Mwenyekiti January Makamba amemkuna kamanda Mbowe kwa mchango wa kamati yake

MKWECHE

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
299
64
Jana kamati ya Nishati na Madini ilitoa hotuba yake kuhusu swala zima la Hali ya Umeme nchini!
Hadi mzee mbowe akatamani Mwana-Makamba angekuwa CDM!
 
Mkweche, injini itakuwa ishakufa hiyo naona mis zinakuwa nyingi.
 
Kuna kitu kinaniambia kuwaJanuary Makamba hakusema aliyosema jana kwa sababu ya kutaka kutatua tatizo la umeme, bali huo ni mpango wake wa kutaka kung'ara na pengine kupata nafasi kwenye baraza la mawaziri. Huyu kijana alikuwa mshauri wa Rais Kikwete kwa miaka mitano, alifanya nini au alimshauri vipi Rais kutatua tatizo la umeme? Why now anaonekana kulivalia njuga swala la umeme na sio wakati akiwa Ikulu sehemu ambayo naamini ndio chimbuko la matatizo yote tuliyonayo? Na mara January alipopata uenyekiti wa kamati ya Nishati alijigeuza kuwa 'msemaji' wengine walimuita 'dalali' wa Dowans!

Kwa maoni yangu, Ngeleja anaweza na naamini ana mapungufu yake lakini January hana track-record ya kuaminika kwenye issue ya umeme hapa nchini. Sanasana naweza kusema anaonesha tabia ya 'work-colleagues' wenye tabia ya kuwavizia wenzio kwa kuanika kila kosa ili mradi tu wao wang'are na pengine kupanda cheo! Dangerously ambitious!
 
upinzani sio kupinga kila kitu.kama kweli Mbowe kakubali basi dogo atakuwa alimwaga pwenti!
 
NYANI KIJANA ANAJIFUNZA MAMBO YA NYANI MZEE,DOGO NI MNAFKI TUU NA MLAFI WA MADARAKA ANAMPIGA VITA NGELEJA ILI APEWE UWAZIRI WA NISHATI NA MADINI KAGUNDUA KUNA HELA NJE NJE

hana jipya
 
jamani ,nyonge mnyongeni haki yake mpeni!! ngeleja ana uwezo wa kuchapana mangumi na walinzi wa ATM tu hana uwezo wa upstairs kama january!

ukichunguza kuna disparity kubwa kati ya wazee na vijana yanapokuja masuala ya maslahi ya taifa!
 
Mkweche, injini itakuwa ishakufa hiyo naona mis zinakuwa nyingi.

Ndugu yangu Ecoli mie Mkweche Umeme wenu Sitaki,mara wa Richmond,mara Dowani mara Symbion Niemeshaachana Nao Muda!
Walkman yangu Inatumia Bettery Mkweche! Na betteri ina Kilo 15 baibeba Kichwani!Nikiwa home pande za Igangidungu Iringa natumia betri hili kwa Taa
Ndo mana hata Mgao wa umeme maanake siijui!
 
Kuna kitu kinaniambia kuwaJanuary Makamba hakusema aliyosema jana kwa sababu ya kutaka kutatua tatizo la umeme, bali huo ni mpango wake wa kutaka kung'ara na pengine kupata nafasi kwenye baraza la mawaziri. Huyu kijana alikuwa mshauri wa Rais Kikwete kwa miaka mitano, alifanya nini au alimshauri vipi Rais kutatua tatizo la umeme? Why now anaonekana kulivalia njuga swala la umeme na sio wakati akiwa Ikulu sehemu ambayo naamini ndio chimbuko la matatizo yote tuliyonayo? Na mara January alipopata uenyekiti wa kamati ya Nishati alijigeuza kuwa 'msemaji' wengine walimuita 'dalali' wa Dowans!

