Mwenyekiti uvccm taifa kwenda zanzibar ni uhuni wa jk

Warue

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
424
810
Si mara ya kwanza kwa chama cha mapinduzi kufanya maamuzi kinyume na kanuni wakiamini katika busara za mwenyekiti,baraza la vijana wa chama hicho hivi karibuni kabla ya kuanza mchakato wa uchukuaji form kwa wagombea wake lilipitisha nafasi ya mwenyekiti kurudi zanzibari huku kukiwa na imani ya kuwa mwenyekiti hakuwa amemaliza mda wake,nimejaribu kutafakari maamuzi hayo huku nikikumbuka maamuzi mazito ya kuwapata viongozi wa juu wa dola na chama na jinsi kanuni zinavyopindishwa, mapema mwaka 2008 katika uchaguzi wa jumuiya za chama hicho, mwenyekiti wa chama akishirikiana na wajumbe wa kamati kuu waliengua majina ya wagombea uenyekiti kutoka bara kwa kuwaweka katika nafasi ya makamu wakieleza kuwa makundi yalikuwa yamezidi hili si la kanuni ila tunaita busara za meza inayo ongozwa na jk,mwaka 2010 chama kikiwa kinafanya maamuzi mazito ya kumpata kiongozi wa moja ya miimili ya nchi bunge huku kikiwa ndicho chenye wabunge wengi zaidi kilipitisha maamuzi kuwa na spika mwanamke hii si kanuni ila busara za meza chini ya uongozi wa JK,hapa pia kulikuwa na utata uliokifanya chama kudharaulika na wengi,wengi tulijiuliza kama ni zamu ya wanawake wanaume wameruhusiwa kufanya nini? lakini swala si mwanamke ila mwanamke wa aina gani,kwanini wasinge tangaza mapema pengine wangejitokeza wanawake wengi na wazuri zaidi. mwaka huu pia jumuiya ya chama hicho imepitisha maamuzi ya nafasi ya mwenyekiti kwenda zanzibar hivyo bara kutoruhusiwa kushiriki,hivi huu si uhuni wa JK?
Swali:
  1. Hatamu za uongozi ni watu au miaka?
  2. Kuangushwa kwa mwenyekiti ndugu masauni ni kosa la wanachama au uongozi uliompitisha?
  3. Mbona kanuni haisemi juu ya mabadiliko ya viongozi kulingana na maeneo?
 
Umeanzisha thred mbili tofauti zenye maelezo yanayofanana ili upate wa kukuunga mkono bahati nzuri hapa ni great thinkers tumekustukia.
 
We upo kundi la mafisadi una uchungu wa kukatiwa mirija ya ufisadi.
 
Haya mambo ya kugawana kuwa hii ni zamu ya Zanzibar ama zamu ya wanawake inatuelekeza kubaya. Haitakuwa ajabu tukisiakia mwaka 2015 Urais kupitia CCM ni zamu ya Zanzibar ama zamu ya mwanamke. Bandubandu humaliza gogo!
 
mi nafikiri,nafikiri anayonia nzuri si dhani kama ni uhuni,isipokuwa ni kutokua na washauri wazuri,kwani bila ya kuwa na washauri wazuri dhamira njema inawezakuonekana vibaya machoni mwa wengi,kimsingi bila kuwa na mpango mzuri nyufa zinawezakutokea ambazo ni hasara kwa taifa. umenena vyema ila mfumo wenyewe umeutazama, mwenyekiti anaweza kukosolewa? au mpaka kukutana na dhoruba ya nje ya nyumba,mkuu nafikiri ulipost vibaya wakati bado unaediti kwani thread imejirudia lakini context ni ile ile.
 
Back
Top Bottom