wa hatima ya Lowassa ni Mwenyekiti wa CCM.
Kwa jinsi CCM wengi wana kichaa..si haba kusikia fulani ni mamluki wa EL au wa CDM...watakimbia reality kuwa JK ndie alipaswa litolewa majibu..Ila JK atalifanya so ugly mapema sana.Akija amka mzee wa mitandao ndio ataamua hatia ya JK
 
Ni matatizo ya mitandao ndani ya chama. Kwa mazingira ya demokrasia ya sasa huwezi kuyazuia kabisa Bali kuweka mfumo wa kuhakikisha hayadhuru chama. Angalia mtandao ulianzishwa na nani na utajua jinsi ilivyo ngumu kwa mwenyekiti kutatua suala lenyewe.
 
Baada ya CHADEMA kumsimamisha Msaliti wao Zitto Zuberi Kabwe na wenzake wawili Samson Mwigamba na Kitilla Mkumbo kwa kosa la kuandaa Waraka wa kukivuruga Chama,,baadhi ya wana Ccm walishabikia na kushadadia kwa kusema kuwa Zitto kaonewa.
Walienda mbali zaidi na kuja na matamko km ZITTO KWANZA CDM BAADAE!

Leo kule Ccm kuna waka moto,mara tu baada ya kina Msindai na Msukuma kutoa tamko juu ya Lowassa,,juzi kijana mwingine aitwae Makonda nae katujia na yake.
Hatujakaa sawa Mzee Malecela nae akaibukia kwingine,swala ni lilelile la Lowassa,
Juzi tena akaibuka mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Shinyanga Hamisi Mgeja akimlalamikia Makonda na Malecela kwa hatua ya kumshambulia Lowassa.

Leo tena ameibuka mh Kikweta (mwenyekiti wa Ccm taifa) huko Mbeya kwenye sherehe za Ccm kuadhimisha miaka 37ya KUTUNYONYA Watanzania nae kwa stail ile ile ya kina Malecela na Makonda akimponda Lowassa japo hakumtaja jina lakini ukweli mlengwa wa hotuba yake hakua mwingine ila ni Lowassa!

Kwa matamko haya yote na sarakasi hizi za sasa ndani ya Ccm ni ishara tosha kuwa EDWARD NGOYAI LOWASSA ni zaidi Chama cha Mapinduzi.
Kwa maana hiyo basi ndani ya Ccm hakuna wa kumzuia Lowassa isipokua ni nje ya Ccm(CHADEMA) pekee ndio wenye uwezo wa kumzuia Lowassa asitimize ndoto zake.

LOWASSA KWANZA CCM BAADAE!!
 
CCM imezidi sana udini na ukanda......sas ammeshikiwa pabaya Lowasa anakubalika ktk misikiti na makanisa ya kiCCM CCM .
 
Hakuna atakayeshindana na chama hata siku moja wenye vihelehele watagota tu wala hamtafika kokote.
Kwa hilo nasubiri sana ...kusikia na kuona kwa CCM...mlidandia sana ya CDM na Msaliti Zitto....Lowasa hakuwahi isaliti CCM hata mlipoiba hela nyingi sana nchini.
 
Wanajamvi

Lowasa keshasema ameanza safari ya ndoto zake, na akasisitiza kuwa kwa nguvu za mungu atashinda. Hapa tunaona maudhui ya kauli ya Lowasa yamo kwenye hii theoretical concept ya 'safari', maana sio ajabu tafsiri ya 'safari' kwa Lowasa ni kubwa zaidi ya wengi tunavyofikiri, pengine ndio sababu Lowasa yupo kimya kabisa, hasemi lolote kuhusiana na wanaomrushia mawe, kumponda, kumnanga na kumdhihaki. Tunachoona ni kuibuka kwa conceptual institutions ambazo zipo zinazompinga kwa sauti kuu, na zipo zinazomuunga mkono bila kuuma maneno.

Hata hivyo taasisi ya CCM ni kama inaelekea kuelemewa na conceptual concept ya 'safari' toka kwa Lowasa, commentators nikiwamo mimi nasubiri kuona namna Lowasa, mwanasiasa nguli aliyelelewa kwenye misingi ya CCM atakavyofanikisha safari yake kwa nguvu za mungu hasahasa kwenye mazingira ambayo waliomlea, kumkuza na kumkubalisha kwa Watanzania wameanza kumkana kuwa hastahili kuwa miongoni mwao.

Tusubiri tuone

cc Masopakyindi
 
Maamuzi ya ccm siyo kama chadema kwamba mbowe na mtei wakiamua mtu afukuzwe lazima afukuzwe ccm ni vikao hutoa majibu yote.

Wewe sio bure lazima utakuwa umevurugwa na Mimba ya Mmoja wa wana CHADEMA
 
Maamuzi ya ccm siyo kama chadema kwamba mbowe na mtei wakiamua mtu afukuzwe lazima afukuzwe ccm ni vikao hutoa majibu yote.

hivyo vikao vitafanyika lini,tokea muanze kusema vikao vikao mbona hamchukui hatua,hv kweli lowasa ni mtu wa kukosa kuhudhuria bath day ya ccm.kweli nimeamini cdm ndicho chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu,
. lowasa is untouchable ndani ya ccm.
 
Back
Top Bottom