Mwanaume ukikosa hela, mpenzi wako atachukuliwa mbele ya macho yako

Leverage

JF-Expert Member
Jan 25, 2021
2,125
3,134
UDSM, 2010 saa moja na nusu usiku nipo dirishani hall 6 nachungulia dirishani. Ghafla anashuka Dada mmoja kutoka juu ghorofa ya kwanza anakutana na kijana mmoja aliyeonekana amebeba mfuko wanakumbatiana na kwenda kukaa kwenye nyasi.

Kijana anafungua mfuko na wote wanaanza kula nadhani ni chips. Zilipita kama dakika 20 gari ikaingia aina ya Verossa/Mark X sina hakika sana Ila ni muundo huo.

Ghafla naona yule msichana kasimama kaenda kwenye ile gari jamaa katoka wakakumbatia akamfungulia mlango demu akaingia gari ikaamsha.

Jamaa wa chips alisimama zaidi dakika 30 akiisindikiza gari kwa macho hadi ilipoishia bado amesimama pale na chips zake mkononi. Niliumia sana kama vile lile tukio limenitokea mimi.

Nikatoka nje na kumtia moyo mshakaji the man was depressed.
 
Back
Top Bottom