Mwanza: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa kufanya maandalizi ya mkutano wa hadhara

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,225
219,401
Huku Kinana, Hamdu Shaka na Chongolo wakiendelea na mikutano ya hadhara nchi nzima, leo viongozi wa Chadema huko Mwanza wamekamatwa wakiwa kwenye maandalizi ya Mkutano halali wa hadhara, kwa nia ya kuongea na wanachama wao ambao wanakadiriwa kuzidi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa Mwanza.

Miongoni mwa Waliokamatwa yumo Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mh David Nyakimwe na Mwanachama wa chama hicho ndugu Oswald Mang'ombe.

Katiba ya Tanzania inatoa haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano bila kikwazo chochote , hawa wanaozuia haki hii ya kikatiba wanatumia katiba gani?

Chama cha siasa ni mabarabarani na majukwaani - JK Nyerere.

FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Huku Kinana , Hamdu Shaka na Chongolo wakiendelea na mikutano ya hadhara nchi nzima , leo viongozi wa Chadema huko Mwanza wamekamatwa wakiwa kwenye maandalizi ya Mkutano halali wa hadhara , kwa nia ya kuongea na wanachama wao ambao wanakadiriwa kuzidi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa mwanza .

Miongoni mwa Waliokamatwa yumo Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mh David Nyakimwe na Mwanachama wa chama hicho ndugu Oswald Mang'ombe .

Katiba ya Tanzania inatoa haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano bila kikwazo chochote , hawa wanaozuia haki hii ya kikatiba wanatumia katiba gani ?

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .

View attachment 2345719
Nilitoka kumwambia mwana chukua chako mapema (ccm) Leo wao kama SII police na Dola hata historian yao ingesha kuwa imefutika kabisa duniani humu na isingepatikana hata makumusho yeyote duniani 🤔
 
Huku Kinana , Hamdu Shaka na Chongolo wakiendelea na mikutano ya hadhara nchi nzima , leo viongozi wa Chadema huko Mwanza wamekamatwa wakiwa kwenye maandalizi ya Mkutano halali wa hadhara , kwa nia ya kuongea na wanachama wao ambao wanakadiriwa kuzidi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa mwanza .

Miongoni mwa Waliokamatwa yumo Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mh David Nyakimwe na Mwanachama wa chama hicho ndugu Oswald Mang'ombe .

Katiba ya Tanzania inatoa haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano bila kikwazo chochote , hawa wanaozuia haki hii ya kikatiba wanatumia katiba gani ?

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .

View attachment 2345719
Mungu ibariki CHADEMA
 
Hapo ndipo mtathibitisha yale maridhiano na CCM ni maigizo tu, na ile Katiba Mpya waliyosema wataileta nayo ni maigizo vile vile..

Samia hayupo serious, Kinana pia ni mnafiki anayejidai kuleta usawa wa uongo, na CCM haipo serious.

Kuendelea kukaa kimya kwa viongozi wa Chadema wakijidanganya wanampa muda mama wa kushughulikia mapendekezo yao ni ujinga.
 
Waache kushindana na CCM hao, utajilinganishaje na mh Shaka au mh kanali Kinana wakati unajuwa hao ndio wenye ilani na Wana haki ya kupita kukagua utekelezaji wa ilani, Sasa hao chadema wanataka wakaongee Nini?

Au wanataka wakapige kelele za uongo uongo Kama kawaida yao, au wanataka picha za kupeleka kwa wafadhiri wao, watulie kwa Sasa wamuache mama yetu awatumikie watanzania kwa amani na utulivu,

Hatutaki chokochoko, wasubiri uchaguzi ndio wakaombe kura, Sasa Ni uwanja wa CCm kufuatilia utekelezaji wa ilani yake
 
kwa ibara ipi ya katiba ya Tanzania ? , halafu ile mikutano anayoifanya Kinana ameruhusiwa na nani ?
Usishindane na mwamba Kinana,Yule Ni msimamizi wa ilani yupo anafuatilia utekelezaji wake katika Yale yalio tolewa Kama ahadi, Sasa nyinyi chadema mnataka mkaongee Nini?

Nyinyi mlikataliwa kwenye sanduku la kura, Tulieni maana watanzania walishawapuuza kwa Sasa
 
Usishindane na mwamba Kinana,Yule Ni msimamizi wa ilani yupo anafuatilia utekelezaji wake katika Yale yalio tolewa Kama ahadi, Sasa nyinyi chadema mnataka mkaongee Nini? Nyinyi mlikataliwa kwenye sanduku la kura, Tulieni maana watanzania walishawapuuza kwa Sasa

Si ndio ilikuwa vizuri CDM waachiwe waongee na wananchi ili ionekane jinsi wananchi walivyowapuuza?

