Mbunge Aloyce Kwezi: Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2024 - 2025 Serikali Ijenge Barabara ya Mpanda - Kaliua - Kahama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE ALOYCE KWEZI: MPANGO WA MAENDELEO YA TAIFA 2024-2025 SERIKALI IJENGE BARABARA YA MPANDA - KALIUA - KAHAMA

"Nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kujenga Taifa letu. Nawapongeza Mawaziri, Komredi Mwigulu Lameck Nchemba na Professor Kitila Mkumbo kwa kazi nzuri walizonazo, sisi watanzania tunazion kwa macho na hatuna haja ya kusimuliwa" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Tuliomba Barabara ya kutokea Mpanda - Kaliua - Kahama ambayo inapitia mikoa mitatu. Maeneo yetu tunazalisha sana Tumbaku, Mpunga, Mahindi na mengine. Uwepo wa barabara hii kiuchumi tutaweza kuuza mazao kwa bei kubwa" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Barabara kiuchumi tutakuwa na uwezo wa kusafirisha mazao kama Mchele tunauza Uganda 🇺🇬, Rwanda 🇷🇼. Mzunguko wa kuitafuta Nzega unakuwa umekwenda nje ya Kilomita 250. Ushauri kama huu mkiuzingatia tutakuwa na Mipango mizuri na endelevu" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Barabara ya Mpanda - Kaliua - Kahama Kwenye Ilani ya CCM 2010 - 2015 ipo, 2015 - 2020 ipo na 2020-2025 ipo. Nashauri tuwe na utashi na mambo ya Msingi, tunaweza kuwa tuweka Mipango ambayo haitekelezeki ikaishia kwenye maneno na siyo kwenye vitendo, tutapata shida" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Tuna wasomi wa kutosha Bungeni lakini usomi pekee yake hautoshi kwasababu usomi ni kitu kingine na utendaji ni kitu kingine. Nawashauri Mawaziri wahakikishe wanaingiza Ushauri wa Wabunge kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2024 - 2025 ikiwemo barabara ya Mpanda - Kaliua - Kahama" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Kuna maeneo pana idadi kubwa ya watu hatujazingatia miradi mikubwa tupeleke. Utakuta maeneo yenye idadi ndogo ya watu yana miradi mikubwa wakati kuna mahali ambapo pangekuwa na Mzunguko mkubwa wa biashara na fedha" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Jambo la SGR naomba tuliunge mkono kwasababu njia nyepesi ya usafirishaji kuziokoa barabara ni pamoja na Reli. Maamuzi ya kujenga Reli ya SGR hususani Tabora - Kigoma, Kaliua - Mpanda ambayo inakwenda kuinua mishipa ya kiuchumi ili wananchi wapate pato na Taifa lipate pato" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.

"Tuna hifadhi za Taifa nyingi karibu 22, kipindi cha masika zinafikika? Tutakuwa na Utalii wa kiangazi tusubiri Mvua ikikata? Tupeleke fedha kwenye ujenzi wa hoteli za kutosha, barabara za kutosha" - Mhe. Aloyce Andrew Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua.
 
Alivyopongeza tu sijataka hata kusoma tena, pesa ni mali ya watanzania, nilitegemea apongeze walipa kodi. Shame on him
 
Back
Top Bottom