Mwenyekiti UVCCM Taifa, Kheri James ateua wajumbe 6 kuhakiki mali za UVCCM

Deo Shy

Member
Oct 18, 2016
98
300
"Tunawashukuru Waandishi wa Habari kuwa bega kwa bega na UVCCM nyakati zote na hata wakati wa Mkutano Mkuu mlihakikisha taarifa zinafika kwa Wanachama, wapenzi, Watanzania na Dunia kwa ujumla." - Shaka

"Moja ya ajenda kuu aliyoanza nayo ni ya Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri James ni kuhakikisha anamuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na kuendana na matakwa ya UVCCM ni kusimamia rasilimali, vitega uchumi pamoja na vianzio vyote vya mapato vya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi" - Shaka

"Mwenyekiti Kheri amedhamiria kusimamia maslahi mapana ya CCM na ya UVCCM kwa kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo, kiutawala na kiundeshaji" - Shaka

"Sote tunafahamu UVCCM ndio kimbilio, ndio tumaini LA Vijana wote pasipo kujali itikadi wala hadhi zao toka UVCCM inaanzishwa mwaka 1978" - Shaka

"UVCCM imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia rasilimali za UVCCM nchini kote. Kamati hii ni maarufu kwa jina la "Kamati ya Makinikia UVCCM" - Shaka

"Wajumbe wa Kamati hii wanaoenda kuchunguza na kufuatilia rasilimali na Mali za UVCCM ni:-
1. Ndugu Mariam Khatibu Chaurembo - Mwenyekiti wa Kamati hii

2. Ndugu Peter Kasera - Mjumbe

3. Ndugu Zailote Saitoti - Mjumbe

4. Ndugu Rose Manumba - Mjumbe

5. Ndugu Sophia Kizigo - Mjumbe

6. Ndugu Elliah Ngowi - Mjumbe
" - Shaka

"Wajumbe wengine wawili (2) wataungana na wengine baadae Mara baada ya kutangazwa rasmi ili kukamilisha idadi kamili ya Wajumbe 8" - Shaka

"Kamati hii inaanza rasmi kazi Mara moja ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli. Kamati hii watapewa mwongozo ndani ya kipindi kifupi sana na watajulishwa namna ya kufanya kazi na hadibu za rejea zipo tayari." - Shaka

"Pindi watakapo kamilisha Kazi Watanzania na kila mtu watapata taarifa ya ripoti ya kamati hiyo" - Shaka

*Shaka Hamdu Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM* aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi ndogo Makao Makuu ya UVCCM Upanga Ijumaa Disemba 22, 2017

Imetolewa Na:

*Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa*
 
Ukisikia mihemko ndiyo hii UVccm wanatafuta mali ipi wakati kuna kamati nyingine imeundwa? Halafu ni mali ipi inayotafutwa wakati ccm haina mali yoyote?
 
Huku ni kurudia kichekesho kilichofanywa na mwenyekiti wa ccm taifa, wanaccm wakacheka saaana.

Sasa na uvccm mnataka wanaccm warudie kucheka. Haiwezekani. Njooni na cha kwenu, vinginevyo huu ni uzwazwa. Vijana kabisa mnarudia mawazo yaliyokwisha kufanyiwa maamuzi??

Hopeless kabisa!!
 
Ukisikia mihemko ndiyo hii UVccm wanatafuta mali ipi wakati kuna kamati nyingine imeundwa? Halafu ni mali ipi inayotafutwa wakati ccm haina mali yoyote?
Duuh we kweli makinikia... UVCCM ina mali nyingi sana sana....
 
Huku ni kurudia kichekesho kilichofanywa na mwenyekiti wa ccm taifa, wanaccm wakacheka saaana.

Sasa na uvccm mnataka wanaccm warudie kucheka. Haiwezekani. Njooni na cha kwenu, vinginevyo huu ni uzwazwa. Vijana kabisa mnarudia mawazo yaliyokwisha kufanyiwa maamuzi??

Hopeless kabisa!!
Sio kwamba kauli ya Rais ilikuwa muongozo. Na sio kurudia. By the way kurudia jambo kama ni jema sio mbaya
 
Ukisikia mihemko ndiyo hii UVccm wanatafuta mali ipi wakati kuna kamati nyingine imeundwa? Halafu ni mali ipi inayotafutwa wakati ccm haina mali yoyote?
Zamani ukiwa mfanyakazi tu unapoajiriwa unajaziwa fomu ya shirika la hifadhi ya jamii mfano PSPF,NSSF n.k na unajazishwa fomu ya vyama vya wafanyakazi,na unakatiwa na kadi ya CCM,na vyote hivyo unakatwa kwenye mshahara wako

Hapakuwa na namna nyingine ya kupata fedha za chama. Mfano kwa fedha hizo CCM ilitafuta maeneo na kujenga ofisi zake na viwanja vya mpira wa miguu,na kila mahali nchini.

Baada ya 1992, yenyewe ikaamua kubaki na mali hizo ikiacha vyama vingine vikianza moja!!
 
Siku utawala unahama kutoka CCM, hutu tu-mbwa twa CCM.tutalia mpaka tukojowe!! Maana hizi mali zote zitahamia serikalini!! Wajifunze kwa KANU yaliyowakuta!
 
Ebu rudisheni Mali za umma mlizozipora kwa nguvu wakati wa mfumo wa chama kimoja kama viwanja vya mipira, shule za wazazi n.k.
Umma ndo umepora mali za chama ama chama kimepora mali za umma??

Fatilia vyema utapata historia Ofisi Nyingi za Umma na majengo mengi ya serikali na vyuo vingine vilikua vya chama.

Afu ivi kwa mfano ofisi alizochangia Dr.Slaa au mbowe ujenz wake akijitoa Chadema mtamrudishia?? Mtampa portion gan wakati ule ni mchango shirikishi? Walizalimishwa kuhama? Wangebaki ili wawe sehemu ya kuendelea kufaid umiliki wa Mali hzo
 
Ukisikia mihemko ndiyo hii UVccm wanatafuta mali ipi wakati kuna kamati nyingine imeundwa? Halafu ni mali ipi inayotafutwa wakati ccm haina mali yoyote?
Kasome sheria ya baraza la wadhamini utajua kama ni za ccm au uvccm
 
Hawa tena ni wa nini wakati Mwenyekiti wa Chama Taifa alishateua Kamati?
Naomba kueleweshwa.
 
Hawa tena ni wa nini wakati Mwenyekiti wa Chama Taifa alishateua Kamati?
Naomba kueleweshwa.
 
Bavicha haya mambo mazuri hutayaona.

Wanachokijua ni kutetea ufisadi wa Lowasa na Sumaye tu.
Hujiulizi kwanini mali za CCM ndo inahakikiwa sasa toka enzi na enzi? Hapa katikati waliokuwa wanafisidi ni Bavicha? Acha upumbavu.
 
Back
Top Bottom