Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro atangaza kuachana na chama hicho! Ajiunga na CCM

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,462
29,163
DkTYSYXX4AA3d84.jpg

Julius Mtatiro, aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu na Moja kati ya wanachama mashuhuri zaidi wa CUF, ametangaza kujitoa katika chama hicho. Mtatiro amechukua uamuzi huo akiwa katika nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi ya chama hicho.

Julius Mtatiro ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kueleza kuwa ameanza kwa kuzungumza na waandishi wa Habari na kutangaza Azma yake ambayo ameitafakari kwa muda mrefu kabla ya kuwataarifu viongozi wa CCM ambao amewaomba wampokee.

“Nawaambia Watanzania kwamba kuanzia leo nitaanza kufanya siasa za maendeleo ili kumsaidia Rais John Pombe Magufuli" amesema mtatiro

===========

Habari zaidi....

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ametangaza kuachana na chama hicho leo Agosti 11, na kusema kuwa anatarajia kujiunga na CCM

"Nimejiridhisha kwa hitaji la Nafsi yangu kwamba nijiunge na Chama cha Mapinduzi CCM, nawajulisha watanzania rasmi kuwa nimeanza mipango ya kutekeleza hili mara moja"

"Siendi CCM kutafuta nafasi na ukuu uamuzi niliofanya ni uamuzi wa kutafuta jukwaa sahihi lakufanya siasa katika kipindi cha mbele cha maisha yangu"

Chanzo; Mwananchi
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ametangaza kuachana na chama hicho leo Agosti 11.

Taarifa Kamili zitakujia punde
 
Back
Top Bottom