Hakuna kitu kigumu kama kutawala watu kwa shuruti, ukiona tu anayekubalika anataka kuongea na wananchi, unaogopa unajua utazidi kupuuzwa.
 
Huku Kinana , Hamdu Shaka na Chongolo wakiendelea na mikutano ya hadhara nchi nzima , leo viongozi wa Chadema huko Mwanza wamekamatwa wakiwa kwenye maandalizi ya Mkutano halali wa hadhara , kwa nia ya kuongea na wanachama wao ambao wanakadiriwa kuzidi zaidi ya nusu ya wakazi wote wa mwanza .

Miongoni mwa Waliokamatwa yumo Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Nyamagana Mh David Nyakimwe na Mwanachama wa chama hicho ndugu Oswald Mang'ombe .

Katiba ya Tanzania inatoa haki kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano bila kikwazo chochote , hawa wanaozuia haki hii ya kikatiba wanatumia katiba gani ?

CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .

View attachment 2345719
Na huu ni mkakati maalum Kuhakikisha kwamba ktk mazingira yaliyopo aliye na uwezo wa kuchota fedha za umma awezavyo achote tu maana wakati ndio huu.
 
Si ndio ilikuwa vizuri CDM waachiwe waongee na wananchi ili ionekane jinsi wananchi walivyowapuuza? Hakuna kitu kigumu kama kutawala watu kwa shuruti, ukiona tu anayekubalika anataka kuongea na wananchi, unaogopa unajua utazidi kupuuzwa.
Huwezi kuwaacha watu wasiojuwa namna ya kutumia midomo yao, CCM ndio yenye dhamani ya usalama wa Taifa hili kwa hiyo huwezi kuwaendekeza watu Kama Chadema wakafanya wanavyotaka.

Ni hatari kwa usalama wa Taifa maana wao huongea lolote tu linalowajia katika midomo yao bila hata kulichuja, si unaona watu mam akina mdude wanavyoongea maneno ya shombo?
 
Tulisema yale maridhiano ya Mbowe na Samia ni utapeli mtupu. Lengo ilikuwa ni kuhadaa umma kuwa kuna maelewano ya kisiasa kwa faida ya mama Samia.

Naendelea kusisitiza, bila machafuko tusitegemee usawa na haki kutendeka. Kenya heshima imekuja baada ya machafuko. Ccm imeshapoteza ushawishi, haiko tayari kukubali ushindani wakati inajua itapoteza.
 
Huwezi kuwaacha watu wasiojuwa namna ya kutumia midomo yao, CCM ndio yenye dhamani ya usalama wa Taifa hili kwa hiyo huwezi kuwaendekeza watu Kama Chadema wakafanya wanavyotaka, Ni hatari kwa usalama wa Taifa maana wao huongea lolote tu linalowajia katika midomo yao bila hata kulichuja, si unaona watu mam akina mdude wanavyoongea maneno ya shombo?

Mtu anayeongea maneno ya shombo sheria zipo. Na kama wamepuuzwa si ndio vizuri wapuuzwe zaidi? Magufuli aliwaambia watu hadharani kuwa wabaki na mavi yao nyumbani, je alizuiwa kufanya siasa?

Ukweli uko hivi, hofu ya CCM kwa CDM ni mvuto, CCM inajua fika CDM ndio yenye mvuto na ndio wananchi wanawasikiliza, hivyo wakitoa mwanya wanawapoteza. Njia pekee ni kutegemea mbeleko ya vyombo vya dola
 
Usishindane na mwamba Kinana,Yule Ni msimamizi wa ilani yupo anafuatilia utekelezaji wake katika Yale yalio tolewa Kama ahadi, Sasa nyinyi chadema mnataka mkaongee Nini? Nyinyi mlikataliwa kwenye sanduku la kura, Tulieni maana watanzania walishawapuuza kwa Sasa
Walipata Kura 0 ?, Kama kuna watu waliwachagua, na Kinana anaruhusiwa basi na hawa waruhusiwe...., pili unasema watu wanawakataa kwahio basi si muwaache sababu watakuwa wenyewe peke yao (viongozi) bila raia wa kuwasikiliza...,

Huku kutumia kodi zetu na kuzifuja hata kwa Rais kufanya kampeni zaidi ya utekelezaji ni aina ya Ufisadi (kutumia Kodi kwa manufaa ya Chama na sio Nchi)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom