Mwanaume kakuzalisha halafu hataki kutoa barua

Kweli adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake! Wanawake ndio wanaoongoza kwa kuleta upinzani na vizingiti ktk kufikia usawa wa kijinsia. Ona huyu anasema alizalishwa, jamani hata ng'ombe hawezi kupandwa kama hajapata joto!Atarusha mateke na kukimbia, sembuse binadamu azalishwe!

Inaonekana hata hiyo mimba hamkupanga na kujadiliana pamoja, ulimtegeshea ili ukiwa na mtoto akuonee huruma na kukuoa! Ungekuwa na busara, ungesubiri uolewe kwanza ndipo uzae. Tatizo la dada zetu mnaona kuolewa ni lazima ktk maisha,kiasi kwamba hata yule ambaye hayupo tayari analazimisha ili mradi aondoe "gundu" la u-single! Mwanaume lazima machale yamcheze maana anaona kila siku anakumbushiwa kuhusu ndoa!
 
nahisi unyanyasaji wa kijinsia hapa. mwanamume kakuzalisha??? kwani wewe hujamzalisha??? wote mmezalishana-hii ndo statement nzuri kutumia na mpaka hapo utakapoibadilisha ndo nitachangia mawazo tena mazuri kabisa ambayo yatukua msaada kwako
 
mwanaume kakuzalisha mtoto halafu hataki kutoa barua,ukimwambia kajitambulishe kwa wazazi hataki na anataka kuendeleza uhusiano. Je, huyo mwanaume ni mkweli au anataka kunipotezea muda tu. Tuna miaka mitano kwenye uhusiano.

Naupinga huu MFUMO JIKE wa kumsingizia mwanaume kwa kila uamuzi wa hiari anaoufanya mwanamke. Hivi mpaka mnakubaliana kwa hiyari yenu, unapanda kitandani, unapata mimba na kuzaa mtoto halafu unaendeleza libeneke kwa miaka mitano hukuwahi kukumbuka masuala ya barua kwa wazazi? Kama alikubaka sawa lakini kama mlikubaliana kwa hiyari yenu mfanye ile starehe ya kiutu uzima basi MLIZALISHANA wote wawili.
 
Ukiufuta ushauri wa humu JF imekula kwako. Ushauri wa humu kuwa nao makini sana. Wewe ndio unajua qualities zake jamaa hadi mkadumu miaka yote hiyo mitano. Sasa hapa watakuchanganya wee mara hivi mara vile, wewe amini akili yako tu katika hili.
 
Hivi mtu kama unapewa lift kila siku, tena wakati wowote unaohitaji kuna sababu ya kununua gari?????


Ushauri wangu,

Hebu funga hilo bomba linalomlewesha kila siku kwa kukata kiu yake walau kwa muda uone kitakachofuate....Kama atahangaika kuomba umsaidiea kulifungua basi huyo ni wako ila kama atauchuna basi uje hilo ndo jibu lake la siku nyingi!
 
Wadada wengi sikuhizi wana kasumba ya kutulengesha mimba ili kuhahalisha ndoa. Narudia tena, Mimba haihalalishi ndoa, you are very wrong!
 
kwani mtu akikuzalisha ni lazima akuoe? mbona wanaume wengi tuu kama unataka kuolewa? acha kumganda mtu bwana huyo akutaki
 
Furahia mtoto wako bibie, mwambie kama hana hakika na wewe muachane, anza date vijana wengine, kama ana nia na wewe atarudi mbio na kleta posa, asiporudi jua kashukuru umeenda, so lazima wewe kuzaa ndio iwe tiketi ya kuolewa
 
pole sana mrembo, lakini inaonekana bado hujajitambua, uko na kwenye uhusiano five yrs,bwana hajaleta barua ya kutaka kukuoa,so ukaamini labda ukibeba mimba atachange mind yake??? unless kama hiyo mimba mlikubaliana kama hamkukubaliana u were very wrong to do that,yaani wewe uliona kabisa jamaa hana msimamo kuhusu ndoa yet u went further kubeba mimba yake!!? sory to say this bt umejitakia mwenyewe
 
mwanaume kakuzalisha mtoto halafu hataki kutoa barua,ukimwambia kajitambulishe kwa wazazi hataki na anataka kuendeleza uhusiano. Je, huyo mwanaume ni mkweli au anataka kunipotezea muda tu. Tuna miaka mitano kwenye uhusiano.

Too late. Hivi huwa mnategemea nini mnapowavulia nguo kabla hawajawaoa? They need you more than you need them (kabla ya kuwavulia nguo).

Sasa wewe ulie tu. Huna cha kufanya na wala si wa kuonewa huruma, kabla kumvulia nguo ulikuja humu au kwenda kwa wazazi wako kutaka ushauri? Huyo mwanamme hakukuzalisha aliyekuzalisha daktari au nurse, huyo kakujaza mimba kwa kutaka wewe mwenyewe na pengine ulikuwa unaulilia "tamu, tamu, tamu". Haya sasa, huo utamu uko wapi? Mnaudhi kwa kuwashwashwa kwenu halafu yakishawafika mnajidai kutaka kutaka ushauri. Kwani ulikuwa hujui kuwa kuna mimba? maradhi? Ukimwi, kutunza mimba? kulea mtoto? kama yite ulikuwa unayajuwa, sasa lea mtoto wako na usilalamike.

Next time be extra careful. Kuanzia leo, badilika u save situation. Kuwa mgumu na usimchekee, usikubali chochote kutoka kwake mpaka atakapo kuoa. Your first and foremost condition should be that, always. Na kwa nyie wasichana wengine wote, usimvulie nguo mpaka akuoe na kabla ya ndoa mkapime kama ni mzima wa magonjwa yote na mzima wa akili. Ukishayajuwa hayo uamuzi ni wako. Akiwa mzima akiwa mgonjwa utaamuwa wewe kama upo tayari kuishi nae kwenye ndoa au la.
 
Back
Top Bottom