Mwenge wa Uhuru Wazindua Miradi ya Bilioni 2.2 Wilaya ya Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Septemba 16, 2023 umepokelewa Wilayani Kaliua, ukitokea Wilaya ya Tabora na kuanza kukimbizwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa ajili ya kukagua,kuona, kuzindua pamoja na kuweka Mawe ya Msingi katika miradi sita (6), ya Maendeleo ikiwemo ya Elimu, Afya, Maji na Barabara yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.2

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Mhe. Dkt. Rashid Chua Chua aliupokea Mwenge huo ambao Septemba 15, 2023 ulikimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora umbali wa kilomita 60 na kuzindua miradi sita (6) yenye thamani ya Bilioni 2.5.

Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2, katika Halmashauri zote nane (8) na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.

Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Kaliua akiwa sambamba na Mhe. Rehema Migilla, Mbunge wa Ulyankulu katika mapokezi ya mbio za Mwenge Kata ya Mwongozo,Wilaya ya Kaliua ambapo Mwenge unatarajia kuzindua miradi mbalimbali pamoja na kukesha Mjini Kaliua,ni kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi Mwangaza.

MWENGE WA UHURU WILAYANI KALIUA - MWENGE WA UHURU UMEZINDUA MRADI WA DARAJA ICHEMBA- NHWANDE

MWENGE WA UHURU WILAYANI KALIUA - Mbunge wa Jimbo la Kaliua Ndg Aloyce Kwezi akiwa amebeba Mwenge wa Uhuru katika Kata ya Mwongozo.

MWENGE WA UHURU WILAYANI KALIUA - MWENGE WA UHURU WAZINDUA SHULE YA MSINGI DKT. SAMIA

Kauli Mbiu ni "Tunza Mazingura, Okoa Vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi wa Taifa.

WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.47(2).jpeg

WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.48.jpeg

WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.43.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.38(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.33.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.36.jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.39(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.36(1).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-18 at 15.20.46.jpeg
    51.9 KB · Views: 2
Namuona Kijana makini kabisa ambaye ni mbunge Wa Kaliua.... Safi sana Mheshimiwa Aloyce Kwezi wewe ni kijana wa mfano wa kuigwa hasa katika kupigania maendeleo ya jimbo lako.
 
Back
Top Bottom