Kwa maoni yangu, Ngeleja anaweza na naamini ana mapungufu yake lakini January hana track-record ya kuaminika kwenye issue ya umeme hapa nchini. Sanasana naweza kusema anaonesha tabia ya 'work-colleagues' wenye tabia ya kuwavizia wenzio kwa kuanika kila kosa ili mradi tu wao wang'are na pengine kupanda cheo! Dangerously ambitious!

Mheshimiwa FJM, January Makamba hakuwa mshauri wa Rais Kikwete, yeye alikuwa ni Personal Assistant to the President – Special Duties (PAP-SD) na kama presidential aide, kazi yake pia ilikuwa kukaa na kuchukua notes wakati Rais anaongea/kukutana na dignitaries
 
Pumba. tangu lini makamba akawa mshauri wa rais. Akiwa mwenyekiti wa nishati na amdini unataka akae kimya tu ili akufurahishe hata kama mambo yanaenda kombo. Wewe utakuwa Zezeta.
 
Mheshimiwa FJM, January Makamba hakuwa mshauri wa Rais Kikwete, yeye alikuwa ni Personal Assistant to the President – Special Duties (PAP-SD) na kama presidential aide, kazi yake pia ilikuwa kukaa na kuchukua notes wakati Rais anaongea/kukutana na dignitaries
huwezi kuchukua notes kama type writer, kumbuka hata madereva ni washauri wazuri tu

you cant delineate january makamba na kikwete regime

to me, january had more to do with lots of stuffs, including mbayuwayu speech
 
ndani ya ccm siyo kuwa wote awafai ila ni mfumo ni mbovu
sana awafai tatizo ni mfumo mbovu wa chama cha magamba
 
ndani ya baraza la mawaziri waziri makini yuko mmoja tu mhe pombe magufuli
yule mama alijaribu kuja juu na kuvunja kuta za watu yuko wapi au likizo mama
wa mazingira, viwanja vya wazi vinaporwa na kujengwa lakini wap kimya
viwanja vya shule vinavyamiwa, wapi kimya magambo magamba ipo
siku inakuja na si nyingi mtakaaa kama chama cha wapinzani na mtajibu,
nyumba za serikali mmejiuzia ostabey iliyokuwa inaheshiimika kila nyumba ni
bar na gyst bubu inauma sana lakini tunasema madikiteta wengi wanashitakiwa
ipo siku itafika na kuna MUNGU asiyependa dhuluma MUNGU siyo wa mafisadi
tu kama mnavyotaka na kukiita chama chenu chama cha MUNGU ipo siku
ipo karibu,

kiikupacho raha na uchungu kitakupa
 
jamani ,nyonge mnyongeni haki yake mpeni!! ngeleja ana uwezo wa kuchapana mangumi na walinzi wa ATM tu hana uwezo wa upstairs kama january!

ukichunguza kuna disparity kubwa kati ya wazee na vijana yanapokuja masuala ya maslahi ya taifa!
Katika context ya post yako, yupi ni Mzee?
 
jamani ,nyonge mnyongeni haki yake mpeni!! Ngeleja ana uwezo wa kuchapana mangumi na walinzi wa atm tu hana uwezo wa upstairs kama january! Ukichunguza kuna disparity kubwa kati ya wazee na vijana yanapokuja masuala ya maslahi ya taifa!
anatafuta uwaziri huyo, hata ngeleja si mzee ccm lao moja
 
Jana kamati ya Nishati na Madini ilitoa hotuba yake kuhusu swala zima la Hali ya Umeme nchini!
Hadi mzee mbowe akatamani Mwana-Makamba angekuwa CDM!

huyo mbowe ni kamanda wa nini? Jeshi mgambo au sungusungu? Na hiyo mzee ni jina lake cheo au nin?
 
uo ni mpira wa kona!!!
watagombana sana mwisho watajua sisi watz tunataka nini<<<<<
 
Aaaah wote wanafki tu!huyo nae akipewa cheo utaona makucha yake kama mwenyekit wa kamati teule ya richmond na mzee six wote kwishney wanaonesha rangi zao.
 
Back
Top Bottom