Mwenye CV ya Novatus Makunga atuwekee humu JF tuifahamu...

CCM wajanja sana hii yote ni kuwafanya wanahabari njaa waanze kuegemea CCM wakifikiria kuja kuulamba ukuu wa Wilaya msije kushangaa siku eti invisible kawa mkuu wa wilaya.
 
Ni kilaza wa nguvu,a know wel by the time ni mtunza stoo pia wa AICC.hana IQ hata ya kuzaliwa kusuluhisha kesi.ana mdogo wake aitwae Ernest Makunga aliwahi kuwa mtandao wa Jk,alitegmea udc mwaka 2005 bt sasa ivi jk amempa asimamie miradi yake bagamoyo.
Mkuu,
Kipindi hicho nilikuwa naishi nyumba moja ya kupanga na huyu mdogo wake eneo la Sakina Silent Inn!..Dogo alikuwa na maconfidence sana ya kukamata u-dc kutokana na kuwa M*KWERE tu, kabila la mzee. Baada ya majina kutangazwa akiwa hayumo alihama mtaa kabisa!, na baadaye akachaguliwa kuwa kamanda wa vijana wa Wilaya ya Bagamoyo!
 
Mnatafuta CV yake ya nini? Kwani mliambiwa ili uwe DC unatakiwa kuwa na elimu kiasi gani? Msipoteze muda, itoshe tu kuwa jamaa anajulikana kuwa ni mwandishi wa habari. Kwanza kazi za DC ni zipi?
 
Ni kilaza wa nguvu,a know wel by the time ni mtunza stoo pia wa AICC.hana IQ hata ya kuzaliwa kusuluhisha kesi.ana mdogo wake aitwae Ernest Makunga aliwahi kuwa mtandao wa Jk,alitegmea udc mwaka 2005 bt sasa ivi jk amempa asimamie miradi yake bagamoyo.

jamani sijui ni wivu,ushamba ama ujinga,usifanye udharauliwe makunga alikuwa pro aicc na mdogo wake ni katibu wa uvccm mkoa wa morogoro mwogope mungu kwa kudanganya kama hujui kitu kaa kimya
 
jamani sasa ebu tupate cv za waandishi wa habari wengi wateule wa udc kuwa wametoka wapi na nani katika siasa za nchi hii kuanzia jackline liana,mahingo rweyemamu,ahmed kipozi na somebody mwalimu,betty mkwasa,sarah dumba na halima kihemba
 
Last edited by a moderator:
Viongozi kushindwa kuweka CV zao hadharani inapelekea kushamiri kwa 'madudu' mengi katika taasisi mbalimbali za umma. Viongozi hawajulikani, wengi wao elimu zao ni za ku-unga unga..tumeona wenyewe mjadala wa CV ya Waziri wa Afya (Mwinyi). Ajabu zaidi wadau wakiomba hizo CV ziwekwe hadharani wanakuja watu kama komeo na kuwakatisha tamaa...sasa bila CV ya kiongozi wa umma, je utawezaje kufahamu leadership skills zake, na accomplishment ya mtu uliyempa dhamana ya kukuongoza!? Nawaomba wanaJF tuache kuwa wavivu wa kufikiria na kuishia kukatishana tamaa. Tukumbuke kwamba, msingi mkuu wa kizazi hiki ni utandawazi huku chachu ikiwa uwazi na uwajibikaji... kubebana bebana bila sifa na vigezo matokeo yake ni mauza-uza yanayojiri kwa caesar kila kukicha!
 
Mkuu,
Kipindi hicho nilikuwa naishi nyumba moja ya kupanga na huyu mdogo wake eneo la Sakina Silent Inn!..Dogo alikuwa na maconfidence sana ya kukamata u-dc kutokana na kuwa M*KWERE tu, kabila la mzee. Baada ya majina kutangazwa akiwa hayumo alihama mtaa kabisa!, na baadaye akachaguliwa kuwa kamanda wa vijana wa Wilaya ya Bagamoyo!

Namkumbuka dc mteule Novatus Makunga aliwahi kujitosa kuwania ubunge wa Kibaha mjini kupitia chama cha magamba mwaka 2005 akaishia kuburuzwa kwenye kura za maoni.
 
mojawapo ya cv zao ni kuriport vizuri habari nzuri za kigambagamba! ushahidi mmojawapo ni uteuzi wa Novatusi! alipendelea sana kuriport mikutano ya magamba juzi kwenye kampeni za Arumeru na kuwabania cdm lakini Mungu akasimama kati na haki ikaenda kunako! nakumbuka kuambiwa kuwa nova alikuwa anajipigia debe la kupata udc sikuamini lkn sasa unaonaje?
 
Bottom line Ni Mtangazaji wa ITV akiripoti kutoka Arusha na amekuwa akiripoti habari za kampeni za uchaguzi kwa upande wa CCM kuanzia uchaguzi mkuu mpaka uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru.

Mytake: Issue ya Education background kwa hili potezea!
 
Ukishakuwa mtumishi wa uma kama dc lazima watu tujue wametuletea mtu wa aina gani kielimu na kisiasa,embu weken CV ya huyo bwana hapa.
 
Cyprian majura musiba kajitahidi kujipendekeza kwa ritz 1 kule facebook lakini kamwagwa nimeamini huhitaji cv kuwa dc tanzania,musiba alikuwa anakomaaa anaongea ujinga ujinga kukitetea chama chali nimeipenda hii!!!!!!!!!!!!!!
 
Mimi nilisoma nae pale chuo cha Diplomasia alisoma certificate international relations anda Diplomacy, mwaka 1999 - 2000 alirudi tena chuo cha Diplomasia na kuchukua stashahada ya uhusiano wa kimataifa na diplomasia.nilikuwa nae Darasa moja napingana na wanJF wengine wanaosema ni kilaza ni mtu anayejiweza tu katika kujieleza hata pale chuoni alikuwa ni miongoni mwa mawaziri wa chuo sikumbuki vzr wizara gani lkn ni mwelewa wa mambo, ni mzuri kwa lugha ya kispanish,
mnyonge nyongeni lkn haki yake mpeni!!!!!!!:flypig:
 
Back
Top Bottom